TANZIA Lala salama Padre Felician V. M. Nkwera

Emaus centre: Ukifika daraja la kijazi kama unaelekea Mwenge upande wa kulia kuna ile petrol station sasa kwa mbele hatua chache tu utaona kibao na njia inayoelekea Emaus center. Huduma ni kila siku.
Pia kuna Agape center ipo Mbezi Kibanda cha mkaa kuna huduma ya Karismatiki pia.
Kwa marehemu mama mwanza ndio EMAUS? Umemuelekeza vizuri, kama hajaelewa mwambie aende nyuma ya iliyokuwa stendi ya mabasi ubungo.
 
Yesu alifanya.
Paul alifanya.
Na Watumishi wengi kwenye Biblia walifanya....!

Wewe hujui Kwa Nini Kanisa Katoriki limezuia, Wacha nikupe Darasa.

Mungu ametoa Karama 5 Kwa Watu wake.
1. Pastor, Apostle, Evanjalist, Teacher and Prophet.
Katika hizo Karama Wapo waliopewa Karama za Uponyaji kupitia Jina la YESU, na hakuna Shule utaenda Duniani ukafundishwa kuwa Pastor ama Apostles, ni Mungu mwenyewe Ndo anaweka hiyo Spirit Kwa Mtu.

Kanisa Katoriki Lina Mapadre wa Aina 2, Wapo Mapadre Wana Karama za Uponyaji, wapo Mapadre Wana Karama za Kinabii kina Suguye wakasome, wapo Mapadre wana Nguvu za Uponyaji Mwamposa akasome, na Wapo Mapadre wa kawaida wasio na hizo Karama.

Ukikuta Padre wa Kikatoriki mwenye Karama za Uponyaji Tena Huwa hawana story mingi, utasikia " Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, ninakuamuru............!" Mapepo ama Ugonjwa unaachia, hawana makelele Yale ya "Katika jina la Yesu....."
Binafsi nimehudumu Kanisani nikiwa Kijana Mdogo, wale Vijana ambao husaidia Mapadre kwenye Misa, nimewahi kutumika Kwa Siri na Padre mwenye nguvu ya Uponyaji, akifanya maombezi Kanisani Kwa Siri na Usiku alfajiri, siku 1 Kwa week, Mimi nimkimsaidia huyo Padre, nimeshuhudia Kwa Macho yangu watu wakipona Kila week.

Kanisa Katoriki limezuià hizo huduma Kwa sababu kutakua na Vurugu kanisani wakiruhusu, utakuta Padre ana Karama ya Uponyaji na Askofu wake Hana, itapelekea Padre kuwa na Nguvu Kanisani kuliko Askofu, na baadaye Kanisa litakua na Migogoro.

Ni Sasa baada ya kufumuka haya Makanisa ya kilokole na huduma za kuombea watu, Kanisa Katoriki nao wameanzisha huduma za maombezi ambazo wanaziita Karesmatiki, na huduma hizo zinasaidiwa na Mapadre ama Masister ama Walei wenye Karama ndani Yao, lakini hizo huduma zimetengwa kwenye vituo Maalumu, na hazifanyiki Makanisani.
Daah! Hii kitu uliyoandika bila shaka umeitoa kichwani kwako.
 
Ni wapi unahisi nimetoa kichwani.
Kanisa Katoriki limezuià hizo huduma Kwa sababu kutakua na Vurugu kanisani wakiruhusu, utakuta Padre ana Karama ya Uponyaji na Askofu wake Hana, itapelekea Padre kuwa na Nguvu Kanisani kuliko Askofu, na baadaye Kanisa litakua na Migogoro.
 
Kanisa Katoriki limezuià hizo huduma Kwa sababu kutakua na Vurugu kanisani wakiruhusu, utakuta Padre ana Karama ya Uponyaji na Askofu wake Hana, itapelekea Padre kuwa na Nguvu Kanisani kuliko Askofu, na baadaye Kanisa litakua na Migogoro.
Huo ndo Ukweli....!
Nakumbuka kipindi hicho namsaidia huduma Padre mwenye Karama ya Uponyaji ambaye pia alikua na Karama ya Unabii, alinambia Usimwambie mtu, Mimi nikaona yule Padre anafanya jambo jema Kwa Nini anasema nisimwambie mtu...!? Kwa Nini iwe Siri....!?

Akanambia Kanisa Katoriki haliruhusu huduma za maombezi, lakini Linao Mapadre wenye Karama za Uponyaji.....! Ni kufifisha kazi za Roho Mtakatifu Kwa Watu wake.

Haya Mimi nimekupa sababu Kwa Nini huduma za Maombezi zimezuiwa Kanisani.....!
Na unahisi siko sahihi, Sasa wewe tuambie Kwa huduma za maombezi zimezuiwa ndani ya Kanisa Katoriki ...!?
 
