Clepatina
JF-Expert Member
- Apr 8, 2023
- 1,266
- 2,577
Hata awe na pesa kias gani hakuna mwanamke anayetaka kutumia pesa zake kwa mwanaume asiye na mapenz ya kweli.Nakujibu kwa kirefu Dada Masai,
Huyo unayemshangaa anawezaje ni kua amesha timiza ndoto zake zote sasa alichobakiza ni kupata penzi moto moto ili afe kwa tabasamu na sio maumivu,
Niliona interview ya Zari alisema alimuomba mumewe mahari ya Qur'an pekee, hakuona kitu kingine cha kumuomba sababu yeye kila kitu anacho, pesa, magari mazuri, vacations nchi mbali mbali, n.k
Sisi tunaona haiwezekani kwa kua bado tunatafuta ila tukishafika levels za kua na kila kitu unabakiza furaha tu na furaha ya mtu wa miaka 40+ au 50+ ataipata kwa wachini yake sio wazee wenzie waliojichokea kwa maradhi ya kudumu ama wengine wameoa wake zaidi ya mmoja utapata wapi kujiachia na kupetiwa petiwa atakavyo,
Nasikia hao Marioo wanajua mahaba kama wanaenda kozi vile na mama akikolezwa vema why not asitoe ahsante.
Mbutananga naamini alitaka mwanaume wa kutulia nae wazeeke pamoja ila alichokosea ni kutojua kuwa wanaume wanaopenda kulelewa hawanaga mapenzi ya kweli.
Mim ninavyojua mwanaume akikupenda kweli hata kama umemzidi kipato anakua na swaga za masikin jeuri.Yuko radhi akakope kwa rafiki zake amalize shida zake kuliko kuomba mwanamke wake.Na akipata hela atahakikisha anatimiza jukumu lake la kukupatia na wewe kidogo na hii inampa jeuri ya kusimama kukufokea au hata kukuwasha vibao ukizingua.
Mimi na mwenza wangu wote tuna maisha yeti ila kaniapia kuwa hata apoteze kila kitu KAMWE haitokaa akinioa tuishi kwenye nyumba zangu.Akasisitiza kabisa kuwa hata ikibidi tutaishi kwenye chumba kimoja cha kupanga cha msingi kodi analipa yeye.Anajua ninajimudu kwa kila kitu ila ananipaga hela na hajawahi hata kuonyesha dalili ya kutaka hata mia yangu.
Hii kiburi yake inafanya namuheshimu sana na hata akinifokea najua kidume kimefoka na sisubutu kujibu zaid ya kuomba msamaha.
Sasa leta swaga za kuniomba hela siku ujitiie mwanaume kunifokea uone kama sijakuchamba😬😆