Wewe nilidhani umefungiwa na wenzako? au kwa vile Mwakalinga ni mwanzilishi wa JF? ha ha ha ha.
Ukishirikiana na Lowasa, Ridhiwani, ROstam na Mwakipesil, basi wewe ni fisadi tu. Hiyo ndiyo label pekee inayomfaa Mwakalinga hivi sasa.
Shida ilianzia vacation yake Monduli na kufanya vikao vya faragha na mzee wa mvua za Thailand na ndege ya uchumi inayopaa.....na baadhi ya wapambe wake hapa akina Kanda2 walipokuja na laptop atakazo nunua Rostam. Sisi watu makini tumefatilia michango ya Mtanzania hapa JF moja kwa moja yuko na Mwakipesile, kwa maana hiyo Mwakalinga hawezi kuwa nje ya mduara wa RA, EL na Mwakipesa (Mwakipesile) kuendeleza siasa za chuki Kyela. Simple arithmatic mkuu....
kwa hiyo na wewe unatumiwa na mafisadi wa upande wa upepo wa singida ?
Mawazo potofu ni potofu tu!! argue za namna hii ni potofu ,na ku argue kinamna hii ni kipotofu potofu tu.
wewe sema kwanini asingombee
Naomba ifahamike wazi hapa kwako mkuu Mfumwa na kwa wengine hapa kuwa mimi Mwafrika sina tatizo na uamuzi wa Mwakalinga kugombea huo ubunge. Kila mtu Tanzania (hata kina Chenge na Lowasa) ana haki kwa mujibu wa sheria za nchi kugombea ubunge wa kokote wanakotaka na kwa muda wowote ule wanaotaka.
Kinachojadiliwa hapa ni siasa ambazo zinazunguka uamuzi na kugombea. Kumbuka pia kuwa hili ni jukwaa la siasa. Kama Mwakalinga kapita Monduli kabla ya kwenda kutangaza rasmi huko Kyela, then ni fair game kujadili hapa yote yaliyotokea Monduli.
Mkuu Mfumwa ahsante sana kwa mchango wako mzuri sana. Ni ukweli usiofichika kwamba kila Mtanzania ana haki ya kugombea ubunge katika jimbo lolote lile ili mrafi tu katimiza miaka 18 na ni mwenye akili timamu.
Pamoja na kwamba Mwakalinga ana haki ya kugombea huko Kyela lakini pia ni lazima tutilie maanani mazingira yote yaliyokuwepo yanayohusiana na kugombea kwa Mwakalinga na kina nani ambao wanampigia debe Mwakalinga katika kinyang'anyiro hicho.
Tukumbuke pia kundi la mtandao ambalo ni la watu hao hao wanaompigia debe ndiyo hao hao walitumia mabilioini ya pesa kuhonga na kumchafua SAS katika kinyang'anyiro cha kumpata mgombea wa CCM katika uchaguzi wa 2010.
Kwa maoni yangu hawa mafisadi wote akina Lowassa, RA na wengineo wote ambao inasemekana wanamuunga mkono Mwakalinga ili amuondoe Mwakyembe nadhani wanafanya hivyo kutokana na kumuona Mwakyembe kama mbaya wao wa aliyevimwagia mchanga vitumbua vyao
Punguza hasira mkuu. Hii ni JF - watu wanaongea openly na kumkoma nyani giladi mchana kweupeeeeee mpaka Monduli.
Ha ha ha ha acha munkari kaka kama huwezi kuandika kitu ila kurusha kauli zenye kubomoa take a time out na baadaye ukishatulia njoo uandike kitu ambacho kitaeleweka badala ya hizi negatives statements zako kuhusiana na mchango potofu.
Sikonge hebu lete uthibitisho wa mimi kuandika kwamba Mwakalinga kachukua pesa za Lowassa au za mafisadi.
wewe ndio ututhibitishie kwamba Mwakalinga anasapotiwa na RA na Lowasa,tofauti na hapo mwanaume kuwa mbea ni aibu kwa familia na jamii nzima.
Tushindane kwa hoja na kuheshimiana lugha gani hii Kiongozi?
Simpambi yoyote hapa nasema kama Mtanzania kwa maslahi ya nchi yangu. Na hii tabia yako ya kuita mawazo ya wenzako ni "mawazo potofu" achana nayo kama una mawazo tofauti na ya kwangu basi yaweke hapa badala ya kuanza kutumia lugha ambazo hazijengi bali zinabomoa.
teh teh teh
hasira gani tena ? hapa nipo yani wewe huko unasali ili nifungiwe teh teh teh mwambie mkumbushe mods anipe kibano ili upumue .
Tushindane kwa hoja na kuheshimiana lugha gani hii Kiongozi?
Kwa watu wote hapa wewe ndiye wa kutoa kibano? Nimekuwa hapa kwa zaidi ya masaa kumi sasa na hukuwepo (ulijificha) kisha unaomba nini cha kupewa hapa.
