Lakini kusema ukweli Zuhura hakutosha ile nafasi! Kitu pekee aliongeza ni Press tu, kwenye Branding alifeli

Kile kitengo kinafaa watu waliokubuhu kwenye propaganda
 
Labda kuna mtu atuwekee Jd's za hiyo kazi ili tupime alitosha au hakutosha.

Kumbrand Rais? Ni kazi ya CCM kumbrand mwenyekiti wao ili achaguliwe muhula mwingine na apeperushe benders yao uchaguzi mkuu.
 
Mteuzi alipata urais kwa upendeleo (sio kwa uwezo) naye akamteua Yunus kwa kuangalia jinsia na sio uwezo.

Wote wana uwezo duni.
 
Msimlaumu zuhura,,hakuna kitu kigumu kama kupromoti bidhaa mbovu sokoni. Kama huna C tatu hutaelewa.
 
Namshauri mama amteue semaji la simba arithi nafasi ya zuhura. Hili semaji la simba litafaa sana kama lengo ni kuchonga uongo uwe ukweli.
Ila tuache uongo, kudos kwake zuhura kwa ku-englishsize ikulu na zile "Pless lirease" zake za kimombo safi.
 
Unasema hayo kwa kuwa hujui namna serikali inavyofanya kazi. Msemaji wa Ikulu hana mamlaka ya kuongelea kuhusu matatizo ya umeme wala kujibu hoja za ujumla za wananchi wakati mawaziri wa sekta na makatibu wakuu wapo. Msemaji mkuu wa wizara ni katibu mkuu akisaidiwa na msemaji wa wizara, siyo mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu. Msemaji wa serikali anaweza kusaidia wizara hizi kutoa ufanunuzi lakini nafasi ya mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu haitoi fursa hiyo. Kwa miaka mingi tumeshauri kuwepo mabadiliko ya muundano wa kutoa taarifa wa serikali lakini mapendekezo yote yamedharauliwa.
Sasa tuone kama kuondoka kwa Zuhura kutapelekea Samia kuacha kushambuliwa au msemaji ajaye ataweza kumtetea.
 
Ni vigumu kum brand mtu asiyeweza ku brandika.

Yani ni hivi, mchonga kinyago hata akiwa fundi mzuri vipi, usipompa mti mzuri wa kuchonga kinyago hawezi kuchonga kinyago kizuri.

Sasa kama rais hana interest ya kutoa hotuba kila mara, Mkurugenzi wa Habari Ikulu atamlazimishaje rais kutoa hotuba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…