Lady Jaydee: Clouds FM ni wanafiki, wanataka wahongwe ili wapige nyimbo za wasanii

Lady Jaydee: Clouds FM ni wanafiki, wanataka wahongwe ili wapige nyimbo za wasanii

kwa kwe hali sio nzuri kwa wakongwe...Stara naye yupo njia panda hajui afanye injili au bongo fleva....Tutarajie visingizio vya kila aina............Any way ninachoweza kumsaidia dadangu Jide ni kuorodhesha vituo vyote ambavyo havichezi nyimbo ya Jide huku MANYARA nao uwachane live.....wamezidi kukubania dada....
 
Ni nani aliyeichagua clouds kama redio ya kuwatoa wasanii ? Tuache kuendeshwa kwa hisia...Muziki ukiwa mzuri utashika tu ?

Huku kwetu kuna wimbo unaitwa nausikia kila kona ninayokatiza unaimbwa "zungusha...zungusha" (nadhani ni wa injili). Sio kwenye maduka ya redio hadi kwa watu wa bodaboda na sasa ni zaidi ya mwaka hata sijawahi kuusikia huu wimbo clouds.....Sasa sijui kwa vipi Jide ulie na clouds...
 
Tatizo letu wabongo ni kukurupuka kusiko na kufikiria... kwa masikio yangu nimeusikia wimbo huu ukipigwa mara kadhaa kwenye kituo hicho halikadhalika niliusikia ukiwa introduced kwenye radio hiyo kwenye kipindi cha xxl na pia nimeisikia mara kadhaa kwenye vipindi tofauti... sitetei may be kama kuacha kuipiga wawe wameacha kuipiga hivi karibuni... ila akisema wimbo wake hauchezwi ni muongo... then inaonesha dhahiri wengi wanaocomment katika hili si wasikilizaji wa radio ila ni ushabiki ndio umetawala.. ni kweli wana matatizo ila si katika hili... binti ana jengine sio suala la wimbo kutokuchezwa hiyo ni sababu ya kujikusanyia idadi ya wafata mkumbo na ushabiki.

Haya Kusaga tumekusikia!lini wafu fm wakatenda haki?labda kama ni msanii kutoka Tatizo Hawataki Tuendelee a.k.a THT!
 
Kama ukifatilia program za superbrand station (kama wanavyojiita). Hawa clouds fm imeonekana dhahiri kabisa ni kikwazo cha maendeleo hapa Tz. Embu nitumie hoja hizi.

1. Kwenye muziki; Hawa clouds wamekuwa wakipiga mziki wa wasanii wao tu ama toka THT au wale ambao meneja wao ni Ruge, au kusaga. Wanatoa promo very selective. Hakuna fairness katika kupiga music na ndo maana hata wakati mmoja wakaingia kwenye ugomvi na mr ii.

2. Siasa; Pia clouds wameonekana kupendelea chama tawala cha CCM katika program zao alafu upande mwingine wana chuki ya dhahiri kwa CHADEMA. Watangazaji wao wawili bwn. Ephrahim Kibonde na Gerald Hando kwenye vipindi vyao moja kwa moja wameonekana wakileta chuki za waziwazi kwa CHADEMA. Ile video ya Lwakatare walijifanya kuikamia sana na kuitangaza huku wakitoa hukumu peke yao badala ya kuiachia mahakama.Ingekuwa kesi ni ya CCM ungemskia Kibonde akisema waziwazi 'suala lipo mahakamani tuwaachie' ila kwa kuwa ni chadema hali imekua tofauti. Clouds ndo mahakama, na hando & kibonde ndo judges. Kifupi hawazingatii ile hoja ya political neutrality au political fairness kama waandishi wanavyopaswa wawe.

3. Maafa yanapotokea..... Clouds wamekuwa wakijipatia pesa kupitia maafa ya watanzania. Nitoe mfano wa mtangazaji wao millard Ayo. Huyu dogo ana page zake kwa internet ambapo analipwa per visit. Kila member wakivisit page yake anaingiza mkwanja. Ok cyo mbaya ni biashara iyo.. Lakini juzi kwene tukio la ghorofa kudondoka ndo akachukulia sehem ya kujipatia ulaji. Kwene facebook anapost stori ya maiti waliopatikana lakini hamalizii anasema ivi 'idadi ya waliofariki hadi sasa iko hapa mtu wangu wa nguvu...' afu anaacha link uvisit. Uyu dogo hana ubinadamu kabisa! Suala la maafa ya kitaifa yeye anatumia kuipatia kipato?

4. Michezo...
 
..kiongozi hilo ni janga la kitaifa,nadhani hawajui style wanayoendanayo will last only for few days...
 
