Kwenye msitu wangu kuna black mamba/ koboko natafuta njia za kumwangamiza bila kuleta madhara kwenye jamii

Yap! Tulio wengi pia tutajifunza hapo.
 
Kwa akili ya kawaida, hakuna namna utafanikiwa kuwadhibiti hao nyoka. Hilo shamba/pori ni makazi yao asili, na watakuwa wengi hadi mashamba ya jirani. Ni bora usihangaike maana kama lengo ni kufuga nyuki na siyo kilimo ambapo inabidi usafishe pori, hao nyoka huwezi kuwaondoa mkuu.
 
Maadamu unelileta humu sisi tutakushauri

Ushauri wangu ni huu. Wasiliana na maafisa wanyamapori waje kuchukua nyara yao
 
Aaah! Usimkatishe tamaa aisee. Hakuna lisilo wezekana chini ya hili jua. Kama amedhamiria ; lazima itapatikana njia tuu. Kikubwa hapo ni yy kuwa mstahimilivu kwani huenda ikamchukua muda (lakini ni muda mfupi sana) kupata ufumbuzi tatizo hilo.
 
Wakiongezeka na hatari inaongezeka kabisa
 
Aaah! Usimkatishe tamaa aisee. Hakuna lisilo wezekana chini ya hili jua. Kama amedhamiria ; lazima itapatikana njia tuu. Kikubwa hapo ni yy kuwa mstahimilivu kwani huenda ikamchukua muda (lakini ni muda mfupi sana) kupata ufumbuzi tatizo hilo.
Upo sawa mkuu yaani anamanisha Hadi 2050 nakuendelea mstu uwe wa kuhifadhi manyoka tu ! Hapana kwakweli
 
Ahsantee Kwa ushauri ila yataka moyo sana mkuu
 
Ni msitu wa ukoo kama umenisoma vizuri katka maelezo yangu nimekiri sio wangu ni WA mzee ndo mmriki wake katika siku za Hivi karibuni nimedhamiria kuanzisha mradi wa ufugaji nyuki mle maana Kwa upande wa mzee Hana shida na yeye kama mzazi wangu ndo atakuwa mnufaika mkubwa
 
Ushauri umetulia huu
Watu wengi wamependekeza Hivo kuwa niruhusu wachoma mkaa ila Kwa sharti la kuwaambia waache baadhi ya miti pakiwa peupe hawezi kaa.

Kabla sijafanya hiyo njia nikawaza nililete humu lengo nikuwa mazingira yataharibika iwapo nitaruhisu wachomaa mkaa najua Fujo za wasukuma katika kukata miti Huwa wanaichimba Hadi visiki
 
Atawapata kivipi au anawa-introduce kwenye msitu wake kwa njia gani na atawazuiaje ili wabaki hapo msituni wasije nao wakahama then ikawa ni back to square one.?
Uzuri wa wale wanapenda maeneo ya vichaka , mangroose anaweza kuwakamata na kuwapeleka ila inahitaji gharama wangu wa vijijini wanajua kuwatega , ila 🦡 ni ngumu kumkamata.

Kwa nature ya eneo aliloelezea wanayapenda sana hawa wadudu sidhani kama wanaweza kuhama labda wafukuzwe
 
Huyu kiumbe ni hatari sana hasa anapokuwa na hasira ana mbio na uwezo wa kuruka , japo huwa sio mkubwa kivile wengine humpamba kwa uhatari wake.

Kwanini usiwaruhusu wanakijiji wamuue au nao hawataki kusikia
Shida anaoneka mstuni tu yaani porini laiti angelionekana maeneo ya wazi angekuwa kama uawa muda sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…