Kwenye Ukatoriki, Yeyote anayetamani kuwa Padre anaweza kuwa Padre, wapo Mapadre ambao Wazazi wao waliwalazimisha kwenda Seminari, Kuna wengine wamekua Mapadre Kwa sababu aliona Baba mdogo, Mjomba, n.k Kawa Padre...!
Na katika Mapadre wapo ambao wameitwa kabisa kumtumikia Mungu, na ndiyo hao wanakua na Karama za Uponyaji n.k.....!
Ila ukija Kwa Watumishi wa Mungu Kama kina Mwalimu Mwakasege, kwao Uchungaji haukua chaguo, ila waliitwa wakiwa kwenye Shughuri za zingine, na ilibidi waache Shughuri zao kumtumikia Mungu, na Wachungaji Aina hii hawahitaji kwenda Chuo Cha Biblia kumjua Mungu, hawahitaji kusoma Theology n.k, Mungu mwenyewe huwafundisha watu Hawa Kwa njia tofauti.
Hutokea Kwa Watu kama kina Marehemu Father Nkwera, ule wito ndani Yao, ule Moto ndani Yao unakua unafukuta, Roho wa Mungu anakua amefinywa kufanya kazi yake, ndiyo Wachache wa Aina yake wanaamua liwalo na liwe, na pale uongozi wa Kanisa unapogundua hawana chaguzi nyingine Zaidi ya kuwatenga watu wa Aina hiyo...!
Wanazo sababu zao, KKKT, Wasabato, Anglikana na Makanisa aina hiyo pia Yana sababu kama za Wakatoriki ila wao wamejitofautisha kidogo.
Cha Ajabu wote wawe Mapadre ama Wachungaji wanahubiri kuwa huu ni wakati wa Mwisho, na wengine husema tupo kwenye Dakika za Nyongeza, lakini Kuna Verse za Biblia wanazisoma na ama hawaziamini ama wanazipuuza, Kwa sababu sio wote wamepewa uwezo wa kuponya, wanaona si sawa.
Wanasahau
Matendo ya Mitume 2 : 17-21 inasema Nini....!!!