Spinning zimeanza, Kiongozi na Kamanda FMES, uliishawahi kuja hapa na kulithibitisha jamvi Mwakalinga hana mpango wa kugombea Kyela yuko vacation tu aliyoianzia Monduli, mbuga za wanyama huko northen circuit, akaenda Zanzibar etc etc, ulipobanwa ukaja na utetezi tata kuwa katiba haijavunjwa yeye kugombea, this is a fact lakini mimi mpiga kura siwezi mwamini huyu mgombea kigeu geu, na ahadi zake kupitia wapambe wake. Leo unakuja na lingine kama kawaida umeongea naye anakanusha maandishi ya gazeti, Kamanda unaheshima zako hapa JF usijiingize kwenye mambo ya aibu hapo mbeleni.....usije banwa ukaishia sema hakuna sheria iliyoparaganywa.
Respect
Masa
- Mkulu Masa wewe unanijua vizuri sana, niamuamini sana George na watu wenye kujiheshimu humu ndani kama yeye, hajawahi kunidanganya hata siku moja, infact ni mmoja wa member wachache sana ninaowaheshimu na kuwaamini kuliko humu JF. Na siku George akinidanganya utakuwa ndio mwanzo na mwisho wangu kujihusisha naye, hilo kwangu huwa wala sifikiriii mara mbili.
- Ninaona juhudi kubwa sana za kutaka kuugeuza mjadala wa George na Kyela, kwenye level za Yanga na simba, kugombea ubunge kuna sheria zake mkuu, Zitto alisema hagombei na sasa ameamua kugombea tena, kwamba hilo linamfanya Zitto awe less ya umahiri wa uongozi kwa taifa, huo ni uamuzi wako, ila kwangu knowing politics as I do hili kwangu ni none-ishu, kwa sababu nitajaza thread nzima na mifano ya viongozi walioshia kuwa maarufu sana duniani na hii promise ya one day kutogombea na next wakagombea, kumbuka Hillary wakati anagombea Senate NY, aligoma kata kata kwamba hana nia ya urais, lakini you know the rest of the story. Sasa eti heshima yangu hapa JF itaharibika wka sababu sijali ishu ndogo ndogo za siasa kama hii ya Hillary, basi kwa standard zako Masa hata Obama hana heshima kwa kumpa kazi huyu mama aliyesema hagombei lakini akagombea au?
- Sasa kama nia yako na yenu ni kumshambulia na kumchafua George, naomba mje na facts au dataz, ama sivyo mtaishia kujishusha hadhi na hasa ya hii forums, ninasema hivi article iliyoandika juzi ilikuwa very low kwa mtu wa calliber ya George, kwamba eti anagombea ubunge kwa sababu aliwahi kuwa mweka hazina wa Tanzanite, that is low mkuu.
- Mimi unaifahamu vizuri, kama unataka kuubadili huu mjadala kuwa FMES unakaribishwa sana, lakini binafsi nitaendelea kusimamia common sense na fairness, ninasema so far sijaamua kutoa my 100% support kwa nani kati ya DK na George, lakini pole pole nitazichambua facts za pande zote mbili na kutoa uamuzi, halafu hata na mimi ninaweza kuishia kuchukua fomu vile vile kwa hiyo mkuu, huu ni mwanzo tu yanakuja mengi sana, relax and chill out!
Respect.
FMEs!