Kwenye mkataba nimemwandika kama mrithi Ila yeye kamwandika baba yake

Umeanza vizuri nikahis uko Upande wangu.....huku mwisho sasaaa
 
Unajiangaisha bure tu, wewe ndio utaanza kufa na yeye ndio mrithi hata usipomuandika kwenye makaratasi, mahakamani mirathi atapewa mke wako na watoto.

Nina uhakika mkubwa wewe ndio utatangulia kufa mke utamuacha.
Kuna mkuu humu anaitwa #sifi Leo
 
Kesi Kama hii nimehusishwa nayo juzi, dada yangu mkubwa wakuzaliwa aliniandika Mimi mdogo wake, mumewe alipojua akamuita na kumuhoji kwanini
Akamaambia "hata nikifa Leo naamini Jane ndo atakae pambana na wanangu wewe rijali utaoa mwingine haki yangu itaenda kwingine,"

Ushauri wangu kaa nae chini umuulize nae anaweza kuwa na sababu
 
Pole mkuu. Badilisha andika watoto na wazazi wako. Usije ishi na kinyongo,mwenzio hakuamini ndo maana kamuandika mzazi wake
 
Mkuu kausha,madamu kawaandika watoto wako na Baba yake,siyo issue kivile.Babu ata likitokea la kutokea sidhani kama Babu anaweza kuwatosa wajukuu zake.Ila angeandika Mjomba au mtu wa mbali na akawaweka kando wanao hapo ingekuwa issue.Kausha tu Mkuu!
 
Sababu ni ya kijingaa maana hata wewe utapata mwanaume na anaweza wafukuza hao watoto na wew usiwe na cha kufanya maana unampenda mumeo kuliko hao watoto wa dada yako...!!

Point kubwa wanawake ni Wabinafsi sanaa na wana mawazo ya kipuuzi kudhani mwanaume anawahi kufariki mapema.. kudhani wao ndo wana uchungu sana ana watoto kuliko wanaume...! Pia kwamba mwanaume hana upendo wa kweli leo ukifa anaoa yeyote na mwanaume akifa kwamba mwanamke hatatafuta mwanaume. UBINAFSI UMEWAJAAA NA HILI HALIWEZI BADILIKAA cha muhimi sisi wanaume upate mwanamke mbinafsi ila mwenye Akili..
 
Tuishi nao kwa akili! Chunguza zaidi yaweza tokea wewe ukaandika mkopo ukaulenga kuboresha familia yenu ( wewe mke na watoto) chunguza mkopo wake atauelekeza kusaidia / kujengea wazazi wake! Hawa ndio wanawake zetu, TUISHI NAO KWA AKILI

Ni jambo la makubaliano tu, kwani hairuhusiwi mwanamke kusaidia wazazi wake?
 
Daaah hii comment tuiwekee lamination. Ndaga fijo shemeji; uzidi kuenjoy ndoa yenu na dada etu[emoji120][emoji120][emoji120]
 
KAA CHINI UMUULIZE SABABU YA YEYE KUFANYA HIVYO, UTAPATA MAWILI MATATU
hana haja hata ya kumuuliza
Mimi ninasema kila siku maisha ya sasa
Mwanamke anafata pesa kwa mwanaume
na
mwanaume na wewe fuata QUUUMA
END OF STORY
atakayebania chake abaki nacho

hayo mambo mengine ukiyawazia sana utakufa na mawazo utawaacha wanao YATIMA
 
Kwamba wazaz wake watamsubir afe ili wawe matajir kw urithi mkuu?
Hapana Mwanamke kajiangalia yeye na akaangalia uchumi wa wazazi wake akaamua kuwaandikia kwenye urithi wake ili lolote likitokea maana binadamu tuna tembea na kifo mkononi ili siku akifa mali zake wachukue wazazi wake, ndiyo maana nikasema kama wazazi wake wana uchumi imara na ndugu zake wapo vizuri hasige waza kuandika baba yake awe mrithi wake.
Kuna utofauti mkubwa sana wa kiakili kati ya wanawake waki Zungu na wanawake waki Tanzania, kuna rafiki yangu mpenzi wake msichana waki Zungu nashangaa mwanamke ana mjengea mshika nyumba ya kuishi na gari kamnunulila, nilicho jifunza kwa wenzetu mali na pesa havi sumbui roho zao .
 
Aishi nae kimkakati....Akipiga chini Kwa ajili ya hilo tu atajuta.

Sisi wanawake kuna wakati tunaiga tu bila hata sababu za msingi. Mfano kazini ikiwa Kuna fomu ya kujaza....isiwe tu ya fweza utakuta mnaulizana vip wewe umejazaje....

So unaweza Kuta tu aliiga bila kufikiria Kwa kina....

Sababu zipo nyingi ila ni kuwa hapa tunasikiliza la mmoja...

Kwa Mimi ....nikigundua mume ana mpango wa Kando.......

Hela hazieleweki zinakoenda........

Anachelewa kurudi nyumbani .....na tupo na amani....

Ana mawasiliano na ex....

Anakunywa pombe kazidisha ...na tupo na mawasiliano mazuri....

Anajali campany yake kuliko familia.....

Analazimisha safari ilimradi asikae nyumbani na ikiwa akiwa na stress za kazini nyumbani ndo sehemu yake ya kutua na kupumzisha akili

Akipiga Hela mingi anapenda matumizi makubwa na hakai home

Doooooooh ......

.HAPO MWANAUME NI HANA DIRA

Aseeeeeeee .......hapo hatuachani ila naishi nae KIMKAKATI.
 
Mkuu kausha,madamu kawaandika watoto wako na Baba yake,siyo issue kivile.Babu ata likitokea la kutokea sidhani kama Babu anaweza kuwatosa wajukuu zake.Ila angeandika Mjomba au mtu wa mbali na akawaweka kando wanao hapo ingekuwa issue.Kausha tu Mkuu!
Babu wanaweza kuwatosa wajukuu sana , mfano huyo baba ana watoto wake maisha magumu unafikiri atawaacha wataabike wakati pesa anazo za marehemu mtoto wake lazima atawagaiya watoto wake ili kuwainua kiuchumi na kuwaacha wajukuu tena wajukuu wa ukoo mwingine na siyo wa ukoo wake.
 
Na wewe ni mpuuuzi kama wao. Kwani mtoto wa kiume hakusomeshwa?

Kwa taarifa yako nina watoto wa kiume na kike, ila sikuinvest kwao ila nilitimiza wajibu kwa kuwasomesha wengi engineering hadi PhD. huo ni wajibu wangu kama mzazi.

Haiwezekani mtoto wa kike akaja kujenga nyumbani kwangu badala ya kwa mume wake. Mimi nahangaika na mambo yangu mwenyewe bila kutegemea watoto.
 
Wewe bwegge tafuta mazuzu wenzanko wa kuwadanganya jinga kabisa.

Mzazi gani anasomesha mtoto mpaka PhD?

Hivi unatuchukuliaje kwani?
 
Mkuu kausha,madamu kawaandika watoto wako na Baba yake,siyo issue kivile.Babu ata likitokea la kutokea sidhani kama Babu anaweza kuwatosa wajukuu zake.Ila angeandika Mjomba au mtu wa mbali na akawaweka kando wanao hapo ingekuwa issue.Kausha tu Mkuu!
Sawa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…