Ladha ya chumvi kwenye maji ya Kilimanjaro inasababishwa na nini?

Ladha ya chumvi kwenye maji ya Kilimanjaro inasababishwa na nini?

Maji ya Kilimanjaro hapo awali hayakuwa na ladha ya chumvi, ila haya ya siku hizi hili tatizo limekuwa sugu, nini sababu ya haya maji kuwa na ladha ya chumvi chumvi? Na ukikagua packaginh yanaonekana ni authentic kabisa, sio fake..
Maji halisi ya Kilimanjaro ni yale yanayozalishwa na kiwanda cha Bonite Bottlers Moshi na kwa kiasi kikubwa yanasambazwa mikoa ya kaskazini na ya jirani.Haya mengine yanayouzwa Dar pamoja na mikoa mingine yanazalishwa hapahapa Dar kwenye kiwanda cha CocaCola yaani wanatumia formula ileile kama wanayotumia Moshi.Hivyo utaona utofauti wa ladha
 
Ukiyanywea kaskazini ni mazuri sana ila ukinunua kwa hapa dar ni full chumvi. Kuna mtu aliniambia nikambishia ila mwisho na mimi nikajionea
 
Maji ya Kilimanjaro hapo awali hayakuwa na ladha ya chumvi, ila haya ya siku hizi hili tatizo limekuwa sugu, nini sababu ya haya maji kuwa na ladha ya chumvi chumvi? Na ukikagua packaginh yanaonekana ni authentic kabisa, sio fake..
Kuna uhuni nadhani ni sabotage au yapo yanayozalishwa kihuni hapo DSM
 
Juzi nimenunua packet ya Lita Moja pieces 6 Kwa 2,500/- nilichoka sana! Packaging sawa ila ndani Yana chumvi!! Na Kuna ambayo ya nusu Lita nanunua 5500 yenyewe yapo poa!! Kuna tatizo kubwa
mkwe ulinunua ya dawasa
 
Hayo maji yatakuwa fake, kuweni makini sana,hata K vant nasikia zipo fake

Pia last week nilinunua soda water (kampuni ya coke) siku zilikuw tofauti lakini soda zote zile hazikuwq na gas
hapa Tanzania kitu ikishapata soko kinachofuata huwa ni feki,.
 
Kilimanjaro wanauzia jina tu na sio ubora. Ubora ni Hill, afya
 
Maji ni Dew Drop, Dasani na Afya The rest yana chumvi sio Kilimanjaro tu hata Uhai na Masafi ni ovyo sana, Kwa Regional brand nikiwa Tanga ntakunywa Amani, Nkiwa Moro ntapiga Udzungwa nkiwa Nyanda za juu ntapiga Hill
 
Maji ya Kilimanjaro hapo awali hayakuwa na ladha ya chumvi, ila haya ya siku hizi hili tatizo limekuwa sugu, nini sababu ya haya maji kuwa na ladha ya chumvi chumvi? Na ukikagua packaginh yanaonekana ni authentic kabisa, sio fake..
Quality ya hayo maji ilipotea alipofariki Mengi
 
Maji ya Kilimanjaro hapo awali hayakuwa na ladha ya chumvi, ila haya ya siku hizi hili tatizo limekuwa sugu, nini sababu ya haya maji kuwa na ladha ya chumvi chumvi? Na ukikagua packaginh yanaonekana ni authentic kabisa, sio fake..
Maji pendwa ila kwa sasa da acha tu!!Ipo hivi: Maji yote ya Chupa yanayouzwa Madukani yanapatikana kwa process inayoitwa Reverse Osmosis. Kwenye Reverse Osmosis Maji yenye Chumvi (maji ya bahari na ya visima) yanapitishwa kwenye Membrane yakiwa na pressure na Umeme, yanapotoka upande wa pili yanakuwa ayana chumvi ata kidogo hii ndo formula ya maji yote mfano hapa Tanzania Uhai, Due Drop, Kilimanjaro, Ndanda, Udizungwa etc.Kwa mimi Maji ya Kilimanjaro kuwa na Chumvi 1. Mashine yao ya RO inatakiwa kufanyiwa Callibrations au 2. Kuwa Serviced (kubadilisha filters etc- kwani kuna mambo matatu kama hayapo sawa maji yanayopita kwenye RO system yatatoka na Kachumvi kidogo kama yalivyo maji ya Kilimanjaro: Wakitaka maji yao yarudi kuwa matamu kama zamani inawezekana waje tu tuwasaidie. Yupo Dogo anaunda RO system 100% Locally Dar es salaam, So inawezekana Kuhufumua mtambo mzima wa Kilimanjaro RO water making system na kuufuma upya. Wakati mtu anataka funguwa kiwanda cha maji ya kunywa ya Chupa- anaekutengenezea RO system lazima apime wingi wa Chumvi maji utakayotumia kujaza kwenye chupa! Iwapo settings za RO system zikachezewa(settings za Umeme unaotakiwa+ pressure) maji yatakayotoka yatakuwa na chumvi kiasi.
 
Mi haya maji ya chupa huwa nakunywa, yaliyonishinda ni Uhai pekee sababu ya kuwa na harufu kama madawa hivi na uchungu
 
Hayo maji kuna wahuni wanayachakachua hapa dar kwa kutumia chupa za kilimanjaro

Nunua kwenye maduka yanaoeleweka
Big NO. maji kwa sasa wanatumia ya visima sio toka kilimatinde as it was before, siku hizi siyatumii kabisa na wala siyauzi tena. Mzee Mengi alisimamia quality control hawa vijana wake wame fail big time na ndio kufa kwa Kilimanjaro water. Bora wayaite Bore hole water...au kisima kili.
 
Mi haya maji ya vhupa huwa nakunywa, yaliyonishinda ni Uhai pekee sababu ya kuwa na harufu kama madawa hivi na uchungu
Kuna ndugu zangu kadhaa wakinywa hayo maji wanaumwa sana vichwa, nilijaribu siku moja waliponitembelea nyumbani nikawamiminia kwenye glass bila wao kuona chupa nilimoyatoa, baada ya kama nusu saa wakaniomba panadol
 
Nahisi zamani yalikuwa yanatoka moja kwa moja kutoka Moshi na yalikuwa halisi kutoka mtoni ila ile idea ya ulazima wa maji kutoka kwenye vyanzo asili vya mito umeondoka baada ya management mpya kuja na wazo la kuwa na viwanda popote bidhaa yao inapouzika.

So kama Dar hakuna vyanzo vya maji ya mto wanategemea kuchimba visima lazima hii shida itokee na ubaya wa maji ya kisima changanya madawa utakavyochanganya lazima kwa anayejua ajue,kwa sasa tumia Hill Water naona kidogo yana asili ya mtoni nasikia yanazalishwa Bagamoyo
 
Ukiyanywea kaskazini ni mazuri sana ila ukinunua kwa hapa dar ni full chumvi. Kuna mtu aliniambia nikambishia ila mwisho na mimi nikajionea
Inawezekana Settings za mitambo ya Dar (kwenye chumvi nyingi-Kuliko Shirimatunda Moshi) ni Settings za Mashine ya RO ya Moshi
 
Mi haya maji ya chupa huwa nakunywa, yaliyonishinda ni Uhai pekee sababu ya kuwa na harufu kama madawa hivi na uchungu
Sijawahi kuona maji mabaya kama brand ya Uhai. Ladha yake ni kama magadi hivi.
 
Back
Top Bottom