HAPANA ndugu
Pascal Mayalla...!!
Unapiga siasa huku ukikwepa kutumia akili yako vyema ili kusema ukweli kuleta tiba sahihi na ya kudumu ya mambo haya kwa taifa letu...!
Ishu ya umeme na hayo mengine maji nk nk kwa hatua ya sasa hazina utetezi unaoweza kukubalika kwa watu wenye akili na ufahamu toka kwa serikali hii ya CCM ya sasa..!
Tatizo la ukame halijaanza leo wala jana. Na utetezi huu si wa kwanza. January Makamba na serikali kwa ujumla ina copy na kupaste tu sababu zilezile za miaka na miaka toka serikali zilizopita...!
Yaani ni takribani miaka 40 sasa utetezi huwa ni huu huu - yaani ukame na kupungua maji tokana na ukame..!!
Ilikuwa hivyo enzi za Hayati Ben Mkapa 1995 - 2005...
Suluhu yake ikawa ni makampuni ya uzalishaji umeme wa kutumia mafuta na ndipo kampuni ya IPTL na zingine zikaingia.. TUKALIWA kama nchi...
Haikuwa suluhu bali tatizo likipozwa tu kwa muda...
Ongezeko la watu na shughuli za uzalishaji kutumia umeme ziliongezeka sana na hivyo mahitaji ya umeme kuongezeka...
Mkapa akatoka zake. Na akaingia mzee wa Msoga Jakaya Kikwete 2005 - 2015...
Tatizo likawa kubwa zaidi na nchi kupitia wakati mgumu sana..
Utetezi ukikuwa ni huu huu, maji + ukame. Huyu akaja na suluhu mbili;
1. Mvua ya kutengenezwa (artigicial rain) toka Malaysia? Singapore? ili ijaze mabwawa yetu ya kuzalisha umeme. TUKALIWA, USHIRUKINA MTUPU..
2. Mradi ya GESI YA MTWARA uliotugharimu karibu trillion 3. NAO TUKALIWA MCHANA KWEUPE bila utatuzi kupatikana..!
Kikwete akaondoka na kuacha shida na matatizo yakiwa palepale..
Akaingia Rais John P. Magufuli 2015 - 2021. Akaipokea shida hii..
Huyu alikuja na approach ya aina yake kwa kutumia ubabe na akili anazozijua mwenyewe pekee..
To some extent aka - stabilize mambo. Umeme ukawa stable karibu kipindi chote cha miaka kama 6 cha uongozi wake. Kama ulikatika, basi mkatiko wake uliweza kuelezeka, watu wakaekewa na kuvumilia...
Kosa kubwa la huyu hata kuleta maswali kiasi cha watu kujiuliza tunafanya nini na tunapelekwa wapi na hawa watu, ni kuachana na mradi wa umeme wa gesi ya Mtwara ambao wao wenyewe walituambia ndiyo suluhu ya kudumu ya umeme Tanzania...!!
U - TURN hii ya ghafla, Ikatushangaza wengi...!!
3trn Tshs zikazikwa mchana kweupe huku tukiona kwa macho yetu...!
Badala yake, Magufuli naye akaja na wazo la kurudi kulekule kwenye umeme wa maji huku akijua lipo tatizo la ukame...
Akaja na mradi wa Stiglers Gorge HEP plant maarufu kama Mwalimu Nyerere HEP Power Station unaokula karibu TZS 8trn.. NA HAPA NI KAMA TUNAKWENDA KULIWA TENA...!!
Sasa watu kama hawa waliotengeneza wenyewe matatizo haya, wanawezaje kuyatatua wao wenyewe tens..?
Mr
Pascal Mayalla ni miaka zaidi ya 35 sasa tatizo hili lipo na approach inayotumika ni ileile kwa muda wote huu huku nchi ikipoteza matrilioni ya shilingi bila tatizo kutatuliwa...??
Hawa ni watu wa namna gani unadhani? Unafikiri wanafeli wapi..?
Ni simple tu. SERA na MIPANGO YAO IMESHASHINDWA na haiwezekani tena kuaminika...
Kama wameshindwa kwa miaka 35 au 40 wanaweza vipi kwa miezi mitatu ijayo...?
TUFANYEJE SASA MAANA NDIYO WAPO MADARAKANI?
Jibu ni Rahisi tu:
1. Tuwafurushe waondoke kwenye mamlaka za kimaamuzi waje watu wangune wenye fikra na mipango tofauti..!
2. Kikwazo ni mfumo wa kisiasa unaozaa mfumo wa utawala wa nchi. Tubadili mfumo wetu wa kikatiba na kisheria, tutengeneze mpya utaozaa mfumo imara wa siasa na utawala unaowajibika kwa wananchi..
That's all. Achaneni na porojo za hawa.