Mwezi February mwaka huu, Serikali ya Tanzania ilisaini hati ya makubaliano (MOU) na Serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwa ajili ya kutusaidia kuendeleza misitu yote nchini, inayosimamiwa na Wakala wa misitu (TFS). Yani waarabu wanaoishi Jangwani wanatusaidia kuendeleza misitu. Kwanini wasipande misitu kule kwao waondokane na Jangwa?
Nadhani kwenye suala la misitu sisi ndio tulitakiwa tuwasaidie waarabu sio wao watusaidie sisi. Sisi tuna misitu ya asili na misitu ya kupanda. Tuna mapori ya akiba na mapori tengefu. Tuna misitu ya mvua (Rain forest) misitu ya minene (tropical thick forest), na misitu hafifu (broadleaf forest). Yani kwa kifupi kuhusu misitu, mapori na masuala ya miti na utunzaji wake, hakuna wa kutuambia kitu. Tupo vizuri.
Waarabu wao ndio wanatakiwa waje wajifunze hapa kwetu kuhusu misitu. Na sisi ndio tunapaswa tuwasaidie ili waweze kuwa na misitu kule kwao au hata mapori ya akiba. Lakini eti wao ndio wanatusaidia sisi kuendeleza misitu? Yani watu wasio na msitu hata mmoja wana kipi cha kutusaidia sisi ambao tuna misitu na mapori kila wilaya? Hii ndio mara ya kwanza nasikia Mzaramo anataka kumfundisha Mmasai kuhusu ufugaji wa ngombe. Apaaa ndenga.!!
View attachment 2663245
Source:
VPO | News