Kwenye ndoa za kikristo uasherati pekee ndio uliruhusiwa kuvunja ndoa, kwanini wakristo huvunja ndoa kwa sababu zingine ambazo hazijaruhusiwa?

Kukosa amani ndani ya ndoa ni ishu kubwa kama vile uasherati
 
kwanini wakristo ambao wanakuja kugundua wameoa wake wachawi hawataki kuishi nao tena, unakuta mwanamke mchawi kamfanya ndondocha mama wa mme wake, kwanini anaachwa ??
Elewa ndugu mchawi, muongo, mzizi, mfitini wote tupo kundi mmoja na MUNGU anatupenda na kutulisha wote
Au wewe uliona mvua haijanyesha kwa mtu kisa ni mchawi???
Nabii Elia aliwateketeza wachawi Agano la kale, kwenye agano jipya Yesu Kristi alitakiwa aagize Moto na kuteketeza kama alivyofanya elia aliwageukia wanafunzi wake AKAWAKANYA akawaambia hamjui ni roho wa namna gan mliye naye.
Ukiwa mkristo yakupasa kusimama kwenye Yale aliyoyaamuru Yesu Kristi ikiwa neno hilo lapingana na Samwel, Eliya and co,
 
Biblia haikuandikwa na Wazungu. Wazungu wameipokea tu kama sisi, sema wao ilikuwa mapema.
Wengi hudhani ukristo ulianza na wazungu...!
Kumbe wameandika nan biblia maana wayahudi hawaitumii na wao sio wakristo?...KUULIZA SIO UJINGA
 
Sheria zipo kwenye Torati tuu huko kwengine ni mafundisho na maoni ya mitume na manabii.
Nadhani huelewi tofauti ya mambo. Wakristo hawafungwi na torati. Ndio maana huwezi mkuta mkristo anampiga mawe mchawi japo torati inaamuru hivyo.

Kwamba mafundisho ya Agano Jipya hayana sheria? kidding me?
Yesu aliposema mpende jirani yako kama nafsi yako yalikuwa ni maoni? Au alipowaambia wanafunzi Amri mpya nawapa, pendaneni yalikuwa ni maoni?

Aliposema enendeni ulimwenguni mkaihubiri injili nayo yalikuwa maoni?
Someone is confused here!

Mfano Mtume Paulo Kwa sehemu kubwa alikuwa anatoa maoni yake zaidi ambayo watu wengi hasa Wakristo wasioelewa Dini wanafikiri maoni yake ndio SHERIA.
Acha kudanganya watu. Na haya ni maoni ama? Au na Biblia nayo haielewi dini?
"Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe; lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe." - 1 Wakorintho 7:10-11

Hata Yesu katika Injili hakuleta Sheria yoyote mpya isipokuwa alikuwa anatimiliza sheria
Haya pingana na Yesu hapo...
"Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo. Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi" - Yohana 13:34-35
 
Kumbe wameandika nan biblia maana wayahudi hawaitumii na wao sio wakristo?...KUULIZA SIO UJINGA
Biblia imeandikwa na Wayahudi. Ile sehemu ya kwanza ambayo tunaifahamu kama agano la kale ndio haswa Biblia ya Wayahudi yaani Tanakh. Wayahudi hawaamini agano jipya. Ila wapo Wayahudi wakristo pia, usisahau hilo.

Petro alikuwa Myahudi, Yohana, Yakobo, Andrea, Marko, Batholomeo, Filipo, ... Mariamu Magdalena, Mariamu wa Heli na wengine wengi!
 
unamtaja maguful kwenye wakat watu wanazungumzia masuala ya ndoa ndo nauliza una apply khaki za mbowe?
Hahahahah
Magufooool alitupa tabu sana kwa chuki zisizokuwa na mpango kisa mzee wako aliwahi kushika cheo serikalin au ccm siku za nyuma!
Sijui alitaka na yeye Babu yake awege katibu siku za nyuma?
 
Uasherati it means umefunga ndoa na ndugu yako hii ndoa inakataliwa.
 
Siyo ndoa za wakristo ongelea Dini yako ikiwa miongoni mwa madhebu ya kikirsto yanatumia ndoa kama agono lisolovunjwa ndo unaweza kusema hivyo ndoa haivunjwi hata kama Kuna mambo yanayoumiza wanandoa hao, madhehebu mengine japo ya kikirsto yanavunja ndoa na Haina haja yakusubiri kibali kutoka ngazi za juu na viongozi wao wapo nchini hapahapa ndoa ikishindikana inavujwa tu kwani kwanini mtu alazimishe au ajumlishe madhehebu yote ya kikirsto hayana kibali cha kuvunja ndoa? Na kwanini ulazimishe ndoa na mtu aliye na matendo mabaya na kutaka watu waamini ni madhehebu yote ya kikirsto yanalamisha hivyo? Hakuna kitu kama hicho.
 
Zaidi ya uasherati!!!
Kwa nin unakosa Aman ni kwa sababu hataki kusamehe and let things go!
Nadhani kuna vitu u can't let it go, Mpaka Mtu anafikia kuacha/kuua ni kwamba yamemfika sehemu ya no point of returning.
 
Uyahudi ni kabila ,asili au dini ?

Mtu ukizaliwa Israeli unakuwa myahudi moja kwa moja ?

Muafrika nikitaka kujiunga dini yao na mimi nakua Myahudi ?
 
Yaah hao wayahudi ndio ila kwan hao ndo wameandika biblia Maana wayahud wanamngoja masiha wanasema yesu sie japo wanakubali alikuwa muhubiri mzuri...MI NAJIFUNZA NIELEWESHE
 
Hiyo agano la kale weka kando, tunaishi agano jipya our role model is Jesus Christ,
Hata hao wachawi Yesu anawapenda na huwalisha kama anavyomilisha Magufoool mwenye chuki na marytina mjaa fitina na majungu ofisini

Mbona zaka na fungu la kumi ni agano la kale ila makanisa ya zama hizi yanasisitiza waumini watoe.. hawasemi waache maana ni agano la kale
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…