Habari ya Liganga imebakia kuwa ni kisima cha kuchotea pesa watawala mafisadi. Wakati ule wa utawala wa msoga, makampuni ya kuaminika katika uchimbaji wa chuma Duniani, yaliutaka mradi wa Liganga, lakini yote yalipigwa chini, baada ya wachina kutoa hongo kubwa kwa mtawala, ikapewa kampuni ya kichina ambayo haijawahi kumiliki mgodi wowote kwao wala mahali pengine Duniani. Tena kampuni ambayo haina hata uwezo wa kifedha. Msoga katika kuwahadaa watu, akaenda mpaka huko Liganga eti kuweka jiwe la msingi. Yalinyimwa makampuni makubwa kama Rio Tinto, makampuni makubwa ya uchimbaji chuma, tena yakiwa yameahidi kuwekeza dola bilioni 3, ikapewa kampuni ya China ambayo kiwango kikubwa cha pesa imewahi kumiliki ni dollar milioni 360, lakini msoga akasema kuwa itawekeza dola bilioni 7. Muda jlivhoenda bila ya kufanyika chochote, hiyo kampuni dalali ikasema kuwa itawaletea kampuni nyingine toka China, wakakubali. Kampuni iliyoletwa, nayo hakuna lolote la maana, ilifanya drilling kwa kutumia machine ya kudrill visima vya maji ili kuhadaa kuwa wameanza kazi!
Ukiwa na watawala mafisadi, usitegemee maendeleo yoyote ya maana maana wanachofikiria zaidi ni wao watapata nini, na siyo taifa litapata nini. Aliwahi kusema mtaalam mmoja wa chuo kikuu kuwa kwa hapa bongo, hata uwe na proposal nzuri kiasi gani, siku unaiwasilisha kwa Waziri, jambo kubwa analosubiria kusikia kutoka kwako, ni yeye waziri atanufaika vipi na huo mradi, kama hicho kipengere hakipo kwenye kauli yako, kamwe, hiyo proposal yako haiwezi kupita, itabakia unadhangaa proposal za miradi ya kipuuzi kabisa ikipitishwa, kwa sababu tu wale wenzio wametanguliza kumwambia waziri atakuwa na mgao gani!