TANZIA Lala salama Padre Felician V. M. Nkwera

TANZIA Lala salama Padre Felician V. M. Nkwera

Hilo nakubaliana nalo asilimia 100. Padre Pio alifungiwa kwa muda asifanye public services.
Na hata Fatima ilichukua muda kusema hii message haina kasoro.

Mtakatifu Bernadeta pia alipitia mlolongo huo huo....
Lakini sio yaliyokuwa yanafanyika jimbo la Dar Es Salaam.
Ile ni aibu kubwa sana. Maana ni kazi kabisa ya luciferi. Kupigana kanisani. Kuleteana ubabe na mpaka kupelekana mahakamani
Naisi kulikuwa na personal beef kati ya Padre na Askofu Pengo (uhenda toka kipalapala huko) nna jamaa yagu alisomaga Seminary ndogo (form one-Six) Darasa Lao limetoa mapadre wengi na Askofu mmoja hapa Tanzania.Alifanikiwa kuchaguliwa kuendelea na masomo ya upadre Seminary kuu moja nchini Kenya- Mwalimu wake mmoja (Bruda- sio Padre ni mtawa anaweka Nadhiri ya kutooa mpaka kifo)wa huku Seminary Ndogo (alikuwa na personal beef na jamaa-siwezi sema hapa najua ugomvi wao
🤣🤣) alituma report mbaya Kenya kama yeye binafsi kumchoma jamaa kuwa afai kuwa Padre
😭 aliitwa na Rector wa hii Seminary Kenya maana report halali toka Seminary ndogo ilikuwa nzuri na ya kuridhisha-jamaa baada ya kumweleza Rector wa Kenya Ukweli walimkubalia aendelee na Shule lakini mshikaji akaaamua kuachana kabisa na masomo ya Upadr e.Yupo Morogoro anafanya kazi. mara ya Mwisho nilikutana nae Moro pale Samaki samaki hivi karibuni tukala beer na kukumbushana maisha ya Shule na vimbwanga vya Walimu wetu.Ni Lecturer katika one of Universities Morogoro-may Be angeweza kuja kuwa Padre na ata Askofu who knows- Zipo stories nyingi za visasi baina ya hawa makasisi na makasisi au wale walio chini yao! Kuna Visa vingi vilikuwa vinatokea kwenye Seminaries ambavyo wahusika walikuwa wanatimuliwa au wanamaliza shule lakini report zao toka kwa magombera na walezi wao zilikuwa na maoni ya kuwashindishwa kufikia ndoto zao za kusimama madhabahuni mwa Bwana- Kuna Dogo mmoja alifukuzwa Seminary akabeba mabegi yake akaenda lala kwenye Groto ya Bikira maria ya pale Seminarini kwao-
🤣🤣 siku 2 Mafather wkaona hii soo- jamaa ni Baba Paroko mpaka kesho
😁😁
Kuna Mwaka nikiwa Form two huko Rombo kuna Familia Dada yao aliejiunga na Usista toka akiwa na miaka 16,Mama mkuu alimfukuza Usista akiwa na miaka 33.Kaka mtu alitoka Dar akaenda akamchukuwa Dada ake mpaka pale kwa masista alipokuwa anahudumia.akaomba kuonana na mama mkuu ofisini wakiwa watatu- wakiwa ofisini akatoa Barreta 9 millimeters! 🤣🤣 akamwambia sister mkuu wa kile kituo nanukuhuu"Dada angu toka mdogo mpaka sasa yupo nanyi.ajui life ya kitaa na vimbwanga vyake na ajui ata maisha ya ndoa yanafananaje-Kumtoa humu na kumrudisha nyumbani ni Kama mmemuuwa
😭😭So bastola hii hapa muue na kimwili ili twende tukamzike maana huko nje ya nyumba hii.awezi ishi kama sisi...akatoka nje akamwacha dada ake na sista mkuu...baada ya dakika kama 10 hivi Sista mkuu akamwambia Baba wewe nenda wambie familia tupo tunashughulikia swala hili hivyo mwache hapa.Tutawasiliana nanyi ndugu zake maamuzi tutakayofikia juu ya dada yenu. jamaa Akachuuwa mguu wake wa kuku akapiga moto Toyota stout yake.akapitia majani ya Ngombe akarudi nyumbani 🤣🤣yule dada mpaka leo ni sista ila ni bibi kwa sasa
..
 
2018 nilisali hapo kibanda cha mkaa... Mwanzoni nilihisi nimekosea kanisa labda hawa sio wakatoliki kutokana na makelel yao ya kuomba na nyimbo za maapambio na kunena kwa lugha(?)... Padre alivyoingia ndio misa rasmi ya kikatoliki ikaanza
Hivi walikua wakinena Kwa Lugha pia...!?
 
Hilo nakubaliana nalo asilimia 100. Padre Pio alifungiwa kwa muda asifanye public services.
Na hata Fatima ilichukua muda kusema hii message haina kasoro.

Mtakatifu Bernadeta pia alipitia mlolongo huo huo....
Lakini sio yaliyokuwa yanafanyika jimbo la Dar Es Salaam.
Ile ni aibu kubwa sana. Maana ni kazi kabisa ya luciferi. Kupigana kanisani. Kuleteana ubabe na mpaka kupelekana mahakamani
Hicho kilikuwa ndiyo kipindi cha uhayawani wa hali ya juu katika historia ya Kanisa ndani ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam
 
Madhehebu mengi hasa haya ya Katoliki, Anglican na Lutheran hayataki wokovu, yaani hayataki maombi, ukifanya maombi yanataka sheria zao kama litrugia, unatengwa na kanisa ukifanya hayo na hii ndio sababu wahubiri wengi wameamua kuacha Madhehebu na kuanzisha makanisa yao...
Mbona wakatoliki wana chama cha kotume wanajiita wacharsmatic ni wana maombi kwelikweli wanasali kama walokole kabisa.
 