Makanisa yote ya Roman Catholic DSM yaliweka vibao vya kuzuiya wanamaombi wasiingie kanisani sababu ya father Nkwera. Ni padre aliyesaidia kuanza kwa karismatiki katoliki kama utume kutokana na kanisa kutaka kupunguza pressure ya wanamaombi. Pumzika kwa amani baba
 
Nimesoma mahali kanisa (RC) limesimamia mazishi yake ilhali lilimtenga enzi za uhai wake!

Ina maana alikuwa bado anasali RC?
 
Makanisa yote ya Roman Catholic DSM yaliweka vibao vya kuzuiya wanamaombi wasiingie kanisani sababu ya father Nkwere. Ni padre aliyesaidia kuanza kwa karismatiki katoliki kama utume kutokana na kanisa kutaka kupunguza pressure ya wanamaombi. Pumzika kwa amani baba
Screenshot_2025-05-18-07-48-06-004_org.mozilla.firefox.jpg
 
Huo ndo Ukweli....!
Nakumbuka kipindi hicho namsaidia huduma Padre mwenye Karama ya Uponyaji ambaye pia alikua na Karama ya Unabii, alinambia Usimwambie mtu, Mimi nikaona yule Padre anafanya jambo jema Kwa Nini anasema nisimwambie mtu...!? Kwa Nini iwe Siri....!?

Akanambia Kanisa Katoriki haliruhusu huduma za maombezi, lakini Linao Mapadre wenye Karama za Uponyaji.....! Ni kufifisha kazi za Roho Mtakatifu Kwa Watu wake.

Haya Mimi nimekupa sababu Kwa Nini huduma za Maombezi zimezuiwa Kanisani.....!
Na unahisi siko sahihi, Sasa wewe tuambie Kwa huduma za maombezi zimezuiwa ndani ya Kanisa Katoriki ...!?
Sababu uliyotoa ni ya kijinga! Hii inadhihirisha kwamba viongozi katika Roman ni watu wenye wivu!! Jambo ambalo halipaswi kuwa kwa viongozi wa kidini kama wao! Inadhihirisha kuwa pengine hata hawakuwekwa na Mungu mahali hapo!!! Kwanini wakatae kazi ya Mungu kufanyika Kanisani?
 
Kwenye Ukatoriki, Yeyote anayetamani kuwa Padre anaweza kuwa Padre, wapo Mapadre ambao Wazazi wao waliwalazimisha kwenda Seminari, Kuna wengine wamekua Mapadre Kwa sababu aliona Baba mdogo, Mjomba, n.k Kawa Padre...!

Na katika Mapadre wapo ambao wameitwa kabisa kumtumikia Mungu, na ndiyo hao wanakua na Karama za Uponyaji n.k.....!

Ila ukija Kwa Watumishi wa Mungu Kama kina Mwalimu Mwakasege, kwao Uchungaji haukua chaguo, ila waliitwa wakiwa kwenye Shughuri za zingine, na ilibidi waache Shughuri zao kumtumikia Mungu, na Wachungaji Aina hii hawahitaji kwenda Chuo Cha Biblia kumjua Mungu, hawahitaji kusoma Theology n.k, Mungu mwenyewe huwafundisha watu Hawa Kwa njia tofauti.

Hutokea Kwa Watu kama kina Marehemu Father Nkwera, ule wito ndani Yao, ule Moto ndani Yao unakua unafukuta, Roho wa Mungu anakua amefinywa kufanya kazi yake, ndiyo Wachache wa Aina yake wanaamua liwalo na liwe, na pale uongozi wa Kanisa unapogundua hawana chaguzi nyingine Zaidi ya kuwatenga watu wa Aina hiyo...!

Wanazo sababu zao, KKKT, Wasabato, Anglikana na Makanisa aina hiyo pia Yana sababu kama za Wakatoriki ila wao wamejitofautisha kidogo.

Cha Ajabu wote wawe Mapadre ama Wachungaji wanahubiri kuwa huu ni wakati wa Mwisho, na wengine husema tupo kwenye Dakika za Nyongeza, lakini Kuna Verse za Biblia wanazisoma na ama hawaziamini ama wanazipuuza, Kwa sababu sio wote wamepewa uwezo wa kuponya, wanaona si sawa.

Wanasahau
Matendo ya Mitume 2 : 17-21 inasema Nini....!!!
 
