A
Anonymous
Guest
Hello habari!
Changamoto yangu naielekeza hasa kwa mabasi ya mikoani yatokayo Mkoa wa Kagera - Karagwe kwenda DSM au mikoa mingine wamezidi kujipangia nauli kipindi hiki mpaka kutoza nauli ya Sh 150,000 - 200,000.
Wahusika hao wanaokatisha tiketi mkononi kwa maana ya ‘physically’ ukijaribu kuwaomba tiketi za elektroniki wanakujibu ovyo na hata kama umekata tiketi muda mrefu wanakurudishia hela kisa umeomba tiketi za elektroniki.
Mfano kuna wengine ukiomba wanakupa tiketi ya kuandika kwa mkono kwa madai kuwa utapatiwa ya elektroniki ukifika kwenye basi kwa madai mtandao unasumbua, lakini hiyo baadaye utaisikia kwenye bomba, hautaipata.
Mfano, kuna hii Kampuni ya Frester na Wahudumu wake ipo siku watashughulikiwa wanachokifanya kwa wateja wao, sijui wanahisi kila mtu hana akili timamu au hana-exposure! Wanawatreat wateja wanavyojisikia.
Mimi pia ni mhanga waweza kuta kwenye basi moja abiria mna nauli zinatofautiana huyu kakata tiketi ya Sh 100,000, mwingine Sh 90,000 n.k
Naomba Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) Iiingilie kati suala hili pesa ni ngumu wakati huu.
Gari hilo juzi wahusika wame-cancel safari yangu ya dharura na kurudisha nauli wakati nilikata zamani kisa tu nimewadai tiketi ya electronic na zilikuwa zinahitajika kazini🙌
Aisee hili ni onyo wahusika zipo namba zao ipo siku watawajibishwa
Ahsante.