Balantanda
JF-Expert Member
- Jul 13, 2008
- 12,480
- 4,775
Hata sijamuelewa anaongea vitu gani aisee..Mwakalinga kusoma SUA na kukopa dagaa sijui vinahusiana nini!!!!!!!!!😱😱Toka Juzi aliishiwa ameanza weka porojo za kiutu uzima, hajajibu kitu!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hata sijamuelewa anaongea vitu gani aisee..Mwakalinga kusoma SUA na kukopa dagaa sijui vinahusiana nini!!!!!!!!!😱😱Toka Juzi aliishiwa ameanza weka porojo za kiutu uzima, hajajibu kitu!
Sikonge,nafurahi kusikia waniheshimu mkuu,nami nakuheshimu sana tu...Sidhani kama ni kosa kutaka Mwakalinga aweke CV yake hapa(keshayavulia maji nguo aisee..........),maana hiyo CV ndo itatueleza yeye ni nani na pia itajibu hayo maswali yanayojitokeza kila wakati kuhusiana na hiyo SUA..Halafu,George njia aliyoitumia (kwangu mimi) naona itammaliza mapemaaa kabla hata form hazijaanza kuchukuliwa...Binafsi,ningekuwa mimi ningesubiri muda muafaka ufike niingie uwanjani(bila hata kujinadi kupitia hapa JF),nina uhakika mengi yanayoandikwa hapa kuhusu George kuna watu wanayahifadhi/wanayachukua kwa lengo la kuyatumia hapo baadaye...George angetulia tu asubiri muda ufike achukue form aanze kujinadi,sasa hivi kaanza mapema mnooo(nionavyo mimi)...
Sikonge,hizi ni dalili kwamba UMEISHIWA HOJA..Mambo gani haya unaanza kuandika aisee
Balantanda,
You are very right. Ndiyo maana George kwa sasa hawezi kuweka CV yake na hasa hapa JF. Muda ukifika, atafungua WWW na kuweka habari zake zote na kila kitu kitaandikwa hapo. Sababu ya yeye kuacha SUA ilikuwa zaidi ni sababu ya KIFAMILIA. Ndiyo maana nimekuandikia hapo kuwa waliondoka yeye na dada yake.... ukisoma kwa mbali unaweza kupata mwanga. Ila sababu hasa kwa kweli na ibaki ya kifamilia. Amini nakuambia, hata ungelikuwa wewe, wampenda dada yako basi ungeliondoka. Na Mungu bariki ondoka yake pale imekuwa ya mafanikio makubwa.
Kama umesoma post za nyuma za Mtanzania, kundi la M-Mbeya wamekuwa wakimuandama sana. Wengi wao hawa unawaona hapa kuuliza CV na SUA, ni kundi hilo. Waliandika hadi makala kwenye MAJIRA wakati Mwakalinga hata Tanzania hajafika. Walipeleka hadi mtu UK na kuomba huku wakileta VITISHO kuwa ASIGOMBEE Kyela. Tatizo anakuomba usigombee huku anakupiga vita. Sasa hii kitu hata kama ni wewe utakaa kimya? Hata kama hukuwa umepanisa kugombea, mwisho unachukia na kusema "ehhh, sasa ngoja nisikilize kilio cha watu na changu mwenyewe, nigombee Ubunge".
Wakati Mwakalinga hata Kyela hajafika, Malafyale akaweka hapa ujumbe kuwa Mwakalinga yuko Kyela na kafanya Mkutano. Kumbe wakati huo Mwakalinga yuko Arusha. Wakageuza kibao kuwa kaenda Monduli kukutana na Lowassa, wakati huo Lowassa yuko Dodoma. Tulipombana Malafyale (ambaye sasa naona kabadili jina) akaja na neno "eti Mwakalinga alikuwa Kyela KIROHO". What a ****, KIROHO?????? Kwa hiyo, Mwakalinga hakutangaza, ila kambi ya wapambe wa M-Mbeya ilitangaza.
[/B]
Ndo maana nikasema Georgr kaanza mapema mnooo...Siasa za Bongo kila mtu anazijua eti,Ni mchezo mchafu...So George awe tayari kukabiliana na lolote litakalosemwa katika kipindi hiki kigumu mpaka kufikia kura za maoni...Halafu,lawama msimpelekee zaidi huyo M-Mbeya,mnajuaje labda kuna mtu mwingine naye anajipanga kimya kimya kulitwaa jimbo hilo la Kyela,cha msingi tusubiri tu wakati muafaka ufike
Leo umejibu walau sababu ni za KIFAMILIA zaidi na si ACADEMIC, ngoja wajuvi tufatilie tujue na kisa cha dada yake kusababisha George Mtanzania kukimbilia Poland tutafahamishana......
Mzee rekebisha hapo sisi wengine tulisoma mambo ya Gender and Gender rights unatukwaza..hutendei haki hapo mama zetu! hata kama wewe umeathirika na mfumo dume
Ninyi mnaomjua Mwakalinga vizuri tuwekeeni CV yake hapa ili kukata mzizi wa fitina...ioneshe alizaliwa lini,alisoma wapi shule ya msingi,sekondari,chuo(under graduate),alikopata hizo Masters zake 3(kama sikosei) na mazagazaga mengine..hapo ndo tutajua huyu mheshimiwa kasoma SUA ama la
3. UDSM kwa miaka miwili mpaka 1988
4. SUA kwa mwaka mmoja mpaka 1989 (hakumaliza shule yake)
Engineer,
Hapa kilitokea nini tena.....? Why UDSM miaka miwili, alikuwa anafanya kozi gani ya miaka miwili? au alidisco?
Tena kwa nini SUA hakumaliza shule yake?
Bado watakuuliza hivi: SASA ANA WATOTO WAWILI KIVIPI?
Ilikuwa course moja ya Agricultural Engineering miaka miwili UDSM na miaka miwili SUA.
Hata kama ange disco yeye atakuwa sio wa kwanza wala sio wa mwisho ila mimi sijui. Hivi kwa CV kama hiyo huyo ni mtu wa ku disco kweli? Labda kama alizembea tu shule.
Mwakalinga haishi wala kufanya kazi kama mhandisi kilimo, anaishi kama mtaalamu wa Kompyuta course ambayo alifaulu vizuri sana mpaka kupewa full scholarship ya Ph.D bila kuomba.
Wadogo zake wanasema baada ya kuona umaskini wa ndugu zake akaamua a concentrate na kazi yake ili aweze kuisaidia familia yake. Amewasomesha wadogo zake wote mpaka vyuo vikuu.
Mimi nilivyotambulishwa Mwakalinga wiki mbili zilizopita, nilidhani wananidanganya. Nafahamiana na wadogo zake ambao ni vibonge mno, kuja kumwona yeye anaonekana kama mdogo wao.
Ndio maana hata wengine wanamwita kijana wakati ana miaka 44.