TANZIA Lala salama Padre Felician V. M. Nkwera

Wanajichanganya tu,mbona wameanzisha charismatic pale ubungo na wanachofanya ni hicho walichokuwa wanakipinga...?
 
R.I.F....Mungu ailaze mahali pema peponi Roho yako
 
Huyu ndiye yule alipata misukosuko kwa kusali kama walokole na pia aliandika kitabu kilichotumika mashuleni miaka ya 1980s?
Wala sio kwa kusali kama walokole. Kwani walokole wanasali rozali? Sehemu kubwa ya huduma yake ni Mama Maria, hata kituo chake alikiita Marian. Je, walokole wana maombezi ya kumuomba Mama Maria awaombee?
 
Kw Lutheran, naweza sema labda baadhi ya Dayosisi zinaweza kuwa na utaratibu huo.
Kuna mwinjilisti mmoja namfahamu alikuwa anatupigisha sana maombi, na mahubiri yake yalikuwa yanavutia sana full hamasa. Kuanzia morning glory, ibada za katikati ya wiki, semina na jumapili. Mpaka nilipokuja kuhama huko, sijawahi kuskia kuwa amekatazwa kuendesha maombezi.
 
Duuuuh hii dunia imejaa unafiki
 
Never outshine your boss.
 
Ujio wa makanisa ya walokole yamefuta ujinga mwingi sana. Yaani makanisa yalijifanya kama enzi za CCM chama kimoja.
 
Ni kweli RC hawataki maombi? Vitu vingine msiishi kwa kusimuliana
 
Huduma yake vs charismatic kuna tofauti gani? Mbona charismatic imeruhusiwa.
Pumzika kwa amani Fr. Nkwera
 
Ujio wa makanisa ya walokole yamefuta ujinga mwingi sana. Yaani makanisa yalijifanya kama enzi za CCM chama kimoja.
Bahati mbaya ni kinyume chake, ujio huo ndio umesababisha upuuzi mwingi, mara mchungaji anapaa, mara kule anawabarikia nguo za ndani ili wazae. Huwezi kukuta ujinga huo Roman Catholic
 
Huduma yake vs charismatic kuna tofauti gani? Mbona charismatic imeruhusiwa.
Pumzika kwa amani Fr. Nkwera
Alitengwa kwa ajili ya kutokuwa mtii kwa Askofu. RC padri wa Jimbo hajipangii majukumu, anapangiwa na Askofu wake.
Karismatiki sio huduma, ni chama cha kitume kama ilivyo Moyo Mtakatifu wa Yesu, Wanaume Wakatoliki UWAKA, Wanawake WAWATA, na Vijana VIWAWA.
 
Bahati mbaya ni kinyume chake, ujio huo ndio umesababisha upuuzi mwingi, mara mchungaji anapaa, mara kule anawabarikia nguo za ndani ili wazae. Huwezi kukuta ujinga huo Roman Catholic
Hayo maigizo siyo lazima yafanywe na walokole, yanafanywa na wanaoigiza ulokole.
Hata kubeba sanamu na kuanza kulitembeza pia walokole wanaona ni upuuzi
 
Kwanini alitengwa??
Katoliki wana taratibu zao.Jamaa wakati Pengo bishop wa Dar es salaam.wwalikuwa wanakingiana kifua(Nkwera akiambiwa afuate kanisa livyotaka-alikuwa anambishia (walisomaga wote seminary)- ila jamaa was talented..akiwa anaenda soma Masters pale UDSM alikuta one of his Book ni part ya syllabus ya Degree yake! 😃😄jamaa kwao wote ni vichwa. Kuna mdogo ake pia alikuwaga pale DIT alikuwa academically yupo vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…