Laini za simu kufungwa, akaunti za pesa kubaki

Nimeshachoka kulalamika kunung'unika na sasa nimechoka kuandika nasubiri tar20 mteja wa simu yangu ninae tayari.
 
Kachomoe pesa zako fasta, usije kuangua kilio hapa
 
wadaiwa wa Mitandao ya SIMU na wadai wa miliki wa laini je huku mitaani itakuwaje; ghafla mdeni wako hapatikani kwa simu. JE SANDUKU LA POSTA litahusika?
 
Naanza kuilaumu serikali kila mtu then mimi mwenyewe katika suala zima la usajili wa laini, najutia kwanini sisi Watanzania huwa tunakurupukia mambo ambayo hatuyawezi. WACHA WAFUNGE TU!
 
Kupata tuu passport lazima uwe na kitambulisho cha NIDA

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndo hapo nionapo wamechemsha... unaanzaje kulazimisha matumizi ya kitambulisho cha taifa wakati hujagawa hicho kitambulisho cha taifa??? Utaratibu wa sms nao ni kujikusanyia hela tu... wachache sana wamefanikiwa kupata namba za NIDA kwa sms....
 
Kama kitambulisho cha NIDA ni msala hio passport itakuaje jamaa yangu

Sent using Jamii Forums mobile app
Cha ajabu kingine ni kuwa
1. Kitambulisha cha taifa
2. Passport
3. Driving licence
4. Kitambulishi cha kupihia kura

Hivyo vyote vina almost info za kufanana.... sijui kwa nini info moja inakusanywa na mamlaka nne za serikali na kila moja ikitumia gharama kulisanya taarifa hizo....

Mfano
Jina, umri, alama za vidole, picha etc
 
Nilivyo pata kitambulisho nilikwenda kusajili laini yangu ya tigo Sasa Leo nakwenda kusajili ya halotel ikagoma namuuliza jamaa kulikoni ananiambia kitambulisho chako kimesha sajili laini tano hivyo huwezi kusajili tena nilibaki kuduaa Kama nimechomwa na miba vile. Niiyombe serekali hili zoezi limesha oza limesha ingiliwa na wajanja wa mjini tufanye utaratibu was kuwazibiti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…