Hao wapumbavu wakina kibonde wasaka ukuu wa wilaya kujikomba komba ccm hawana jipya siku moja litawashuka,redio ambayo kutwa inafarakana na wasanii
 
kama hutaki stress acha kuwasikiliza hao jamaa.Mimi nimefanya hivo sasa hivi sisikilizi story za kijinga kijinga
 
Hii ni redio ya mtu binafsi na si ya serikali.
na wewe ushangae,ile ni redio ya ruge na joseph,wanauhuru wa kutangaza kwa style yeyote ili mradi hawavunji sheria.

Hii redio wanaisema sana hapa lakini cha ajabu inasikilizwa kila kona na style yao ya kutangaza iko unique
 
Mbona kaongea tena kimafumbo kama yeye kweli ni mwanaume na ameamua kufunguka?!
nimesoma tweet zake za leo amemtaja RUGE KABISAAA,PIA AMELAUM KUWA CLOUDS WALIMUHUJUM BAADA YA MUANDAAJ MMOJA KUANDAA SHOW NYUMBAN LOUNGE,HAKUISHIA HAPO AKASEMA RUGE ANAWAKATAZA VIJANA WA THT WASITUMBUIZE NYUMBAN LOUNGE NA ALIMTAJA BEN PAUL KUWA ALIMPA ADVANCE NA HAKUFIKA KWENYE SHOW,PIA NIMESOMA AKISEMA KUWA YEYE SI UNDERGROUND SO HAJUTII NGO,A ZAKE KUTOCHEZWA,NA AMESEMA KUWA ANACONDA (JINA ALILOJIPA( HUWA HAFATI WATU HADI WAMCHOKONOE (WAMFUKUNYUE) SO KWA SASA WAMEMCHOKOZA,,,,KUNA KM TWEET TATU AU 4 NILIZSOMA
 
Hii redio inafanana na zile redio za rwanda zilizosababisha mauaji ya kimbari
Nasikilizaga SPORT EXTRA ndio kipindi kinachoeleweka
 
Mkuu sio wanapondea chadema tu, bali hata wakristu na viongozi wao. Huwa hawathubutu kuongelea jambo lolote la kiislam, wakiofia ugaidi kwenye ofice au nyumbani kwao.
Ishu ya Millard Ayo, nathan yuko poa. Jamaa ni proffessional. Huwa hatoi mawazo yake kuwamilisha mawazo ya watanzania ka hao villaza wengine.
Ishu ya kulipwa sio ishu kwani ni ubunifu. Hata radio/tv yako ya taifa unayoilipia kodi wanatoza hela kwenye matangazo ya vifo au bango tv.
 
Hata kama cloudsfm ni private media, kisiasa hawaja declare kuwa wao ni ccm au chama gani. Wanajiita 'redio ya watu'
asa cha kusikitisha ni pale wanaposhindwa kuwa 'political neutral'
 
ningekuwa na uwezo ningefungua akili ya Gerald, PJ, Kibonde (kwa mifano michache) na kuwaonyesha hatari ya wanachokifanya...

macho yao hayaangalii mbali, wana upofu mkubwa na wa hatari kwao na kwa familia zao.. i pity them... lakini mara nyingine naona kama ni tatizo la ukosefu wa elimu, exposure, vision na kubwa zaidi KUJISAHAU..

Wamejisahau sana hawa watu...
 
Chakushangaza sasa hao mnaolalamika ndio kila siku mnasikiliza, si muache kwani radio maria inayotangaza habari za chadema imefungwa?
 
Chadema ITAKAPOCHUKUA nchi 2015, WATAKOMA UBISHI. Waacheni tu-time will tell
 
Mkuu sio wanapondea chadema tu, bali hata wakristu na viongozi wao. Huwa hawathubutu kuongelea jambo lolote la kiislam, wakiofia ugaidi kwenye ofice au nyumbani kwao.
Ishu ya Millard Ayo, nathan yuko poa. Jamaa ni proffessional. Huwa hatoi mawazo yake kuwamilisha mawazo ya watanzania ka hao villaza wengine.
Ishu ya kulipwa sio ishu kwani ni ubunifu. Hata radio/tv yako ya taifa unayoilipia kodi wanatoza hela kwenye matangazo ya vifo au bango tv.

Uislamu ni dini ya haki.................. au ulikuwa hujui?
 
Chadema ITAKAPOCHUKUA nchi 2015, WATAKOMA UBISHI. Waacheni tu-time will tell

KUMBE CHADEMA NI CHAMA CHA KULIPIZA VISASI? KWA KOSA GANI SASA CLOUDS WAMEWAKOSEA CHADEMA?
Kwa taarifa yako CHADEMA hawatachukua nchi 2012 au mwaka wowote ule. Mpaka sisi na wajukuu zetu tutakufa bila ya CHADEMA kupata urais.........'
 
na wewe ushangae,ile ni redio ya ruge na joseph,wanauhuru wa kutangaza kwa style yeyote ili mradi hawavunji sheria.

Hii redio wanaisema sana hapa lakini cha ajabu inasikilizwa kila kona na style yao ya kutangaza iko unique

Si bureeee umerogwa mkuuu...
 
Back
Top Bottom