Ladha ya chumvi kwenye maji ya Kilimanjaro inasababishwa na nini?

Ladha ya chumvi kwenye maji ya Kilimanjaro inasababishwa na nini?

D2BE0F2B-543F-4D1D-9895-F80AF99DF5B2.jpeg

Mchawi wa Kilimanjaro Water ni hicho control Box hapo juu- kuna settings azipo sawa.
 
Nahisi zamani yalikuwa yanatoka moja kwa moja kutoka Moshi na yalikuwa halisi kutoka mtoni ila ile idea ya ulazima wa maji kutoka kwenye vyanzo asili vya mito umeondoka baada ya management mpya kuja na wazo la kuwa na viwanda popote bidhaa yao inapouzika.

So kama Dar hakuna vyanzo vya maji ya mto wanategemea kuchimba visima lazima hii shida itokee na ubaya wa maji ya kisima changanya madawa utakavyochanganya lazima kwa anayejua ajue,kwa sasa tumia Hill Water naona kidogo yana asili ya mtoni nasikia yanazalishwa Bagamoyo
Hill water na Udizungwa source yao ya maji ipo sawa na maji ya mtoni so RO system yao inawork vizuri- Kilimanjaro water Source ya maji Shirimatunda Moshi ni tofauti na Dar factory , Inaonekana Kuna settings azipo sawa so kiasi fulani cha Chumvi kinapita kwenye RO system zao
 
Kuna ndugu zangu kadhaa wakinywa hayo maji wanaumwa sana vichwa, nilijaribu siku moja waliponitembelea nyumbani nikawamiminia kwenye glass bila wao kuona chupa nilimoyatoa, baada ya kama nusu saa wakaniomba panadol
Maji nyumbani ni bora uwe unachemsha mwenyewe. Na ukichemshia mkaa ni bora. Ukiweza kutumia kuni ni bora zaidi kwani yanakuwa na taste ya moshi ambayo naipenda sana. Chemsha, chuja, weka kwenye mtungi msafi yapoe.
 
Maji nyumbani ni bora uwe unachemsha mwenyewe. Na ukichemshia mkaa ni bora. Ukiweza kutumia kuni ni bora zaidi kwani yanakuwa na test ya moshi. Chemsha, chuja, weka kwenye mtungi msafi yapoe.
Tatizo maji yetu wameyatreat, hayanyweeki kutokana na madawa wanayoweka kuyatibu, tunachofanya tunavuna rain water ni mara 100 bora kuliko hayo ruwasa, ila tukiishiwa option ni chupa
 
Tatizo maji yetu wameyatreat, hayanyweeki kutokana na madawa wanayoweka kuyatibu, tunachofanya tunavuna rain water ni mara 100 bora kuliko hayo ruwasa, ila tukiishiwa option ni chupa
Unataka kusema madawa wanayoweka hayafai kwa matumizi ya binadamu au? Duniani kote maji ya bomba huwa treated. Hakuna maji yanatoka eg kwenye mto au ziwa na kupelekwa direct kwa watumiaji bila kuwekwa dawa.
 
I know all of that
Kama uko Dar, kinachofanya maji yale na ladha mbaya ni nature ya maji yenyewe na sidhani ni dawa. Sehemu kama Kilimanjaro maji yana ladha nzuri sana japo nayo yanawekwa dawa.
 
Hata ukinunua kwenye magari yao maji ya chumvi tu yashanishinda mim zamani Mengi akiwepo yalikuwa hayana chumvi
 
Ukiyanywea kaskazini ni mazuri sana ila ukinunua kwa hapa dar ni full chumvi. Kuna mtu aliniambia nikambishia ila mwisho na mimi nikajionea
Sio kweli nipo kaskazini na maji ndio radha hiyo hiyo ya Chumvi chumvi nimebadili wakala naona yapo hivyo hivyo nimejaribu Jibu naona sio mbaya kidogo..
 
Maji halisi ya Kilimanjaro ni yale yanayozalishwa na kiwanda cha Bonite Bottlers Moshi na kwa kiasi kikubwa yanasambazwa mikoa ya kaskazini na ya jirani.Haya mengine yanayouzwa Dar pamoja na mikoa mingine yanazalishwa hapahapa Dar kwenye kiwanda cha CocaCola yaani wanatumia formula ileile kama wanayotumia Moshi.Hivyo utaona utofauti wa ladha
Daah nipo kaskazini naona radha ya chumvi hii kauli ningekua kusini ungenikamata...
 
Maji ya Kilimanjaro yanatokana na mfumo wa RO hivyo basi mashine inayofanya kazi hiyo ile membrane filter inahitaji kubadilishwa pia kabla ya kuzalisha maji hayo wawe wanafanya flashing kuondoa particles za fluoride.
 
Bei tu ingekushtua....

Maana Bei ya Jumla ya Lita Moja maji ya Kilimanjaro ni elfu nane na mara nyingi yanakaa 12.
Bei ilinitisha sana, ila muuzaji kajifanya ni promoter WA Kilimanjaro akasema wanachuana na hill
 
Kikubwa ni kuangalia label yao ili kuona kilichomo ndani na faida kwa public health perspective.

Ukiangalia level ya Na(sodium) kwenye kilimanjaro ni kubwa sana ambayo kwa mwenye pressure na hypertension au dalili, siyo mazuri na haitakiwi kuyatumia.

Tulisoma kwenye food microbiology, public health na animal microbiology na kuona kuna maji ambayo ni sahihi kwa matumozi husika kama kunywa, kutumia nyumbani, kwa ajili ya mifugo na mengine hayapaswi hata kutumiwa

Tulifanya coliform test na MPN test na confirmatory test kwa baadhi ya bidhaa za hapa ndani kama jiuce na maji na kugundua mambo kadha wa kadha.

Kikubwa kama utaweza kuchemsha maji ni vyema kufanya hivyo, kama una matatizo ya moyo achana na Kilimanjaro.

Tuwe na utamaduni wa kuangalia kwenye label(lebo) ya bidhaa husika ili kuepukana na dhahama za kujitakia

Screenshot_20221225-224502_Chrome.jpg
 
View attachment 2458589
Duuu, hiyo Sodium balaa
 
Back
Top Bottom