LAPTOP inaharibika muda gani usipoizima bali inapiga mzigo

LAPTOP inaharibika muda gani usipoizima bali inapiga mzigo

wakurochi

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2017
Posts
2,647
Reaction score
2,951
Poleni wandugu kwanza.

Ni kwamba kuna kazi nafanya na laptop yangu ya siku nyingi Acer Quad Core 8gb ram.

Sasa shughuli nyingine masaa 18 inachapa mzigo nazima nusu saa. Halafu inapiga masaa 6 huu mchezo wiki nzima nimekuwa nafanya usiku na mchana sasa nimeanza kuogopa nitaikuta imezima moja kwa moja.

Ingawa chini yake nimeunganisha kwa usb "kipozeo" notebook cooler" kina fan lakini nimeona niongee na watalaam mnipe ujuzi.
 
Kama haipati Joto sana we Piga mzigo tu mkuu, mi yangu inakaa miezi haizimwi.

Computer hazijatengenezwa zizimwe, ni vifaa vya kazi hivi.

Hapa unaandika jf Masaa 24 ipo online, ujue somewhere kuna computer zinapiga mzigo hazizimwi.
 
Huwa nazima laptop pale tu inapobidi nifanye hivyo kama kuinstall new updates. Other than that naweza kaa miezi bila kuizima.

Laptop haifi kwa kuzima au kutokuizima.

Ukiona unawaza laptop itakufa kwa sababu hiyo jua huna hela teh teh
 
Unaiweka sehemu yenye upepo wa kutosha, ama eneo ambapo Joto linaondoka kirahisi. Mfano laptop ambayo ipo juu ya Godoro ni rahisi kupata Joto la haraka kuliko ambayo ipo juu ya tiles.
Mkuu ikikaa kuanzia miezi mitatu bila kuwashwa kuna madhara yanaweza tokea ??
 
Mkuu ikikaa kuanzia miezi mitatu bila kuwashwa kuna madhara yanaweza tokea ??
Kama Una plan kutotumia kifaa chochote kile chenye battery kwa muda mrefu kicharge nusu, hata vifaa vipya kama simu ama laptop vikija kwetu vimekaa miezi kwenye shelf za maduka tunavikuta na charge nusu

Zima ama toa battery.

Battery ni kitu kimoja kiharibifu sana, ukiacha battery bila charge kwa muda mrefu inaweza kudischarge siku unataka kutumia ikawa kama imekufa isiwake hadi uitoe.

Pia ukiacha battery ina charge 100 kwa muda mrefu battery inaweza kuoza na kuanza kutoa maji, kwa battery za alkaline kama za remote zinatabia ya kutoa hayo maji, na battery za lithium kama za simu zile zina tabia ya kuhifadhi gas ndani (kibongo bongo tunasema imevimba) zote mbili hizi ni hatari.
 
Shukrani mkuu kwa maelezo mazuri.
 
Mi nauliza matumizi mazuri ya betri ya laptop. Je, inabidi nitoe chaja ikijaa wakati naendelea na kazi au iendee kukaa kwenye chaja? Chief-Mkwawa
 
Mi nauliza matumizi mazuri ya betri ya laptop. Je, inabidi nitoe chaja ikijaa wakati naendelea na kazi au iendee kukaa kwenye chaja? Chief-Mkwawa
Iache, laptop za kisasa battery likijaa zinachukua umeme moja kwa moja kwenye adapter na sio battery hivyo battery lako linakuwa haitumiki.
 
Asante Chief-Mkwawa, maana nimewahi kusikia betri ikijaa chomoa, then ikifika asilimia fulani mfano 15 weka chaja.
Battery inakufa ikichaji na kudischarge zile seli zake zinapungua uwezo wa kubeba chaji mpaka inakufa.

Njia nyengine ya kuitunza kama unataka uchomoe waya ni kuitoiacha ikaisha ama ikabaki na chaji kidogo subiri around 50% ama 40% chomeka waya mpaka 80% ama 90% hivi then Fuata hio circle.
 
Mimi binafsi yangu kuizima ni bahati mbaya, either umeme umekatika na charge imeisha, au ina install updates so inaji restart automatically, otherwise naweza kaa hata 3months au zaidi nisiizime, yani in short sikumbuki ni lini mara ya mwisho nilizima laptop yangu. Maana im a graphic designer so napiga mzigo 24/7, mahali popote nilipoishia nikipata mzuka tu nafungua laptop naendelea kuchapa kazi, hata nikiwa bar, so sioni umuhimu wa kuzima.
 
Katika kutumia Lenovo ideapad 130 usiku ilitoa pop up ya update. Nika kubali ila ilichukua muda kidogo kumaliza hiyo download isivyo kawaida kwa updates nyengine.
Sasa baada ya ku update nikitaka kuweka password nifungue, mara keyboard hazifanyi kazi - kwa maana na type hewa!
Nimejaribu option ya ku reboot/safe mode nimefeli - no response.
Next step kwenye troubleshoot wanasema nitoe betri na kuirudisha. Betri imefungiwa ndani sina device ya kufungua vi-screw.
Je, hili tatizo limetokana na nini?
Muarobaini ni kwenda kwa fundi atoe betri na kuirudisha au kuna solution nyingine?
Msaada.
Chief-Mkwawa
 
Back
Top Bottom