Laiti ningelijua mapema, nisingelinunua lile shamba

Laiti ningelijua mapema, nisingelinunua lile shamba

Asante.

Ndio nimelizingatia hilo na ndio sababu ya Sisi kusitisha taratibu za kufanya hiyo Shughuli kwenye Shamba tunalolimiliki kwa sasa
au unaweza jengea uzio yani kwa maana shamba zungushia fensi ili mifugo yenu iwe ndani kwa ndani na kijana wakukatia majani na kuilisha mifugo,

fugeni kisasa zama zimebadilika na population ni kubwa ya watu huwezi achilia mifugo itembee kila kona na ikaharibu mazao ya watu,fugeni kisasa na ndiyo kwenye hela zaidi
 
Nilivoelwa alinunua shamba la mikorosho lipo barabarani ila anafuga kwahiyo linamkosesha fursa za kulishanmifugo yake kwani lipo karibu na maeneo ya watu wengine analazimkka kutafuta eneo lingine japo la mbali na hilo ili aweze kufuga anaeneo kubwa la ekari 10

Sijui ni hivohivo ama😀😀
Hata mimi nimemuelewa hivyo...lakini anaweza kuligawa hilo shamba na kacha hata heka tatu kwajili ya malisho. Kama halina nyasi apande nyasi
 
Hata mimi nimemuelewa hivyo...lakini anaweza kuligawa hilo shamba na kacha hata heka tatu kwajili ya malisho. Kama halina nyasi apande nyasi
Ekari 10 kwa unenepeshaji zinatosha kabisa, yeye anafikri ng'ombe wa kunenepesha wanahitaji kuzurura. Kwa ufupi ili afanye unenepeshaji wenye tija anatakiwa atumie mfumo wa feedlot!
 
au unaweza jengea uzio yani kwa maana shamba zungushia fensi ili mifugo yenu iwe ndani kwa ndani na kijana wakukatia majani na kuilisha mifugo,

fugeni kisasa zama zimebadilika na population ni kubwa ya watu huwezi achilia mifugo itembee kila kona na ikaharibu mazoe ya watu,fugeni kisasa na ndiyo kwenye hela zaidi
Asante kwa mawazo mazuri

Inawezekana kufuga kwa kuwakatia malisho lakini itahitaji pesa nyingi na nguvu kazi kubwa kubwa sana kulingana na malengo yetu.

Malengo ni kumiliki idadi kubwa ya mifugo hivo hili wazo linakuwa ngumu kutekeleza kama mfuko haujitoshelezi

Pia nadhani Kule kusini bhado kuna maeneo mengi na makubwa yanayofaa kwa malisho hivo itasaidia kupunguza gharama.
 
Hata mimi nimemuelewa hivyo...lakini anaweza kuligawa hilo shamba na kacha hata heka tatu kwajili ya malisho. Kama halina nyasi apande nyasi
Shamba tayari lina mikorosho na ishakuwa mikubwa, kuotesha nyasi itakuwa changamoto uko mbeleni mfugo utakapoongezeka.
 
Sasa unakuja kuhangaika na Sisi huku badala uende hapo halmashauri uulize hayo maswali wewe unahangaika na akina cc mahondow? Majibu hayo yatapatikana kwa afisa mifugo wa wilaya.
Ningeweza kufanya hivyo pia, lakini napendelea kutumia majukwaa kama haya kwa faida ya wote
 
Ekari 10 kwa unenepeshaji zinatosha kabisa, yeye anafikri ng'ombe wa kunenepesha wanahitaji kuzurura. Kwa ufupi ili afanye unenepeshaji wenye tija anatakiwa atumie mfumo wa feedlot!
Asante

Lengo si unenepeshaji tu, pia na ufugaji. Hivyo sitoweza kufuga kwa feedlot

Pia, kutumia feedlot pekee itagharimu pesa nyingi ukilinganisha na kwenda machungani ukizingatia shughuli hii itafanyika mkoa wa Mtwara, ambao gharama ya vyakula ipo juu.
 
