Labda ni dini zetu ndio zinazotuchanganya na kupotosha kuhusu Mungu

Labda ni dini zetu ndio zinazotuchanganya na kupotosha kuhusu Mungu

AlhamduliLlah mimi ni Muislam, siamini katika Miungu namuamini Allah pekee.
 
Dini ni moja tu, Uislam.
Na mkristo nae anasema dini ni moja tu ukristo! Na budha nae anasema dini ni moja tu ubudha! Kuna mamia ya dini hapa duniani kila mmoja anadai upande wake ndio sahihi! Kiufupi masuala ya dini ni kama kubeti! 😂😂
 
Mimi naamini zaidi utakavyo mjua Mungu ndio zaidi utakavyo ujua ukweli na kuwa huru zaidi. Lakini tulichofanya nikujua dini zaidi ya Mungu.

Kwa kuwa mashirika haya ya dini yanataka uzame ndani yao zaidi huku wakituambia bila wao hatutamfikia Mungu basi hawako tayari kukupa nafasi ya kuweza kujua na kutambua uwepo na ukweli wa Mungu.

We fikiria kiundani zaidi, kwa kuwa Mungu ni mmoja sasa kwa nini Mungu aabudiwe katika misingi tofauti na ya ajabu isio kuwa na umoja wa kumuabudu Mungu. Mashirika haya ya dini yanagawanya watu na kufundisha chuki dhidi ya wasio wa dini ya kufanana, hii ikiwa ni ishara ya kukosa umoja kwa Mungu tunaemini ni mmoja.

Kuna njia ya kumjua Mungu zaidi na ukweli kuhusu Mungu lakini umekuwa coiled in someway kwamba ukidadisi sana utalaaniwa na kukufuru. Sijui kama hii ni ukweli, lakini in some kinda of way nafikiri Mungu mwenyewe angependa tumtafute zaidi yeye kuliko jinsi tunavyoelekezwa na mashirika yetu ya dini.
"nafikiri Mungu mwenyewe angependa tumtafute zaidi yeye kuliko jinsi tunavyoelekezwa na mashirika yetu"
Mkuu Eli Cohen kama unafikiri hivyo kwamba tumtafute zaidi Mungu, huyu Mungu amejifunua au kujidhihirisha kwa watu/wanadamu kwa kiasi gani?
 
Back
Top Bottom