Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 59,804
- 134,593
Yes wanapewa, wenyeviti wote wa serikali za kijiji ni wasajili wa ndoa za kimila, zile ndoa kabla ya kufungwa simila, wanapaswa kwenda kujisajiliWatu wanaoana kijijini huwa wanapewa cheti cha ndoa?
Vyeti vyote vya kuzaliwa, ndoa na vifo, hutolewa na RITA pekee, ndoa za kanisani, msikitini, za kimila na za kiserikali, wale wasajili wote, wanapewa kibali na RITA na vyeti vyote ni vya RITA!, wafungisha ndoa wote, wanafungisha kwaniaba ya RITA. Haijalishi ndoa imefungwa wapi na ni aina gani, lazima isajiliwe RITA, na kwa kukusaidia, hata talaka kwa ndoa ya cheti, haijalishi ni ya kiserikali, kidini au kimila, talaka inatolewa na Mahakama only, hivyo kwa ndoa za Kiislamu, ile talaka rejea au talaka tatu, haitambuliwi kisheria, baada ya kutolewa, lazima ipelekwe Mahakamani Mahakama ndio itoe talaka!. Hakuna talaka ya kanisani wala ya msikitini!.Cheti kitolewe kijijini tu, mpaka Rita kutafuta nini?
Jaribu kuoa kimila alafu utake kumlipia Bima ya afya mke wako uone kitakachokupata. Utaambiwa mpaka ukaape kwa mkuu wa wilayaYes wanapewa, wenyeviti wote wa serikali za kijiji ni wasajili wa ndoa za kimila, zile ndoa kabla ya kufungwa simila, wanapaswa kwenda kujisajili
kwanza, kisha baada ya sherehe za kimila, wanapaswa kwenda kusaini vyeti.
P
Hiyo maana yake hiyo ndoa ya kimila, haikusajiliwa, hivyo kwenda kuapa kwa DC ndiko kuisajili kwenyewe.Jaribu kuoa kimila alafu utake kumlipia Bima ya afya mke wako uone kitakachokupata. Utaambiwa mpaka ukaape kwa mkuu wa wilaya
Hamna sehemu nyingine utakayoambiwa ukaape tofauti na DCHiyo maana yake hiyo ndoa ya kimila, haikusajiliwa, hivyo kwenda kuapa kwa DC ndiko kuisajili kwenyewe.
Ni kama watoto wanaozaliwa nyumbani, hawana vyeti vya kuzaliwa, likitokea jambo linahitaji cheti cha kuzaliwa, ni lazima huyo mtoto aapishwe kwa affidavit
Watanzania wengi ni wavivu tuu kufuata sheria, taratibu na kanuni, wanakutana vichochoroni, wanabebana, wanalipana mahari kimila, ndoa tayari, bila kuandikisha popote!.
Huu ni mwanzo mzuri wa formalization of informal institutions, huko mbele tutafikia viwango hadi mama ntilie, machinga na informal trades zote zinasajiliwa zinalipa kodi.
P
Unaweza kuapa kwa wakili yeyote, mawakili wote ni ma kamishna wa viapo, ila kama ni kiapo cha ndoa, nenda kwa msikitini, kanisani au kwa Mwenyekiti wa kijiji mwenye kibali cha kufungisha ndoa.Hamna sehemu nyingine utakayoambiwa ukaape tofauti na DC
Sijawahi kukutana na mwenyekiti mwenye kibali cha ndoaUnaweza kuapa kwa wakili yeyote, mawakili wote ni ma kamishna wa viapo, ila kama ni kiapo cha ndoa, nenda kwa msikitini, kanisani au kwa Mwenyekiti wa kijiji mwenye kibali cha kufungisha ndoa.
P
Nchini Tanzania, masuala ya ufungishaji na usajili wa ndoa yanasimamiwa kisheria na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) chini ya Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 (Sura ya 29).Sijawahi kukutana na mwenyekiti mwenye kibali cha ndoa
Huu usumbufu ndio siutaki, nataka ndoa ziwe simple na clear kupunguza gharama, single mothers na watoto wa mitaaniNchini Tanzania, masuala ya ufungishaji na usajili wa ndoa yanasimamiwa kisheria na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) chini ya Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 (Sura ya 29).