Je, Ni Vijiji/Maeneo Gani Mkoani Mtwara Yametengwa Rasmi Kwa Ajili Ya Malisho ?
Fika ofisi ya Kijiji watakupa mwongozo. Uandaaji wa ramani ya Matumizi Bora ya Kijiji huwa ni shirikishi (kama kuna mpango wa matumizi bora ya ardhi). Kwahiyo viongozi wa vijiji husika wanajua.
 
Asante kwa mawazo mazuri

Inawezekana kufuga kwa kuwakatia malisho lakini itahitaji pesa nyingi na nguvu kazi kubwa kubwa sana kulingana na malengo yetu.

Malengo ni kumiliki idadi kubwa ya mifugo hivo hili wazo linakuwa ngumu kutekeleza kama mfuko haujitoshelezi

Pia nadhani Kule kusini bhado kuna maeneo mengi na makubwa yanayofaa kwa malisho hivo itasaidia kupunguza gharama.
sawa mkuu all the best
 
Hakuna vijiji vilivyotengwa kwa malisho ya mifugo Mtwara labda kwa mkoa wa Lindi bado kuna maeneo makubwa yenye mapori unaweza kujificha huko.
Ukitaka kuliuza hilo nitangazie bei tu
Ni takribani miaka 8 tangu niliponunua pori lenye ukubwa wa ekari 10 katika kijiji cha Nnyengedi mkoa wa Mtwara na kuligeuza kuwa Shamba la Mikorosho.

Shamba ambalo halipo mbali sana na barabara kubwa na makazi ya watu. Lilozungukwa na Mashamba ya wanakijiji na Wawekezaji wengine kutoka mjini.

Fauka ya yote, hiyo imekuwa kama msumari wa moto moyoni mwangu, na si faida kwani imenitenganisha na fursa ya Unenepeshaji na ufugaji wa Wanyama kama Ng’ombe na Mbuzi katika Shamba hilo.

Inanilazimu kuingia gharama kubwa ya kutafuta eneo lingine zuri mbali na mashamba ya wakulima, karibu kabisa na maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya Malisho

Je, Ni Vijiji/Maeneo Gani Mkoani Mtwara Yametengwa Rasmi Kwa Ajili Ya Malisho ?

Maongezi yetu yalimalizika huku nikiachiwa swali hilo.
 
Mkuu otesha malisho Ya mifugo Yako u switch kwenye fatten farming business, otesha juncao grass 5 acres na Rhodes grass 5 acres, sio mpaka utengewe maeneo ya malisho mkuu.
 
Ningeweza kufanya hivyo pia, lakini napendelea kutumia majukwaa kama haya kwa faida ya wote
Hapa mkuu huwezi kupata jibu la moja kwa moja kuliko ungeenda halmashauri! Huko wangekupa orodha ya vijiji vyote vilivyopimwa!
 
Fika ofisi ya Kijiji watakupa mwongozo. Uandaaji wa ramani ya Matumizi Bora ya Kijiji huwa ni shirikishi (kama kuna mpango wa matumizi bora ya ardhi). Kwahiyo viongozi wa vijiji husika wanajua.
Asante sana leaplai
 
Hakuna vijiji vilivyotengwa kwa malisho ya mifugo Mtwara labda kwa mkoa wa Lindi bado kuna maeneo makubwa yenye mapori unaweza kujificha huko.
Ukitaka kuliuza hilo nitangazie bei tu
Haliuzwi, kama unahitaji Shamba la mikorosho lipo moja kijiji cha Maundo nilinadishiwa.
 
Mkuu otesha malisho Ya mifugo Yako u switch kwenye fatten farming business, otesha juncao grass 5 acres na Rhodes grass 5 acres, sio mpaka utengewe maeneo ya malisho mkuu.
Shamba lina mikorosho, Hakuna namna linaweza tosha kulima nyasi za kulisho mifugo mingi kulingana na malengo yangu.
 
  • Thanks
Reactions: al1
Back
Top Bottom