Naumia sana nikifikiria wazazi walivyojinyima kutulipia ada, kuna kipindi walikopa kabisa, naumia sana kuona mategemeo ya wazazi kwa ada walizolipa hayajafikiwa,,, Inauma sana !!
Ukiachana na maumivu ya wazazi na mimi napitia maumivu mazito, kaka na mdogo wangu walisoma kwa juhudi sana, sioni kama ipo fair kwa wanachopitia, walistahili zaidi sana sana sana. mtu alie kwenye unafuu wangu akijisifu ana ahueni basi ni wazi ni mjinga.
Binafsi niliishia form 4 mwaka 2012 shule ilinipita kushoto, mzee aliniambia nijiandae kurudi kijijini, ilibidi nikajiongeza nianze kujifunza chochote nikaingia kwenye useremala kwa msaada wa mjomba wa rafiki (mjini connection), nikawa saidia fundi kidogo nikaweza kuhama hata nyumbani na kumiliki pikipiki, nikajichanga changa na mimi nikawa na ofisi yangu inayonipa kipato si haba kwakweli hata kagari kapo, haikuwa rahisi hata kidogo hasa mwanzoni, kuna kipindi kidume chozi lilinitoka kwa ugeni wa kazi lakini nilikomaa.
Sasa hapo home kuna bro na mdogo wangu wa kike wamemaliza vyuo ngazi ya degree lakini mambo si mambo kiuchumi, bro alihangaika hizi kazi za kujitolea, akaingia kitaa akapata kazi kampuni binafsi kazi kibao malipo kiduchu, alisota miaka minne kampuni ikafungwa na kazi ikaisha,,, ikabidi home pale tujichange tumpe mtaji, ikabidi ajifunze kunyoa nae akafungua ofisi yake, kiuchumi pana nafuu lakini hadi kafika hapo kapitia misoto kwa ukosefu wa ajira za ofisini.
Kwa mdogo wangu nae tangu 2020 alipomaliza chuo hali bado sio poa, ilibidi tujichange change nae apige mwendo, biashara ya keki mara ya kwanza ilibuma kwake akawa yupo home, tukajikusanya kusanya kwa sasa angalau ana kamgahawa kidogo pana unafuu.
Nilichokuwa najiuliza ni kwamba, hizi elimu zinaandaa wengi wawe maofisini wanasukuma kalamu na kukaa kwenye viti wakisubiri mishahara lakini hizi ajira zimekuwa adimu, nimeona kwamba yafaa zaidi kungekuwa kuna veta kabla ya kwenda chuo.