TANZIA Lala salama Padre Felician V. M. Nkwera

Nilimpenda kusoma kazi zake. Watu mwengu hasa wanafunzi humfahamu kwa jina la F. Mkwera.

R.I.P Father.
 
Hapana.
Karismatic na huduma ya Fr. Nkwerani vitu tofauti kabisa, ni bangi na polisi. Kimoja (Karismatic) kinahubiri kuokoka, kingine (Fr. Nkwera) kinahubiri ukatoliki uliokolea kwa kumshika zaidi Maria.
Umewahi shiriki vyote ukaona huo utofauti ulioandika hapa?

Sidhani kama umefanyia uchunguzi ulichoandika
 
Si kweli, bali ni chuki ya Askofu Mwanyika kwa kuwa Padre Nkwera alikuwa amenyooka sana kwenye maadili ya useja. Alikuwa ana hoji mwenendo wa mapadri ambao ni ndugu na Askofu Mwanyika walipokuwa wanapinda kimaadili
Asante sana kwa maelezo haya, japo swali bado linakuja ilikuwaje kwa Askofu Mgulunde na hata kwa Kardinali Pengo?

Wote walikua na chuki nae?
 
Sio kweli, ninafahamu mapadre kadhaa wanaofanya maombezi na wala kanisa halijawahi kuwa na shida nao.

Suala la Fr. Nkwera lilikua ni kukiuka kiapo cha utii ambacho alikiapa akipewa daraja la upadri.
Mkwera ndio chanzo cha hiki kiitwacho ulokole wa kikatoliki.
 
Wanajichanganya tu,mbona wameanzisha charismatic pale ubungo na wanachofanya ni hicho walichokuwa wanakipinga...?
Nadhani kipindi hicho ilikuwa ni kabla ya Uamsho. Lakini miaka ya baadaye ndiyo Karismatiki ikakubalika lkn miaka ya nineteenth huko karismatiki ilikuwa inakubaliki kwenye baadhi ya makanisa machache tu. Askofu wa jimbo wa kipindi hicho haikutaka karismatiki kabisa. Kwa sasa karismatiki ipo karibu parokia zote na baba Askofu Ruwaichi anaikubali sana.
 
Nani amewahi enda hapo Emmaus center ubungo anielekeze ?
Emaus centre: Ukifika daraja la kijazi kama unaelekea Mwenge upande wa kulia kuna ile petrol station sasa kwa mbele hatua chache tu utaona kibao na njia inayoelekea Emaus center. Huduma ni kila siku.
Pia kuna Agape center ipo Mbezi Kibanda cha mkaa kuna huduma ya Karismatiki pia.
 
Asante hii ya ubungo ni muda gani kesho niende ili nipate uzoefu wa ratiba zao, naona mbezi mbali kidogo
 
Alikuwa anatumia ekaristi vibaya kwa kuwawekea sehemu za siri wanawake wenye shida ya uzazi
 
Asante sana kwa maelezo haya, japo swali bado linakuja ilikuwaje kwa Askofu Mgulunde na hata kwa Kardinali Pengo?

Wote walikua na chuki nae?
Kumbuka Mgulunde alikuwa ni Askofu wa jimbo la Iringa. Kwa hiyo yeye na Askofu Mwanyika walikuwa "washikaji", hivyo wakati Nkwera anakosana na Askofu Mwanyika asingweza kukaribishwa jimbo la Iringa.

Then Mihayo ndiyo akakubali kumpokea Nkwera na akawa ni Padre mgeni wa Jimbo la Tabora. Akiwa Tabora alikuwa anafanya kazi Serikalini kama Mwl wa Milambo Sekondari, Padri wa Parokia ya Cathedral na Makokola.

Muda wa jioni alikuwa anatembea Kitete hospital na majumbani kuwaombea wagonjwa kwa kutumia maji ya baraka na rosary.

Mwaka 1990 alikuwa ni mwanafunzi wa Post graduate pale UDSM. Mwaka huo ndiyo ule mgomo wa UDSM ulioongozwa na akina Harun Kimaro, Basigiza na James Mbatia ulipomkumba na yeye kwa chuo kufungwa. Hili likitokea huko Tabora pia Askofu Mihayo akafariki na mbadala wake akawa Askofu Mgulunde kutoka Iringa.

As usual hakuweza kukubalika kurudi Tabora kwa Mgulunde, ndipo waumini wake wakiongozwa na Salvatory Mosha (RIP- Ex Tanesco CEO) na mama Maria Nyerere wakamuwezesha Nkwera kujenga kituo cha maombezi (Marian Healing Centre) pale Ubungo Riverside
 
Lala salama mtumishi wa Mungu aliye hai.

Nilichojifunza kwako ni kwamba Mungu wetu hawekewi mipaka, yeye humpa karama amtakaye kwa sifa na utukufu wake.

Felician V. M. Nkwera​

Felician Venant Nkwera (alizaliwa Luilo, leo katika Wilaya ya Ludewa, mkoa wa Njombe[1], 28 Aprili 1936 (umri 89)) ni padri aliyetengwa na Kanisa Katoliki [2] na mwandishi nchini Tanzania.
Felician V. M. Nkwera
Amezaliwa28 Aprili 1936 (umri 89)
Lwilo
NchiTanzania
MakaziRiverside, Dar es salaam
Anafahamika kwaPadri Mwasisi wa Kituo Cha Maombezi cha mAma Bikira Maria

Maisha yake​

Wazazi wa Padri Nkwera walikuwa ni Venant Nkwera (baba) na Emmaculata Mhagama (mama).

