TANZIA Lala salama Padre Felician V. M. Nkwera

TANZIA Lala salama Padre Felician V. M. Nkwera

Charismatic ni moja ya matokeo ya Fr Nkwera. Yeye kama padre alifungiwa ila walipoinuka waumini kanisa liliona kuliko kuwafukuza heri kuwaacha 😁😁😁
Si kweli. Charismatic haijaanzia Tanzania. Au mnafukiri RC ni kanisa la bongo tu?
 
Upuuzi nimeuandika hapo unaruka kusoma kama mlivyoruka amri ya kupiga marufuku sanamu.
Unaruhusiwa tu kufanya miujiza upate waumini. Waache RC wasiotaka miujiza wala waumini wa kulazimisha
 
Acha mbaambaa ukiulizwa alifanya nini umekaza fuvu alikiuka alikiuka
Au alibaka vitoto maana ndio zao wakatoliki

princess ariana asante kwa lugha nzuri..
Ni kwamba alkiuka mafundisho kwenye msisitizi wa ibada ya bikira maria.
Kwake yeye ibada nzima/yote alidedicate kwa bikira maria ambapo mafundisho ya kanisa hayasemi hivyo.
Maria ktk kanisa katoliki anapewa heshimà yakipekee lakini ktk ibada msisitizo hakukadhiwi moja kwa moja kwake
 
Lala salama mtumishi wa Mungu aliye hai.

Nilichojifunza kwako ni kwamba Mungu wetu hawekewi mipaka, yeye humpa karama amtakaye kwa sifa na utukufu wake.

Felician V. M. Nkwera​


Felician Venant Nkwera (alizaliwa Luilo, leo katika Wilaya ya Ludewa, mkoa wa Njombe[1], 28 Aprili 1936 (umri 89)) ni padri aliyetengwa na Kanisa Katoliki [2] na mwandishi nchini Tanzania.
Felician V. M. Nkwera
Amezaliwa28 Aprili 1936 (umri 89)
Lwilo
NchiTanzania
MakaziRiverside, Dar es salaam
Anafahamika kwaPadri Mwasisi wa Kituo Cha Maombezi cha mAma Bikira Maria

Maisha yake​

Wazazi wa Padri Nkwera walikuwa ni Venant Nkwera (baba) na Emmaculata Mhagama (mama).

Alipata upadirisho mwaka 1968 akaanza huduma ya maombezi akiwa bado padri kijana mkoani Tabora na baadaye kuhamia jijini Dar es Salaam. Ni huduma ambayo imemfanya awe kwenye mgogoro mkubwa na jimbo alilokuwa akilihudumia wakati huo; mgogoro huo ukafika makao makuu ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania na baadaye Roma.

Ni huduma ambazo wenye imani wamekuwa wakikiri kwa kinywa na maandishi kwamba wameponywa huku rozari, maji ya baraka na sala vikiwa ndio msingi mkuu wa maombi yaliyopelekea kuponywa huko. Shuhuda za uponywaji wa wagonjwa zinaandikwa ama kusimuliwa na wahusika wenyewe.[3]

Muda mrefu umepita tangu Padri Nkwera asimamishwe kuhudumia Kanisa. Baadhi wanakosoa huduma hizi za maombezi, hasa wakiangazia namna sakata hili lilivyoanza. Baadhi wanaangalia sababu kuu ni ukaidi, huku wakiainisha bayana kwamba Padri Nkwera hakuwa mtii kwa aliyekuwa kiongozi wake kwa wakati huo alipokuwa akilihudumia Jimbo Katoliki la Njombe na zaidi hakutii maamuzi na maelekezo yaliyotolewa na viongozi wake wakubwa yaani maaskofu, Baraza la Maaskofu na hata Kardinali Polycarp Pengo kwa wakati huo.[4]

Kesi mahakamani​

Padri Felician V. Nkwera amekuwa na kesi nyingi mahakamani huku baadhi ya waumini au wafuasi wake pia wakiwa na kesi zenye sura tofautitofauti.

Vitabu na machapisho yake​

  1. Tumbuizo la jioni (1968)[5]
  2. Johari Ndogo (1979)
  3. Sarufi na Fasihi Sekondari na Vyuo (1979)[6]
  4. Kiswahili Sekondari na Vyuo (1979)
  5. Maana na Lengo la Adhabu ya Kifungo (1987)[7]
  6. Tamrin za Fasihi Simulizi, Secondary na Vyuo (1998) [8]

View attachment 3328526


CC Sky Eclat
Mwamba amelala Huduma za Fr Felician Nkwera bado zinaendelea?
Upumzike kwa Amani Mtumishi Mwaminifu wa Mungu 🙏🙏🙏🙏
 
Charismatic ni moja ya matokeo ya Fr Nkwera. Yeye kama padre alifungiwa ila walipoinuka waumini kanisa liliona kuliko kuwafukuza heri kuwaacha 😁😁😁
Upo sahihi. Kushughulikia ishu za kiroho kunahitajika sana hekima kuliko kutumia mabavu.
 
