TANZIA Lala salama Padre Felician V. M. Nkwera

Unaweza kuwa mtii kwa watu na mifumo ya dunia lakini ukawa muasi kwa Mungu

Father Nkwera alishika neno kwa jinsi alivyopokea kwa Mungu wake

Mathayo 10:37-39​

Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili;
wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.
Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili.
Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona.
 
Katika swala la mambo ya kiroho Boss ni mmoja tuu, Mwenye enzi Mungu mkuu

Na yoyote anayetaka kuwa boss katika upande huo atafute sana kuishi maisha bora ya kiroho
Huko sahihi ila pia kuna viongozi wa dini nao ni boss. Ndiyo maana ukishalijua hilo kwamba Mungu ndiye Mkuu. Huwezi kuogopa kutengwa na mwanadamu mwenzako.
 
Binafsi nimemfahamu huyu Padre kwa zaidi ya Miaka 30. Hakika huyu baba alikua mtumishi wa Mungu aliye hai... ni vile kwamba alikua mwanadamu na alipaswa kufa kwa kua alizaliwa na mwanamke. Lakini it's fair to say kwamba hii ilikua ni zawadi bora kabisa kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa uhai wa huyu Padre... Hakika malaika leo wanaimba kwa furaha kumkaribisha mbele ya uso wa Mwenyezi Mungu huyu binadamu aliyejitoa maisha yake kwa ajili ya kuokoa roho za wanadamu...
 
Dah JF ya sasa ina vijana wadogo wengi sana inaonekana, haya majina maarufu wanauliza ni nani?!

Anyway RIP Fr. Nkwera, umeishi maisha yako na yamegusa watu wengi sana, upate pumziko la milele Amen
Huyu ndiye yule ambaye alikuwa na Kanisa la kuvua viatu jirani na Mabibo hostel?
 
Niliwah kumsikia sikia kidgo japokua sikua na taarifa zake nying
 
Nasikia akikutupia Yale MAJI ya BARAKA kama unapepo lazima upagawe.

K
 
Dead churches. Wanaamini Mungu hana jipya zaidi ya kutetea na kuhifadhi za zamani
 
Muasisi wa Kituo cha Maombezi cha Mama Bikira Maria (Marian Faith Healing), Padri Felician Nkwera (89) amefariki dunia.

Waamini wamekusanyika katika kituo hicho kilichopo Ubungo Riverside, Dar es Salaam leo Mei 9, 2025 kuomboleza.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa kituoni hapo, Padri Nkwera alifariki dunia jana Alhamisi Mei 8, 2025 usiku.

"Aliaanza kujisikia vibaya jana asubuhi akiwa kanisani, hivyo aliporejeshwa nyumbani kwake, madaktari walipompima walibaini presha yake ipo chini, lakini muda wa jioni hali ilibadilika wakampeleka Hospitali. Hata hivyo ikaonekana presha yake ilikuwa sawa na akaruhusiwa kurudi nyumbani, lakini wakiwa njiani hali yake ikabadilika kisha wakampeleka Hospitali ya TMJ, huko ndipo alifikwa na umauti," kilieleza chanzo cha taarifa.

Padri Nkwera aliwahi kuhudumu Kanisa Katoliki kabla ya kutengwa na uongozi wa kanisa hilo.

 
Huduma yake vs charismatic kuna tofauti gani? Mbona charismatic imeruhusiwa.
Pumzika kwa amani Fr. Nkwera
Charismatic ni moja ya matokeo ya Fr Nkwera. Yeye kama padre alifungiwa ila walipoinuka waumini kanisa liliona kuliko kuwafukuza heri kuwaacha 😁😁😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…