Alipata upadirisho mwaka 1968 akaanza huduma ya maombezi akiwa bado padri kijana mkoani Tabora na baadaye kuhamia jijini Dar es Salaam. Ni huduma ambayo imemfanya awe kwenye mgogoro mkubwa na jimbo alilokuwa akilihudumia wakati huo; mgogoro huo ukafika makao makuu ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania na baadaye Roma.

Ni huduma ambazo wenye imani wamekuwa wakikiri kwa kinywa na maandishi kwamba wameponywa huku rozari, maji ya baraka na sala vikiwa ndio msingi mkuu wa maombi yaliyopelekea kuponywa huko. Shuhuda za uponywaji wa wagonjwa zinaandikwa ama kusimuliwa na wahusika wenyewe.[3]

Muda mrefu umepita tangu Padri Nkwera asimamishwe kuhudumia Kanisa. Baadhi wanakosoa huduma hizi za maombezi, hasa wakiangazia namna sakata hili lilivyoanza. Baadhi wanaangalia sababu kuu ni ukaidi, huku wakiainisha bayana kwamba Padri Nkwera hakuwa mtii kwa aliyekuwa kiongozi wake kwa wakati huo alipokuwa akilihudumia Jimbo Katoliki la Njombe na zaidi hakutii maamuzi na maelekezo yaliyotolewa na viongozi wake wakubwa yaani maaskofu, Baraza la Maaskofu na hata Kardinali Polycarp Pengo kwa wakati huo.[4]

Kesi mahakamani​

Padri Felician V. Nkwera amekuwa na kesi nyingi mahakamani huku baadhi ya waumini au wafuasi wake pia wakiwa na kesi zenye sura tofautitofauti.

Vitabu na machapisho yake​

  1. Tumbuizo la jioni (1968)[5]
  2. Johari Ndogo (1979)
  3. Sarufi na Fasihi Sekondari na Vyuo (1979)[6]
  4. Kiswahili Sekondari na Vyuo (1979)
  5. Maana na Lengo la Adhabu ya Kifungo (1987)[7]
  6. Tamrin za Fasihi Simulizi, Secondary na Vyuo (1998) [8]

View attachment 3328526

CC Sky Eclat
Mwamba amelala Huduma za Fr Felician Nkwera bado zinaendelea?

Kupitia fr nkwera mungu aliwai kuniponya ugonjwa ambao ulishindikana katka hospital.

Ilo sitokuja kulisahau katika maisha yangu.

Sehemu pekee ambayo nikipokea ekaristi najiona nina Amani, unapokea kwa kupiga magoti, mdomoni na uku mikono umeikunja.

Fr.Nkwera kupitia ww pia mungu aliniponya ugonjwa ambao ulishindkana hospital.

Tunamshukuru mungu kwa huduma aliyotupa kupitia ww, mungu aiweke roho yako mahali pema peponi
 
Kumbuka Mario Mgulunde alikuwa ni Askofu wa jimbo la Iringa. Kwa hiyo yeye na Askofu Mwanyika walikuwa "washikaji", hivyo wakati Nkwera anakosana na Askofu Mwanyika asingweza kukaribishwa jimbo la Iringa.

Then Mihayo ndiyo akakubali kumpokea Nkwera na akawa ni Padre mgeni wa Jimbo la Tabora. Akiwa Tabora alikuwa anafanya kazi Serikalini kama Mwl wa Milambo Sekondari, Padri wa Parokia ya Cathedral na Makokola.

Muda wa jioni alikuwa anatembea Kitete hospital na majumbani kuwaombea wagonjwa kwa kutumia maji ya baraka na rosary.

Mwaka 1990 alikuwa ni mwanafunzi wa Post graduate pale UDSM. Mwaka huo ndiyo ule mgomo wa UDSM ulioongozwa na akina Harun Kimaro, Basigiza na James Mbatia ulipomkumba na yeye kwa chuo kufungwa. Hili likitokea huko Tabora pia Askofu Mihayo akafariki na mbadala wake akawa Askofu Mgulunde kutoka Iringa.

As usual hakuweza kukubalika kurudi Tabora kwa Mgulunde, ndipo waumini wake wakiongozwa na Salvatory Mosha (RIP- Ex Tanesco CEO) na mama Maria Nyerere wakamuwezesha Nkwera kujenga kituo cha maombezi (Marian Healing Centre) pale Ubungo Riverside
Mkuu upo vzr saaana kuifafanua historia
 
Mkuu upo vzr saaana kuifafanua historia
Mimi najuwa kiini cha mgogoro wa Nkwera dhidi ya Kanisa kwa kiwango cha juu sana.

Pengine Nkwera asingekuja Dar es Salaam huo mgogoro usingetokea. Ngoja nikupe kiini sasa

Hadi 1990 Askofu wa Dar es Salaam alikiwa Laurean Cardinal Rugambwa (RIP), Nkwera alikuwa hana shida na huduma zake japo alikuwa hajapokelewa na jimbo la Dar. Alijulikana kama Padre mtoro. Mwaka huo huo Pengo akawa Askofu Msaidizi (Coadjutor Archbishop) wa Dar es Salaam chini ya ulezi wa Rugambwa.

Ilipofika mwaka 1992 baada ya Polycarp Pengo kutawazwa kama Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar ndipo shida za Fr Felician Nkwera zikaanza.

Nitaendelea......
 
Back
Top Bottom