Ifike mahali ukweli usemwe, Fr. Nkwera alikuwa akisema anaponya watu ni kama kina mwamposa, wengine tuna ndugu walipoteza maisha pale kwa kuaminishwa wataponywa na walikuwa ni wagonjwa na waliishia kupoteza maisha. Fr. Nkwera alikuwa akisema anaongea na mama Bikira Maria kila siku, wenye Imani katoliki tunajua namna Bikira Maria anavyokuja, sio kwa kujificha au kwa mtu mmoja kila siku, hiyo pia haikuwahi kuthibitishwa, inawezekana alikuwa akisali anaonyeshwa maono lakini si kuongea nae kila siku, akilala akiamka anasema ameambiwa hivi, kesho tena ameambiwa vile. Ni mengi kwa kweli. Honestly Dunia ya leo kuingia Choo cha umma peku eti kinatumia maji ya Baraka ilhali yeye anatumia chake peke yake na viongozi wana vyao ni hatari sana, na ndio maana hawakosagi UTI kwa ninaowafahamu.
we nawe akili yako unaijua mwenyewe, ukweli wako umeutia chumvi nyingi ukaongezea na uwongo juu yake,

1. Tangu lini uti ikasababishwa na kutembea peku? labda ungesingizia gonjwa lingine, lakini sio uti, huu ni uwongo. Na tuseme ulimaanisha uti inasababishwa kwa ku share vyoo, hivi makanisani, misikitini mashuleni na kadhalika kila mtu ana choo chake??? au hukuenda shuleni? na kanisani jee? au wewe popote unapoenda umejengewa na unatumia choo chako mwenyewe??
Kuhusu viongozi wa dini kua na vyoo vyao, wewe shuleni ulitumia choo kimoja na mwalimu wako?, si kuna vyoo vya walimu na vya wanafunzi? yaani nyumbani kwako uwe na choo chako mwenyewe na kwa watu i.e shuleni, kanisani,msikitini napo utake choo chako mwenyewe, ni akili gani hizi?
Please acha kutafuta visingizio kwa vitu visivyo na maana.
 
2. Kusema kua father "alisema" anawaponya wagonjwa sio kweli, hapo umetia chumvi, father pamoja na viongozi wengine wa dini waliopewa karama ya uponyaji na Mungu, wao watakuombea na kukuweka katika njia sahihi, ni Mungu na ni MUNGU tu ndio atakaekuponya kupitia msaada na maombezi yao, ndio maana hata kituo chake pale kinaitwa "kituo cha sala na huduma za maombezi" hapo uliposema kua "amesema anaponya" sio kweli, ni akili finyu za binadamu kutotambua kua ni Mungu anakuponya kupitia maombezi ya watumishi wake, watu wanaoponywa kupitia viongozi hawa ni Mungu anawaponya na sio kiongozi fulani aliekuombea ulijue hilo. Hamna kiongozi wa dini yoyote anaetumia nguvu zake za kibinadamu kumponya mtu, ni Mungu tu ndio anaeponya, labda hukulielewa hilo.

Na unakosea sana, tena sana pale unapowalalamikia viongozi wa dini na hata kuwaita waongo pale shida zako zisipo tatuliwa, kama nilivyokuelezea ni Mungu tu ndio atakaekuponya sio padre, yeye anakuombea tu na kukuweka kwenye njia sahihi. Hujiulizi kwanini wengine wanaponywa na sio wewe? na je watu wote hao walioponywa na kusaidiwa wanasema uwongo?

Uache kuwalalamikia bila sababu za msingi, na pia ujue shida za watu zinatofautiana tena sana, na unakuta wengine shida wanazopata ni kwasababu ya makosa waliofanya, wengine siku zao za hapa duniani zimeisha. Mungu hana formular ya lini na wakati gani atamponya au kumsaidia mtu, na ana makusudio yake ambayo sisi binadamu hatuyajui na hatuwezi jua ndio maana inatupasa kuendelea kumuomba bila kuchoka na pia kubadilika na kuacha maisha ya dhambi. Kuna watu wanaponywa hapo hapo wakishaombewa, kuna wengine wanaponywa baada ya masaa, wengine baada ya masiku miezi na hata miaka.

Shida watu mnapenda mambo marahisi, unataka uombewe siku moja tu upone, wengine hawataki kubadilika na kuacha maisha ya dhambi na katika hali hiyo wanataka waombewe hivo hivo wapone lasivyo kiongozi anaitwa muongo
 
Hivi unaweza kuwaambia waumini wako waende chooni peku kwa kuwa kumesafishwa na maji ya Baraka? Hivyo vyoo wanatumia wakubwa kwa wadogo. We nawe huelewi, huko shuleni na misikitini mnaingia chooni peku?
 
