Pia hakuna ushahidi wowote kuwa jamaa anafadhiliwa na Lowasa ama mafisadi. Ni mbinu zinatumika kumchafua tu. Letenu ushahidi kuwa anafadhiliwa na mafisadi ndio tuseme hilo halifai, ila sio kuzusha ili kumharibia jamaa mipango yake. Kama mnazungumzia mtandao jinsi walivyomchafua SAS, vipi nanyi mnatumia mbinu hiyo hiyo kuchafua watu kwa kusema wametumwa na mafisadi?. Hii yote ni kuwa kuna watu wanadhani wao ndio wana haki ya kuwa Wabunge, akitokea mtu kutaka kugombea, kumharibia inatumika mbinu ya kumuandama kuwa katumwa na mafisadi. Mnaosema kuwa Mwakalinga anatumiwa na mafisadi, nyinyi ndio mafisadi, na mnatumia mbinu zilezile walizotumia 2005 kumchafua SAS.