TANZIA Lala salama Padre Felician V. M. Nkwera

TANZIA Lala salama Padre Felician V. M. Nkwera

Alitengwa kwa ajili ya kutokuwa mtii kwa Askofu. RC padri wa Jimbo hajipangii majukumu, anapangiwa na Askofu wake.
Karismatiki sio huduma, ni chama cha kitume kama ilivyo Moyo Mtakatifu wa Yesu, Wanaume Wakatoliki UWAKA, Wanawake WAWATA, na Vijana VIWAWA.
Unaweza kuwa mtii kwa watu na mifumo ya dunia lakini ukawa muasi kwa Mungu

Father Nkwera alishika neno kwa jinsi alivyopokea kwa Mungu wake

Mathayo 10:37-39​

Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili;
wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.
Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili.
Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona.
 
Katika swala la mambo ya kiroho Boss ni mmoja tuu, Mwenye enzi Mungu mkuu

Na yoyote anayetaka kuwa boss katika upande huo atafute sana kuishi maisha bora ya kiroho
Huko sahihi ila pia kuna viongozi wa dini nao ni boss. Ndiyo maana ukishalijua hilo kwamba Mungu ndiye Mkuu. Huwezi kuogopa kutengwa na mwanadamu mwenzako.
 
Binafsi nimemfahamu huyu Padre kwa zaidi ya Miaka 30. Hakika huyu baba alikua mtumishi wa Mungu aliye hai... ni vile kwamba alikua mwanadamu na alipaswa kufa kwa kua alizaliwa na mwanamke. Lakini it's fair to say kwamba hii ilikua ni zawadi bora kabisa kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa uhai wa huyu Padre... Hakika malaika leo wanaimba kwa furaha kumkaribisha mbele ya uso wa Mwenyezi Mungu huyu binadamu aliyejitoa maisha yake kwa ajili ya kuokoa roho za wanadamu...
 
Dah JF ya sasa ina vijana wadogo wengi sana inaonekana, haya majina maarufu wanauliza ni nani?!

Anyway RIP Fr. Nkwera, umeishi maisha yako na yamegusa watu wengi sana, upate pumziko la milele Amen
Huyu ndiye yule ambaye alikuwa na Kanisa la kuvua viatu jirani na Mabibo hostel?
 
Lala salama mtumishi wa Mungu aliye hai.

Nilichojifunza kwako ni kwamba Mungu wetu hawekewi mipaka, yeye humpa karama amtakaye kwa sifa na utukufu wake.

Felician V. M. Nkwera​


Felician Venant Nkwera (alizaliwa Luilo, leo katika Wilaya ya Ludewa, mkoa wa Njombe[1], 28 Aprili 1936 (umri 89)) ni padri aliyetengwa na Kanisa Katoliki [2] na mwandishi nchini Tanzania.
Felician V. M. Nkwera
Amezaliwa28 Aprili 1936 (umri 89)
Lwilo
NchiTanzania
MakaziRiverside, Dar es salaam
Anafahamika kwaPadri Mwasisi wa Kituo Cha Maombezi cha mAma Bikira Maria

Maisha yake​

Wazazi wa Padri Nkwera walikuwa ni Venant Nkwera (baba) na Emmaculata Mhagama (mama).

Alipata upadirisho mwaka 1968 akaanza huduma ya maombezi akiwa bado padri kijana mkoani Tabora na baadaye kuhamia jijini Dar es Salaam. Ni huduma ambayo imemfanya awe kwenye mgogoro mkubwa na jimbo alilokuwa akilihudumia wakati huo; mgogoro huo ukafika makao makuu ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania na baadaye Roma.

