Kwenye sakata la Mchungaji Kimaro, nasimama na Kiongozi wangu Askofu Malasusa

Point hii
 
YESU ALIHUBIRI UFALME WA MUNGU, NA SI TAMADUNI ZA KANISA FLANI
JE NI UTAMADUNI WA KANISA KUMSIMAMISHA UCHUNGAJI MTU BILA KUTOA TAARIFA YA SABABU NI NINI?
KWA SASA KIMARO NI MAARUFU KULIKO KANISA LENYEWE
 
Misingi ipi? Mfano Lutheran huku kaskazini hasa Arusha imejaaa ukabila full yaani kama wewe sio Mwarusha au Mmsai basi sahau hata kuwa mchungaji, asilimia 100 ya wachungaji ni wamasai na Waarusha, Shule za kanisa asilimia 100 ya wakuu wa shule ni the same, njoo sasa kwenye project za kanisa.

Binafisi mara 1000 nikasali kwa manabiii ila sio kwa hawa lutheran
 
Upo sahihi
 
Hizi dini zenye zilikuja kututawala. Aanzishe kanisa lake kama hananja.
 
Mimi nashindwa kuelewa nini msingi wa Hoka ZOTE hizi. Mchungaji kimaro hajalalamika popote. Alilopewa barua ya likizo alitii maagizo ya mwajiri wake na alikabidhi ofisi kwa mtumishi mwingine na akawaaga waumini wake. Sasa kafanya kosa gani hapo? Waumini msimamo wao sio wa mchungaji Kimaro. Ila tufike pahala tuuseme UKWELI KKKT Kuna ukiritimba mwingi sana. Mimi ni m- KKKT Nina zaidi ya mwaka sijaenda katika makanisa Yao kwa ukiritimba. Pesa zinapigwa anayehoji anatishiwa na michango ndiyo imejaaa tele tena ya kupangiwa na inatakiwa ulipe upended usipende.
 
KKKT muna tabu swanaaa, mwenzako humu kasema kabla yake yalijaa madeni pakakosa muelekeo. Kwanini ulikimbia madeni ya kanisa lako? Sasa ndio unaona sawa pako bila madeni? Wewe ni chawa au Askofu mwenyewe.
 
Walianza kwa kumpora YouTube channel yake, siku hizi inaitwa Lutheran kijitonyama tv. Sasa wamrudishie
 
YESU ALIHUBIRI UFALME WA MUNGU, NA SI TAMADUNI ZA KANISA FLANI
JE NI UTAMADUNI WA KANISA KUMSIMAMISHA UCHUNGAJI MTU BILA KUTOA TAARIFA YA SABABU NI NINI?
KWA SASA KIMARO NI MAARUFU KULIKO KANISA LENYEWE
Mkuu umejidanganya sana, Kimaro awe maarufu kuliko kanisa? Kimaro ni maarufu sababu yupo ndani ya Kanisa, kama anaamini yeye ni maarufu kuliko kanisa, mwambie asiende hiyo likizo aliyopewa aone umaarufu wake utamfikisha wapi?
 
Walutheri tuna bahasha ya Ahadi na Jengo- naahidi mwenyewe kiasi cha kumtolea Mungu kwa mwaka mzima ninachoona nitaweza.
Kanisa lenu la magomeni pale mataa
Na lile la kinondoni mahakamani mbona hazikamiliki [emoji1]

Ova
 
Naona Kimaro ndiye kataka leta mtafaruku, hakuwa na sababu ya kutangaza vile alivyo tangaza.

Pia inaonesha yeye ndo anawatumia Mwananchi na EFM kuonesha watu hawakubaliani na kilichofanyika.

NB: Kanisa lisirudishwe nyuma na watu wanaotaka wawe juu ya kanisa.
Kama wanabanwa waanzishe makanisa yao
 
Unajua maana ya utamaduni? Ngoja nikisaidie....ni totality of doing things ...ni namna hii ya kufanya mambo inayotofautisha msabato na mroma na mkkkt. Hata sisi kuna pastor alikuja na style yake ya kufanya mambo na kanisa likamkataa . Akafungua kanisa lake hapo sinza na waumini debe wakamfuata. Baada ya muda yakamshinda akarudi kundini. Why alitolewa kwakuwa alienda nje ya utaratibu. Mkitaka mfanye style yoyote nendeni kwa akina masanja wao ni free church
YESU ALIHUBIRI UFALME WA MUNGU, NA SI TAMADUNI ZA KANISA FLANI
JE NI UTAMADUNI WA KANISA KUMSIMAMISHA UCHUNGAJI MTU BILA KUTOA TAARIFA YA SABABU NI NINI?
KWA SASA KIMARO NI MAARUFU KULIKO KANISA LENYEWE
 
Kila kitu kina taratibu na misingi yake
 
YESU ALIHUBIRI UFALME WA MUNGU, NA SI TAMADUNI ZA KANISA FLANI
JE NI UTAMADUNI WA KANISA KUMSIMAMISHA UCHUNGAJI MTU BILA KUTOA TAARIFA YA SABABU NI NINI?
KWA SASA KIMARO NI MAARUFU KULIKO KANISA LENYEWE
Akili unazo za kuchambia ww..KKKT ilikua maarufu kabla ya uyo kimaro kuzaliwa
 
Umeongea Jambo la msingi. Kila kanisa liheshimu misingi yake. Mimi nasali kanisa moja haliruhusu matumizi ya maji na mafuta. Sasa akaja muhubiri mmoja anatumia maji na akawa amepanga kumwagia watu maji, wazee walimzuia kabla hajaanza kumwagia watu maji. Sasa ukiruhusu Kila mtu afanye ya kwake kisa uhamsho hatutafika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…