princess ariana asante kwa lugha nzuri..
Ni kwamba alkiuka mafundisho kwenye msisitizi wa ibada ya bikira maria.
Kwake yeye ibada nzima/yote alidedicate kwa bikira maria ambapo mafundisho ya kanisa hayasemi hivyo.
Maria ktk kanisa katoliki anapewa heshimà yakipekee lakini ktk ibada msisitizo hakukadhiwi moja kwa moja kwake
Anhaa kwahiyo mafundisho yake yame base kwa bikira Maria
 
Sio kweli, ninafahamu mapadre kadhaa wanaofanya maombezi na wala kanisa halijawahi kuwa na shida nao.

Suala la Fr. Nkwera lilikua ni kukiuka kiapo cha utii ambacho alikiapa akipewa daraja la upadri.
Si kweli, bali ni chuki ya Askofu Mwanyika kwa kuwa Padre Nkwera alikuwa amenyooka sana kwenye maadili ya useja. Alikuwa ana hoji mwenendo wa mapadri ambao ni ndugu na Askofu Mwanyika walipokuwa wanapinda kimaadili
 
Madhehebu mengi hasa haya ya Katoliki, Anglican na Lutheran hayataki wokovu, yaani hayataki maombi, ukifanya maombi yanataka sheria zao kama litrugia, unatengwa na kanisa ukifanya hayo na hii ndio sababu wahubiri wengi wameamua kuacha Madhehebu na kuanzisha makanisa yao...
No usiseme hayataki wokovu hakuna Kanisa ktk uliyoyataja hayahubiri ktk wokovu kinachopaswa kuzingatiwa ni kutii.

Hata kama muhusika anaamini alilolivumbua ni jema hupaswa kulifanya ni la Kanisa then zinafuatwa kanuni za kuliingiza ktk Jimbo husika ambapo taratibu hizo hupitia kwa askofu so inawezekana walikinzana hapa mmoja anataka lijulikane ni la Kanisa mwengine anataka ijulikane ni idea yake na makasisi viapo vyao huapa baada ya Mungu wa pili kuwaheshimu ni viongozi walio juu yao so ikitokea ameenda kinyume ndiyo hutengwa japokuwa havuliwi taji ya Upadre.
 
Lala salama fr nkwera,,,

umenikumbusha wamama wa maghorofa ya jeshi na custom pamoja na mwenge kijijini walivyokuwa wakienda kuchongea wenzao waliokuwa wakienda kwa fr nkwera.
Nakumbuka mama mmoja namhifadhi alienda parokia ya Maximilian kolbe mwenge kwenda kutoa taarifa ya kwamba katokewa na bikira maria akiwa anasali rosali paroko wa wakati huo fr Babu alimtimua!!!!!!! Sasa wakati huo fr nkwera alikuwa alienda kusali hapo huku akiwa katengwa na kanisa
Fr nkwera Alimchukua huyo mama na kuwa mmoja wapo ambao waliokuwa Wana maombi na waliifanya hiyo kazi vizuri.
Kilichokuwa kikiniumiza ni wakatoliki wa wakati huo waliipenda huduma yake lakini iliwapasa waende kwa Siri kuogopa kutengwa na kanisa
Na wakati huo wale wanoko walikuwa wanakagua wakati wa kwenda kupokea ekaristi takatifu kuhakikisha wafuasi wa fr nkwera hawapokei ekaristi takatifu.

Halafu yote yamepita kama upepo....RIEP Fr. Nkwera
 
Huyu bila shaka ndiye alianzisha Karismatiki, au siyo mkuu??
Hapana.
Karismatiki na huduma ya Fr. Nkwera ni vitu vwili tofauti, ni kama mbingu na ardhi.
Watu wengi hawajui na hawakujua nini alikuwa anafanya Fr. Nkwera.

Kwa kifupi sana, Fr. Nkwera alianzisha huduma ya maombezi ya kikatoliki kwa misingi ya Bikira Maria huku akidai Bikira Maria alimtokea, alikuwa akimtokea na alikuwa akimpa ujumbe mahususi, jambo ambalo kanisa katoliki waliona ni usanii. Kiujumla huduma yake ilikuwa ni ukatoliki uliopitiliza huku Maria akitumika kama ngao yake.
 
Charismatic ni moja ya matokeo ya Fr Nkwera. Yeye kama padre alifungiwa ila walipoinuka waumini kanisa liliona kuliko kuwafukuza heri kuwaacha 😁😁😁
Hapana.
Karismatic na huduma ya Fr. Nkwerani vitu tofauti kabisa, ni bangi na polisi. Kimoja (Karismatic) kinahubiri kuokoka, kingine (Fr. Nkwera) kinahubiri ukatoliki uliokolea kwa kumshika zaidi Maria.
 
Back
Top Bottom