Lamine Yamal avunja ukimya kuhusu kauli za kibaguzi na kejeli dhidi ya Uislamu

adriz

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2017
Posts
17,595
Reaction score
39,893
Moja kwa moja .

Katika mechi ya kimataifa ya Kirafiki wiki hii kati ya timu ya taifa ya Uhispania (Spain) dhidi ya Misri (Egypt) kundi mashabiki wa Spain walisikika wakiimba na kuruka "Asiyeruka ni Muislamu (kama hauruki ni Muislamu" wakati pambano likiendelea .

Baada ya mchezo huo video hiyo ya mashabiki wa Spain ilikuwa ikienea kwa kwa Kasi sana mitandaoni . Baada ya tukio hilo mchezaji tegemezi wa timu ya Spain kinda Lamin Yamal ambaye ni Muislamu amekemea vikali tukio hilo kwa kuandika kama ifuatavyo katika akaunti yake ya Instagram ;

Mimi ni Muislamu, alhamdulillah.

Jana uwanjani kishindo cha maneno "asiyeruka ni Muislamu" kilisikika. Najua nilikuwa nikiichezea timu pinzani na halikuwa jambo la kibinafsi dhidi yangu, lakini kama Muislamu, bado ni jambo la utovu wa heshima na lisilostahimilika.

Naelewa kuwa si mashabiki wote wako hivi, lakini kwa wale wanaoimba mambo haya: kutumia dini kama dhihaka uwanjani kunawafanya muonekane kama watu wajinga na wabaguzi wa rangi. Mpira wa miguu ni wa kufurahia na kuhimizwa, si kwa ajili ya kuwakosea heshima watu kwa sababu ya uasili wao au kile wanachoamini.
Baada ya kusema hayo, asanteni kwa watu waliokuja kutushangilia, tukutane kwenye Kombe la Dunia. 🤍

IMG_20260401_225728.jpg

#UziTayari
 
Nakumbuka kauli ya mwanahabari maarufu na gwiji Marekani katika podcast alisema.

" Miaka ya nyuma kulikuwa na tatizo kubwa la Uislamu wa itikadi Kali lakini sasa Waislamu wengi wapo kawaida na itikadi Kali zimepungua ndio maana unakuta Qatar , UAE nk ni Waislamu lakini hakuna itikadi Kali , lakini sasa itikadi Kali zimerudi kwetu kwa Wakristo na Wayahudi kwa Kasi sana na nchi nyingi unakutana na Wakristo Wenye itikadi Kali wasiovumilia dini nyingine"
 
Uislamu utapambana sana na upinzani wa Wagalatia wahafidhina Ulaya enzi hizi na miaka mingi ijayo.
Wakristo wahafidhina wanakuja kwa Kasi sana .

Marekani Ramadhani hiii walikuwa wanawafanyia Fujo Waislamu wakiswali times square , uingereza kulifanyika ati_muslim protest , Trump alileta kauli za kibaguzi baada ya London kuchaguliwa mayor Muislamu .
 
Kuna ubaguzi gani hapo? Hao wasioruka basi ni waislam, wabaki na uislam wao haidhuru
Ukiangalia kwa juu unaona kama haina madhara sawa na Mimi Leo niseme kukuita mkiristo "Kafiri" Kuna madhara gani ? na ukiangalia maana ya Kafiri ni "disbeliever" yaana mtu ambaye haamini katika Uislamu.

Lakini katika muktadha wa lugha na jamii neno "Kafiri" linachukuliwa kama offensive word neno la uchokozi ndio maana Mimi siwezi kumuita rafiki yangu au jirani yangu mkiristo Kafiri japo kiuhalisia yeye ni Kafiri na kumuita Kafiri(asiye amini Uislamu ) ni sawa na kumuita mkiristo sababu wote hawaamini Uislamu .

Tukija kwenye hiyo nyimbo inajulikana kama anti_muslim chant , mfano wake Leo mtu aseme asiye simama "Mwanamke" hapo umeiweka sifa ya Uwanamke kama kitu cha kuzarauliwa na cha hovyo na kutaka wote wasimame kwa nguvu
 
Wakristo wahafidhina wanakuja kwa Kasi sana .

