Malafyale,
Muheshimu mungu wako, kama kweli unamwamini mungu.
Unaidhalilisha Kyela kwa kuendeleza kumwaga hapa mambo ambayo hayana ukweli wowote.
Maandishi kama haya ndiyo yawafanya watu wengi waamini kama Kyela kuna vurugu au watu wanagombana.
Sisi tumetembelea kata zote 21 bila ulinzi na hakukuwa na sehemu hata moja ambayo angalau hata mtu alitusemea neno baya. Naamini ni hivyo hivyo hata kwa Dr. hakuna mtu hata mmoja ambaye anamtukana akipita barabarani.
Kupingana siasa na Dr. Mwakyembe haiwezi kugeuka ugomvi au uadui. Mwamuzi ni wananchi hapo 2010.
Ifike mahali JF tuunde kamati ndogo ya watu wenye busara na wasio na interests binafsi kwenye haya mapambano. Kazi yao iwe ku confirm au kukanusha habari husika. Siku hizi kuna simu na mitandao kila sehemu, ni rahisi mno kupata ukweli wa jambo. Naamini mtu akiumbuliwa mara mbili kwamba ni muongo, watu wote watamdharau.
Malafyale ni mtu muongo ambaye ameamua kutumia PC yake kuandika kila aina ya uongo kuhusu siasa za Kyela. Alifanikiwa kuidanganya JF kule kwenye thread ya Mwakalinga na sasa kesha onja nyama ya mtu, ameona ni nzuri na anataka kuendelea kuitafuna.
Tuwaangalie watu kama hawa kuelekea 2010, watakuwepo wengi. Siku hizi kuchukua picha ni kitu rahisi mno, kwanini walete maneno matupu bila picha?