Lagos inanuka uchafu na Rushwa!

Lagos inanuka uchafu na Rushwa!

and 300

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2012
Posts
26,398
Reaction score
36,406
1. Watanzania tujifunze kujivunia kwetu japo sisemi sisi Ni Bora kabisa Ila tunajitahidi

2. Binafsi, nimetembelea miji kadhaa Afrika (Kigali, Nairobi, Kampala, Bujumbura, Johannesburg, Durban, Cape Town, Windhoek, Gaborone, Cairo, Algiers, Lusaka) na nje ya Afrika (London, Vienna, Zurich, Madrid, Barcelona, Paris, Amsterdam, Frankfurt, Oslo, Stockholm, Dubai, Doha, Abu Dhabi, Manama, Muscat, Jeddah, Tokyo, Beijing) Ila sijawahi kuona mji mchafu kushinda Lagos.

3. Picha linaanzia airport hapo Ni mwendo wa uchafu kuanzia chooni, Hadi vibanda vya biashara (mbali na kuombwa rushwa na Immigration, customs na polisi wa kawaida). Ukiingia mtaan ndo utajua umefika mji wa namna gan. Hakika Lagos wanaupiga mwingi!

images (8).jpeg
images (1).jpeg
download.jpeg
images.jpeg
images.jpeg
images (5).jpeg
 
Wewe ukiona watu wako tayari kufa maji almradi wafike Ulaya; watu wanasambaa na kulowea kwenye Nchi nyingine, siyo kwamba (wanaijeria) wanapenda kulowea, shida na mustakabali usio wa uhakika ktk Nchi yao ndiyo unawafanya kukimbia kwao. Waethiopia, wasomalia, hali kadhalika. Tz tuko vizuri.
 
Ni kweli Mkuu. Nilipigwa na butwaa day 1 natua Murtala Muhammed airport, Lagos Kwa yafuatayo,
1. Visa on arrival (nimekaa foleni Zaid ya masaa 4),

2. Trolley za kubebea mizigo zinalipiwa tofaut na airports nyingi ambako huwa ni bure.

3. Immigration, Customs na Polisi wanaomba rushwa bila woga.

4. Taasisi za Umma (Hospitali, vyuo vikuu miundombinu ya ovyo kupitiliza, vyoo vimefurika mpaka pomoni),

5. Barabara nazo msala mtupu (mashimo mwanzo-mwisho)
 
Mkuu kweli hapo ni pachafu au sio ila matajiri wa nigeria ni wanakaa banana island huko ikonyi, huko mkuu ni nyoko sana, billionaires wanaishi huko masta na kuna sehemu kama saba ivi, kuna lekki, victoria island na eko atlantic na ikeja, hizi sehemu nlizotaja mzee WEKA MBALI NA WATOTO, usije ukafananisha na tanzania kabisaaaaaa, NI NOMAAAAAAA
Kwa hiyo kumbe Wanigeria huwa wanatuonyesha mapicha ya City Centre pekee siyo?

Nijuavyo Lagos ni boonge la Jiji lenye mandhari safi
 
Mkuu kweli hapo ni pachafu au sio ila matajiri wa nigeria ni wanakaa banana island huko ikonyi, huko mkuu ni nyoko sana, billionaires wanaishi huko masta na kuna sehemu kama saba ivi, kuna lekki, victoria island na eko atlantic na ikeja, hizi sehemu nlizotaja mzee WEKA MBALI NA WATOTO, usije ukafananisha na tanzania kabisaaaaaa, NI NOMAAAAAAA
Ikeja Uswazi tu mbona
 
Miji misafi zaidi mitatu uliyojieonea ni ipi?
 
Back
Top Bottom