Marekani Ramadhani hiii walikuwa wanawafanyia Fujo Waislamu wakiswali times square , uingereza kulifanyika ati_muslim protest , Trump alileta kauli za kibaguzi baada ya London kuchaguliwa mayor Muislamu .
Tatizo Wahamiaji Waislamu wanataka wadumishe tamaduni zao za Kiislamu katika Ulimwengu wa magharibi, hapo lazima watatifuana tu na wenyeji, Wazungu wengi huko hawajawahi kuona watu wanafunga barabara kuswali au wanawake wanajifunika gubigubi kwa hiyo wanachanganyikiwa wanaona kama ni uvamizi wa kitamaduni.

Hata leo kukitokea wimbi kubwa kwa wahamiaji wa Kikristo Saudia halafu wanawake wengi wahamiaji mtaani wawe hawavai Kiislamu, wahamiaji wawe wanajiachia kunywa pombe, kula kitimoto, kujenga makanisa n.k italeta shida.
 
Moja kwa moja .

Katika mechi ya kimataifa ya Kirafiki wiki hii kati ya timu ya taifa ya Uhispania (Spain) dhidi ya Misri (Egypt) kundi mashabiki wa Spain walisikika wakiimba na kuruka "Asiyeruka ni Muislamu (kama hauruki ni Muislamu" wakati pambano likiendelea .

Baada ya mchezo huo video hiyo ya mashabiki wa Spain ilikuwa ikienea kwa kwa Kasi sana mitandaoni . Baada ya tukio hilo mchezaji tegemezi wa timu ya Spain kinda Lamin Yamal ambaye ni Muislamu amekemea vikali tukio hilo kwa kuandika kama ifuatavyo katika akaunti yake ya Instagram ;

Mimi ni Muislamu, alhamdulillah.

Jana uwanjani kishindo cha maneno "asiyeruka ni Muislamu" kilisikika. Najua nilikuwa nikiichezea timu pinzani na halikuwa jambo la kibinafsi dhidi yangu, lakini kama Muislamu, bado ni jambo la utovu wa heshima na lisilostahimilika.

Naelewa kuwa si mashabiki wote wako hivi, lakini kwa wale wanaoimba mambo haya: kutumia dini kama dhihaka uwanjani kunawafanya muonekane kama watu wajinga na wabaguzi wa rangi. Mpira wa miguu ni wa kufurahia na kuhimizwa, si kwa ajili ya kuwakosea heshima watu kwa sababu ya uasili wao au kile wanachoamini.
Baada ya kusema hayo, asanteni kwa watu waliokuja kutushangilia, tukutane kwenye Kombe la Dunia. 🤍

View attachment 3565959

#UziTayari
Tunawapenda sana Lamine Yamal pamoja na Mo Salah. Mungu awajalie hawa wawili Ballon d'Or, ntafurahi sana.
 
Ukiangalia kwa juu unaona kama haina madhara sawa na Mimi Leo niseme kukuita mkiristo "Kafiri" Kuna madhara gani ? na ukiangalia maana ya Kafiri ni "disbeliever" yaana mtu ambaye haamini katika Uislamu.

Lakini katika muktadha wa lugha na jamii neno "Kafiri" linachukuliwa kama offensive word neno la uchokozi ndio maana Mimi siwezi kumuita rafiki yangu au jirani yangu mkiristo Kafiri japo kiuhalisia yeye ni Kafiri na kumuita Kafiri(asiye amini Uislamu ) ni sawa na kumuita mkiristo sababu wote hawaamini Uislamu .

Tukija kwenye hiyo nyimbo inajulikana kama anti_muslim chant , mfano wake Leo mtu aseme asiye simama "Mwanamke" hapo umeiweka sifa ya Uwanamke kama kitu cha kuzarauliwa na cha hovyo na kutaka wote wasimame kwa nguvu
Kwenye mikutano ya wanasiasa nao husema piga makofi, asiyepiga makofi ni mchawi
 
Wakristo wahafidhina wanakuja kwa Kasi sana .

Marekani Ramadhani hiii walikuwa wanawafanyia Fujo Waislamu wakiswali times square , uingereza kulifanyika ati_muslim protest , Trump alileta kauli za kibaguzi baada ya London kuchaguliwa mayor Muislamu .
Wamewavumilieni wamechoka. Kwa miaka mingi Waislamu wamekaribishwa ulaya na wakaanza kuwasumbua wenyeji wao wakilazimisha itikadi yao ndio iwe.
 
Back
Top Bottom