Mbona wakatoliki wana chama cha kotume wanajiita wacharsmatic ni wana maombi kwelikweli wanasali kama walokole kabisa.
Charismatic ni kweli wanasali kama walokole lakini sessions zao haziingiliani na liturjia ya misa ya Parokia yeyote.

Kwa hiyo inamaanisha kuwa Jumapili wataingia kanisani kama kawaida na kusali. Ila baadaye jioni watakwenda kwenye kituo kilichpangwa kwenda kufanya maombi yao
 
Dah JF ya sasa ina vijana wadogo wengi sana inaonekana, haya majina maarufu wanauliza ni nani?!

Anyway RIP Fr. Nkwera, umeishi maisha yako na yamegusa watu wengi sana, upate pumziko la milele Amen
Hata wakubwa kukuzidi hawawezi kumjua kila mtu,na umri wangu mdogo nimesikia huduma yake (sio padre) kupitia jamaa ambaye ni ndogo kwangu.
 
Hata wakubwa kukuzidi hawawezi kumjua kila mtu,na umri wangu mdogo nimesikia huduma yake (sio padre) kupitia jamaa ambaye ni ndogo kwangu.
Poa sumbe sio big deal! Apumzike kwa amani tu kaka ndio kikubwa , sgd wp hiyo?😎
 
Kw Lutheran, naweza sema labda baadhi ya Dayosisi zinaweza kuwa na utaratibu huo.
Kuna mwinjilisti mmoja namfahamu alikuwa anatupigisha sana maombi, na mahubiri yake yalikuwa yanavutia sana full hamasa. Kuanzia morning glory, ibada za katikati ya wiki, semina na jumapili. Mpaka nilipokuja kuhama huko, sijawahi kuskia kuwa amekatazwa kuendesha maombezi.
Fuatilia/uliza uliowaacha kwenye eneo hilo,kwa maelezo yako alishaingia matatani na viongozi wa juu wa kanisa ana akasimamishwa huduma.
 
Long story. Nikipata muda nitaweka version yangu.

Huyu ni Mwalimu wangu wa Sarufi Milambo Secondary akiwa anahudumu chini ya Askofu Mihayo. Ni mzaliwa wa Ludewa na alipata Upadre Jimbo la Njombe by then. Ila alishindwa kuelewana na Askofu Mwanyika na hapo ndipo akakimbilia jimbo la Tabora
Nitaomba tag mkuu nitashukuru sana
 
Mbona Emaus na Agape ni vituo vinavyofanya hizo huduma na kuna mapadre kabisa wanafanya ibada za misa za uponyaji yupo father Msafiri, Father Rimisho na Father Ndemasi na wengine nimewasahau majina .
Yawezekana misimamo ya watu kama marehemu padre nkwera wamelipa kanisa msukumo kuona namna ya kubaki na mapadre wenye karama ndani ya kanisa...wangejitenga wote ingekua mwanzo wa anguko la kanisa.
 
2018 nilisali hapo kibanda cha mkaa... Mwanzoni nilihisi nimekosea kanisa labda hawa sio wakatoliki kutokana na makelel yao ya kuomba na nyimbo za maapambio na kunena kwa lugha(?)... Padre alivyoingia ndio misa rasmi ya kikatoliki ikaanza
Kibanda cha mkaa niliwahi kusali pale kwaya yetu ilienda kuhudumu kwa mualiko,emaus center pia.Binafsi hizi sehemu sikukubali namna yao ya kusali wale ni walokole pure wanaweka ukatoliki kidogo hasa ekaristi.
 
Kibanda cha mkaa niliwahi kusali pale kwaya yetu ilienda kuhudumu kwa mualiko,emaus center pia.Binafsi hizi sehemu sikukubali namna yao ya kusali wale ni walokole pure wanaweka ukatoliki kidogo hasa ekaristi.
Kwani ulokole ni mbaya ndugu?
 
Ifike mahali ukweli usemwe, Fr. Nkwera alikuwa akisema anaponya watu ni kama kina mwamposa, wengine tuna ndugu walipoteza maisha pale kwa kuaminishwa wataponywa na walikuwa ni wagonjwa na waliishia kupoteza maisha. Fr. Nkwera alikuwa akisema anaongea na mama Bikira Maria kila siku, wenye Imani katoliki tunajua namna Bikira Maria anavyokuja, sio kwa kujificha au kwa mtu mmoja kila siku, hiyo pia haikuwahi kuthibitishwa, inawezekana alikuwa akisali anaonyeshwa maono lakini si kuongea nae kila siku, akilala akiamka anasema ameambiwa hivi, kesho tena ameambiwa vile. Ni mengi kwa kweli. Honestly Dunia ya leo kuingia Choo cha umma peku eti kinatumia maji ya Baraka ilhali yeye anatumia chake peke yake na viongozi wana vyao ni hatari sana, na ndio maana hawakosagi UTI kwa ninaowafahamu.
 
Mwili wa Padri Felician Nkwera unatarajiwa kuzikwa Jumamosi Mei 18, 2025 katika kituo chake cha Maombezi kilichopo Ubungo jijini Dar es Salaam


 
Back
Top Bottom