Watu kama wewe na sera zako hizo za kuishi ulaya miaka 18 hamnipi tatizo lolote. Watu mnaoshabikia na kuunga mkono chama cha mafisadi kwangu ni watu wa kawaida kabisa nisio na sababu yoyote ya kuwapa huruma hapa jamvini.
Tukumbuke pia kundi la mtandao ambalo ni la watu hao hao wanaompigia debe ndiyo hao hao walitumia mabilioini ya pesa kuhonga na kumchafua SAS katika kinyang'anyiro cha kumpata mgombea wa CCM katika uchaguzi wa 2010.
Kwa maoni yangu hawa mafisadi wote akina Lowassa, RA na wengineo wote ambao inasemekana wanamuunga mkono Mwakalinga ili amuondoe Mwakyembe nadhani wanafanya hivyo kutokana na kumuona Mwakyembe kama mbaya wao wa aliyevimwagia mchanga vitumbua vyao,
Sikonge hebu lete uthibitisho wa mimi kuandika kwamba Mwakalinga kachukua pesa za Lowassa au za mafisadi.
Wakuu Mwafrika na BAK, mimi sipingi kujadiliwa kwa Mwakalinga kuwa anafaa kuwa Mbunge ama la. Ninalopingana nalo ni kumuhusisha na mafisadi sababu tu ya kuweka nia ya kugombea jimbo la Dr. Mwakyembe. Jee Dr. Mwakyembe ni Mbunge wa maisha?. Miaka mitano ya Wabunge inaisha mwakani, ni haki ya Mtanzania yoyote anayetimiza masharti ya kuwa Mbunge kujitokeza kugombea iwe Kyela, Kawe, Nyamagana, Same nk.
Hili suala la kusema Mwakalinga alienda Arusha, Mkuu Sikonge kalitolea maelezo kuwa alienda ona watoto wa marehemu Kaka yake. Lakini hata kama ingekuwa hakwenda kwa hilo, jee si haki mtu anayegombea Ubunge nje ya Mkoa wa Arusha kutembelea mkoa huo?, ina maana ukiwa unagombea Ubunge ukaonekana Arusha (Monduli) ama Tabora (Igunga) basi unafadhiliwa na mafisadi?. Hii hatuwezi kukubaliana nayo, Mtanzania yeyote ana haki ya kutembelea mkoa wowote na wakati wowote.
Pia hakuna ushahidi wowote kuwa jamaa anafadhiliwa na Lowasa ama mafisadi. Ni mbinu zinatumika kumchafua tu. Letenu ushahidi kuwa anafadhiliwa na mafisadi ndio tuseme hilo halifai, ila sio kuzusha ili kumharibia jamaa mipango yake. Kama mnazungumzia mtandao jinsi walivyomchafua SAS, vipi nanyi mnatumia mbinu hiyo hiyo kuchafua watu kwa kusema wametumwa na mafisadi?. Hii yote ni kuwa kuna watu wanadhani wao ndio wana haki ya kuwa Wabunge, akitokea mtu kutaka kugombea, kumharibia inatumika mbinu ya kumuandama kuwa katumwa na mafisadi. Mnaosema kuwa Mwakalinga anatumiwa na mafisadi, nyinyi ndio mafisadi, na mnatumia mbinu zilezile walizotumia 2005 kumchafua SAS.
Hii lugha ni nyepesi sana kulinganisha na kumwita mtu fisadi ama anasapotiwa na mafisadi bila uthibitisho
Mkija kwa hoja mkuu tutashindana kwa hoja lakini kwa njia za kupana tutacheza hivyo hivyo mana mndundiko ndivyo unapigwa.
Hayo maandishi yenye NYEKUNDU, Mwakalinga anaungwa mkono vipi?
Inawezekana mie sikuelewa na ulikuwa na maana :-
1. Kumpigia debe (wanachukua debe na kumpigia) au wako stendi ya mabasi na wanapiga bati la Bus na kuita abilia "Haya wa Mwakalinga".
2. Wanamuunga Mkono. Inawezekana basi mkono wake ulikuwa umekatika au kupata crack. Sasa sijui wanaunga kwa kutumia Pins au Bolts. Inawezekana pia wanafanya Soldering au Welding kabisaa.
Kama ulikuwa na maana hizo hapo juu, basi samahani. Mie nilidhani kwamba MAFISADI wakikuunga mkono ni kuwa WANAMWAGA mamilioni ya EPA. Samahani sana BAK kwa hili.
Hah haha ha ha,
Unamtisha nani sasa?! mvua za Thailand zimekosa radi nini?!
zimekosa mvua na tatizo jingine ambalo limeibuka ni kwamba singida kumenyesha mvua mfululizo na msitu umeota balaa sasa unazuia upepo.kifupi singida hakuna upepo tena wa kuzalisha umeme na hata wawekezaji wameota mbawa ktk kuwekeza upepo singida.
Kaishiwa hoja huyo. Alitegemea mteremko hapa JF kwa sera za kifisadi za laptop na kuishi ulaya miaka 18 (my foot).