Nadhani huelewi tofauti ya mambo. Wakristo hawafungwi na torati. Ndio maana huwezi mkuta mkristo anampiga mawe mchawi japo torati inaamuru hivyo.
Kwamba mafundisho ya Agano Jipya hayana sheria? kidding me?
Yesu aliposema mpende jirani yako kama nafsi yako yalikuwa ni maoni? Au alipowaambia wanafunzi Amri mpya nawapa, pendaneni yalikuwa ni maoni?
Aliposema enendeni ulimwenguni mkaihubiri injili nayo yalikuwa maoni?
Someone is confused here!
Acha kudanganya watu. Na haya ni maoni ama? Au na Biblia nayo haielewi dini?
"Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe; lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe." - 1 Wakorintho 7:10-11
Haya pingana na Yesu hapo...
"Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo. Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi" - Yohana 13:34-35
Hapo hakuna amri mpya Sheikhe!
Acha ubishi usio na maana.
Kwenye injili hakuna sheria mpya hata Moja.
Unaposoma Biblia jaribu kuelewa kuwa Sheria zipo Kwa Musa, huko kwingine ni maoni na mafundisho ya manabii na mitume.
Haihitaji akili kubwa kutambua Hilo.
Hiyo amri ya Upendo IPO kwenye Torati,
Kumbukumbu la Torati 6:5-7
Nawe mpende BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako; nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyasema uishipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.
Mambo ya Walawi 19:18
Usifanye kisasi, wala kuwa na kinyongo juu ya wana wa watu wako; bali umpende jirani yako kama nafsi yako; Mimi ndimi BWANA.
Huyo Paulo mambo mengi aliyokuwa anayaeleza ni maoni yake binafsi Kwa Wamataifa.
Ukisoma Biblia jaribu kuelewa anayeandika yupo katika Mazingira gani, na alikuwa anawaandikia kina nani.
Usipojua hayo utajikuta badala ya kupata maarifa unakuwa mjinga zaidi.
Alafu kuna mambo bado huyaelewi kuhusu sheria hizo za kupiga mawe, ungeomba ueleweshwe.
Wayahudi Mwanzoni kabla ya kuwepo wafalme walikuwa wanaongozwa na Mungu mwenyewe, baadaye wakakataa kuongozwa na Mungu hivyo wakataka kuongozwa na wafalme wa kibinadamu Kama mataifa mengine.
Ndipo wakatokea Waamuzi kabla ya ujio WA Wafalme.
Mpaka hapo bado hujaelewa Kwa nini watu hawapigwi mawe?
Jibu ni Kwa sababu dunia haifuati sheria za Mungu Kwa 100% isipokuwa zinafuata upagani na ushetani.
Bado hujanielewa?
Sheria za Mungu ni zilezile hazibadiliki