Ni huduma ambazo wenye imani wamekuwa wakikiri kwa kinywa na maandishi kwamba wameponywa huku rozari, maji ya baraka na sala vikiwa ndio msingi mkuu wa maombi yaliyopelekea kuponywa huko. Shuhuda za uponywaji wa wagonjwa zinaandikwa ama kusimuliwa na wahusika wenyewe.[3]

Muda mrefu umepita tangu Padri Nkwera asimamishwe kuhudumia Kanisa. Baadhi wanakosoa huduma hizi za maombezi, hasa wakiangazia namna sakata hili lilivyoanza. Baadhi wanaangalia sababu kuu ni ukaidi, huku wakiainisha bayana kwamba Padri Nkwera hakuwa mtii kwa aliyekuwa kiongozi wake kwa wakati huo alipokuwa akilihudumia Jimbo Katoliki la Njombe na zaidi hakutii maamuzi na maelekezo yaliyotolewa na viongozi wake wakubwa yaani maaskofu, Baraza la Maaskofu na hata Kardinali Polycarp Pengo kwa wakati huo.[4]

Kesi mahakamani​

Padri Felician V. Nkwera amekuwa na kesi nyingi mahakamani huku baadhi ya waumini au wafuasi wake pia wakiwa na kesi zenye sura tofautitofauti.

Vitabu na machapisho yake​

  1. Tumbuizo la jioni (1968)[5]
  2. Johari Ndogo (1979)
  3. Sarufi na Fasihi Sekondari na Vyuo (1979)[6]
  4. Kiswahili Sekondari na Vyuo (1979)
  5. Maana na Lengo la Adhabu ya Kifungo (1987)[7]
  6. Tamrin za Fasihi Simulizi, Secondary na Vyuo (1998) [8]

View attachment 3328526


CC Sky Eclat
Mwamba amelala Huduma za Fr Felician Nkwera bado zinaendelea?
Niliwah kumsikia sikia kidgo japokua sikua na taarifa zake nying
 
Nasikia akikutupia Yale MAJI ya BARAKA kama unapepo lazima upagawe.

K
 
Madhehebu mengi hasa haya ya Katoliki, Anglican na Lutheran hayataki wokovu, yaani hayataki maombi, ukifanya maombi yanataka sheria zao kama litrugia, unatengwa na kanisa ukifanya hayo na hii ndio sababu wahubiri wengi wameamua kuacha Madhehebu na kuanzisha makanisa yao...
Dead churches. Wanaamini Mungu hana jipya zaidi ya kutetea na kuhifadhi za zamani
 
Muasisi wa Kituo cha Maombezi cha Mama Bikira Maria (Marian Faith Healing), Padri Felician Nkwera (89) amefariki dunia.

Waamini wamekusanyika katika kituo hicho kilichopo Ubungo Riverside, Dar es Salaam leo Mei 9, 2025 kuomboleza.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa kituoni hapo, Padri Nkwera alifariki dunia jana Alhamisi Mei 8, 2025 usiku.

"Aliaanza kujisikia vibaya jana asubuhi akiwa kanisani, hivyo aliporejeshwa nyumbani kwake, madaktari walipompima walibaini presha yake ipo chini, lakini muda wa jioni hali ilibadilika wakampeleka Hospitali. Hata hivyo ikaonekana presha yake ilikuwa sawa na akaruhusiwa kurudi nyumbani, lakini wakiwa njiani hali yake ikabadilika kisha wakampeleka Hospitali ya TMJ, huko ndipo alifikwa na umauti," kilieleza chanzo cha taarifa.

Padri Nkwera aliwahi kuhudumu Kanisa Katoliki kabla ya kutengwa na uongozi wa kanisa hilo.

Screenshot 2025-05-09 204528.png
 
Huduma yake vs charismatic kuna tofauti gani? Mbona charismatic imeruhusiwa.
Pumzika kwa amani Fr. Nkwera
Charismatic ni moja ya matokeo ya Fr Nkwera. Yeye kama padre alifungiwa ila walipoinuka waumini kanisa liliona kuliko kuwafukuza heri kuwaacha 😁😁😁
 
Back
Top Bottom