Mamlaka ya kisheria yanatambua makundi mawili makuu ya wafungishaji ndoa: [1, 2]
1. Wafungishaji wa Ndoa za Kidini (Makanisani na Misikitini)
Viongozi hawa wa dini wanapaswa kuwa na leseni hai ya ufungishaji ndoa iliyotolewa na RITA. Hawa ni pamoja na: [1, 2]
Kumbuka: Ni kosa kisheria kwa kiongozi wa dini kufungisha ndoa bila kuwa na leseni hai au bila kusajiliwa kwenye mfumo wa kidijitali wa e-RITA. [1, 2]
- Mapadri na Maaskofu (Ndoa za Kikatoliki, Kianglikana n.k.)
- Wachungaji (Makanisa ya Kilutheri, Kipenteokoste n.k.)
- Masheikh na Maimamu (Ndoa za Kiislamu/Nikkah)
2. Wafungishaji wa Ndoa za Kiserikali (Civil Marriages)
Hawa ni viongozi wa kiserikali ambao kisheria ndio wasajili wa ndoa katika maeneo yao na hawahitaji kuwa na leseni maalum ya RITA kufanya hivyo. Hawa ni: [1]
Mambo Muhimu ya Kuzingatia Kuhusu Ufungishaji Ndoa:
- Wakuu wa Wilaya (DC)
- Makatibu Tawala wa Wilaya (DAS) [1]
You are right,ndoa za kimila hazitambuliki,na wafungishaji ndoa za kimila walifutwa tulipofuta uchifu!
- Uthibitisho wa Vyeti: Mfungishaji wa dini anapaswa kutoa vyeti vya serikali vilivyosainiwa katika nakala tatu (mume, mke, na nakala ya RITA). Ndoa inayofungwa kwa cheti cha ndani cha dini pekee (kama cheti cha Bakwata au cheti cha ndani cha kanisa pekee) bila cheti cha RITA haitambuliki kisheria. [1]
- Kutoa Taarifa (Nia ya Kufunga Ndoa): Wanandoa wanatakiwa kutoa taarifa ya nia ya kufunga ndoa siku 21 kabla ya siku ya harusi kupitia mfumo wa e-RITA au kwenye ofisi za wilaya
- p
Kama hazisajili ni kosa kwa sababu zinatambulika kwa sheria ya TanzaniaKwa nini hazisajiliwi?
Ndio hoja yangu ilipo
Hoja nzuri sana hiiWewe waziri Dk Gwajima kinachofanya mpaka leo ndoa za kimila hazina cheti halali ni nini?
Kwa sasa ili ndoa ipate cheti ni lazima iwe ya kanisani, msikitini au kiserikali tu ,swala hili linasikitisha sana.
Kuongezeka kwa single mothers, watoto wa mtaani sababu ni wewe waziri Gwajima na wizara yako kulifanya swala la ndoa kuwa gumu sana na lenye gharama.
Swala la ndoa lilitakiwa liwe simple yani wakwe wakielewana na kupeana mahali kulingana na mila na desturi zao basi vijana wao wapewe cheti halali ila pia wakitaka kuongeza cheti cha kanisani au msikitini ni sawa,
Lakini hili swala la kusema kama huna cheti cha kanisani au msikitini hupati huduma hata ya Bima ya afya siyo Sawa na tutaendelea kushuhudia ongezeko la single mothers.
Jaribu kuoa kimila alafu utake kumlipia Bima ya afya mke wako uone kitakachokupata. Utaambiwa mpaka ukaape kwa mkuu wa wilaya
First Prev2 of 2
Write your reply...
Post reply
Attach files Insert quotes…
Similar Discussions
Share:
Vita dhidi ya ushoga: Waziri Gwajima amechagua silaha kali au butu?
- Started by Kiranja wa jamii
- Mar 22, 2026
- Replies: 272
Jukwaa la Siasa
- Started by Sijapewa username bado
- Oct 13, 2025
- Replies: 31
FacebookXBlueskyLinkedInRedditWhatsAppEmailLink
TopBottom