La umeme Watanzania ni waelewa, wavumilivu na linavumilika. Assuarance hii from "The Horse's Mouth" ni toshelevu. Lakini la maji linavumilika?

Hahaha
 
Kwa hili laumu serikali yako ya ccm kwa kushindwa kazi.
 
Nani ataweza kuwafurusha, sanduku la kura hio sahau, wameshakuwa Kama Gamba la Kobe, ukilitoa Kobe anakufa, inahitaji tu muujiza wa Mwenyezi Mungu
 
Huyo Pascal na yeye ni genge la hao hao ccm! Hapo unapigia mbuzi gitaa.
 
Kwa hiyo mkuu Tangu tupate Uhuru tumeshindwa kuwa na vyanzo vya maana vya umeme?Hali hii inaonesha aina ya viongozi tulionao.
 
Hapa nimemuona bwana Paskali Mayalla mwenyewe ninayemfahamu, keep it up mkuu.
 
Poor Planning.
Poor Leadership.
Lack of Priorities.
Nchi hii haijawahi kutengeneza mpango ukatekelezeka wala haijawahi kuwa na vipaumbele! Maofisa mipango wa serikali hawana wanachofanya ni bora ofisi zao zikafungwa na ajira zao zikafutwa!

Kinachofanywa na serikali ni kutekeleza maono ya kukurupuka ya Rais. Leo hii Rais akiamua kununua magari 1000 ya magereza yatanunuliwa hata bila kuwa na bajeti yake!
 
Awamu hii ya mpito wanajua kusafiri tu, hata aibu hawana. Inasikitisha sana.
Tegemea visingizio, ubabaishaji, chawa kuipigia campaign ya propaganda serikali, kutembea bakuli duniani, ombaomba. Ila kuchapa kazi, kutatua matatizo ya Watanzania, sahau.

Tegemea safari, kongamano, warsha, semina, upigaji kuongezeka.

Tegemea kuchaguliwa viongozi wengi wabovu na kuwatimua viongozi wanaowajibika.

Tatizo ni katiba ni kama mwimbaji taratibu unampa kazi ya kuendesha ndege.

Obvious hana huo uwezo, ndege lazima ipate misukosuko mingi kama sio kuanguka.
 

Paskali, kweli maji ni uhai, kwa maana nyingine ukikosa maji umekosa uhai? Si ndio maana yake, yaani mtu akikunyima maji anakunyima uhai au nimekosea?

Waziri wa Fedha, yeye anasema tuko 74% kitaifa kwa upatikanaji wa maji, naona hizi data za Mwigulu za kwenye makaratasi tu. Wabunge wamepinga vikali sana kuhusu hiyo 74% ya nchi nzima kwa upatikanaji wa maji.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…