Kumbe unajua kuwa ni Mungu pekee ndie mponyaji, ushuhuda wangu ni huu, mtoto anaumwa, mzazi anampigia simu father, father anamwambia mlete mtoto kanisani tumuombee atapona, mlete kwenye mkesha apate na maji ya Baraka, mtoto anakufa hapo kwenye kituo cha maombezi sababu hakupelekwa hospitali au hakupata huduma sahihi, wewe kama mdogo wako anakufa kwenye hayo mazingira ungesemaje? Si hilo tu kuumwa wote tunaumwa hata marehemu ameumwa akaenda hospitali, iweje wengine awaambie akawaombee na si kwenda hospitali? Kuomba ama kuombewa kupo lakini si kuacha kupata huduma sahihi. Hakuna mgonjwa asiyeamini kama Mungu atamponya mbona wasiende hospitali kuwaponya?
 
Linda sana moyo wako, soma neno ulielewe utamsikia na kumwona Mungu.

Na umtafute Mungu na kushika sheria yake kwa moyo wako wote.

Usiabudu dini, kiongozi wa dini wala jengo linaloitwa kanisa.

Jitafute wewe mwenyewe kama kanisa la Mungu , mwamini Mungu na uwe mwaminifu kwake. Hutajuta!

Warumi 3
9 Ni nini basi? Tu bora kuliko wengine? La! Hata kidogo. Kwa maana tumekwisha kuwashitaki Wayahudi na Wayunani ya kwamba pia wamekuwa chini ya dhambi;

10 kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Hakuna mwenye haki hata mmoja.

11 Hakuna afahamuye; Hakuna amtafutaye Mungu.

12 Wote wamepotoka, wameoza wote pia; Hakuna mtenda mema, la! Hata mmoja.

13 Koo lao ni kaburi wazi, Kwa ndimi zao wametumia hila. Sumu ya fira i chini ya midomo yao.

14 Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu.

15 Miguu yao ina mbio kumwaga damu.

16 Uharibifu na mashaka yamo njiani mwao.

17 Wala njia ya amani hawakuijua.

18 Kumcha Mungu hakupo machoni pao.

19 Basi twajua ya kuwa mambo yote inenayo torati huyanena kwa hao walio chini ya torati, ili kila kinywa kifumbwe, na ulimwengu wote uwe chini ya hukumu ya Mungu;

20 kwa sababu hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria; kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria.

21 Lakini sasa, haki ya Mungu imedhihirika pasipo sheria; inashuhudiwa na torati na manabii;

22 ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti;

23 kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;

24 wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu;

25 ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake,ili aonyeshe haki yake ,kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa MUNGU dhambi zote zilzotangulia kufanywa.
Umeongea vyema sana mkuu, tunahitaji sana kusikia vitu kama hvyo ili tuondokane na mambo km aliyofanyiwa Padri Nkwera
 
nimekulia river saidi nimecheza sana mule ndani kwenye kituo chake cha maombezi!!! Ila ukweli usemwe ukishaanza kuwa muumini wa lile kanisa kuna mawili usipo kuwa zezeta basi utaanza kutembea kwa kuchechemeea!!! Mnisamehe ntakao wakwaza
 
Hivi unaweza kuwaambia waumini wako waende chooni peku kwa kuwa kumesafishwa na maji ya Baraka? Hivyo vyoo wanatumia wakubwa kwa wadogo. We nawe huelewi, huko shuleni na misikitini mnaingia chooni peku?
Unaweza kudhibitisha maji yanayotumika kusafishia vyoo ni maji ya baraka??
No research no comment, (kama hujafanya uchunguzi wa kina usitoe maoni kuepuka kusema uwongo, ni dhambi)
 
Kumbe unajua kuwa ni Mungu pekee ndie mponyaji, ushuhuda wangu ni huu, mtoto anaumwa, mzazi anampigia simu father, father anamwambia mlete mtoto kanisani tumuombee atapona, mlete kwenye mkesha apate na maji ya Baraka, mtoto anakufa hapo kwenye kituo cha maombezi sababu hakupelekwa hospitali au hakupata huduma sahihi, wewe kama mdogo wako anakufa kwenye hayo mazingira ungesemaje? Si hilo tu kuumwa wote tunaumwa hata marehemu ameumwa akaenda hospitali, iweje wengine awaambie akawaombee na si kwenda hospitali? Kuomba ama kuombewa kupo lakini si kuacha kupata huduma sahihi. Hakuna mgonjwa asiyeamini kama Mungu atamponya mbona wasiende hospitali kuwaponya?
Ndio maana nimekwambia ufanye research kwanza, lile sio kanisa ni KITUO CHA HUDUMA ZA MAOMBEZI.

Pili, una mgonjwa mahututi kilichokufanya umpigie simu Father kwanza badala ya kumpigia simu daktari ni nini??

Tatu, na je ungemkimbiza hospitalini akafia mikononi mwa daktari nae ungemlaumu??

swala la kuombewa na kupona linahitaji IMANI, hata wakati wa Bwana Yesu hawakuponywa wote na walioponywa waliambiwa, "ENENDA ZAKO IMANI YAKO IMEKUPONYA."
 
Back
Top Bottom