LATRA kampuni ya mabasi ya BM inastahihli kufungiwa kwa utapeli

LATRA kampuni ya mabasi ya BM inastahihli kufungiwa kwa utapeli

Tanzania tabia za kihuni haziwezi kuisha, bora waige ile shule ya KAIZIREGE NA KEMEBOS ya Bukoba wana mabasi yao special kama 50 hivi kwa ajili ya kusafirisha wanafunzi wao mikoani, Anuarite ni shule kubwa ilipaswa wawe na mabasi yao wenyewe kuepuka karaha hizo.
Wewe unasifia shule kuwa na mabasi kwa ajili ya kubeba wanafunzi wakati wa likizo likizo zenyewe 2 kwa mwaka huo muda mwingine mabas yote hayo yanafanya kazi gani..?
Si mabus yote kuna uhuni, inategemea na wewe unataka nini wakat wa kusafiri..
 
Kama huwa hausafiri huwezi kujuwa class za mabasi.

Luxury haliwezi kufanana na min luxury au ordinary kwa lolote.

Mimi nikisafiri lazima nipande hasa zile 2 by one.

Anayesafiri kwa luxury zile seat hazibananishwi ni zilezile kutoka kiwandani unaweza kunyoosha miguu ukafika safari yako miguu haijavimba wakati hizi za kawaida wanang'owa viti nakuongeza viti huwezi kunyoosha miguu.
Ukiwa kwenye luxury unaweza kusafiri umenyoosha miguu? Hiyo luxury inaenda mkoa gani?
 
Binafsi huwa sioni tofauti yoyote ya maana kwenye hayo mabasi ya mikoani, kati ya luxury na kawaida, labda tofauti iliyopo ni hayo majina mawili tu.

Umetumia kigezo gani kuita hilo bus luxury? ukubwa wa nauli au kuna kingine?
Ukubwa wa nauli na choo, upuuzi mtupu, mtu na akili zako timamu unakaa kwenye bus la 2x2 kama sisi matolu tunabana miguu alafu unaita laxury, kelele mtindo mmoja. Wanawadanganya wajinga kama hawa na kuwapiga hela ndefu
 
Kama utakuwa mwl acha umbea baada ya kupigwa changa

Kama mzazi ,jitahidi sana kujua mchezo ,mwl aliyeratibu safari hizo ndo mwizi nambamoja ,mdili naye
 
Mkuu acha hizo ,mmepangiwa basi saa kumi na mbili unapofika kituoni unakuta umepanhiwa basi tofauti na ulilokuwa umestahili
Siku nyingine uliza wakupe simu za LATRA kabla hujapanda bus au kurudi nyumbani na badae kulalamika Jf..
 
ungewasiliana na walimu kwanza isije kua unawaharibia mchongo hapa
 
Ukiwa kwenye luxury unaweza kusafiri umenyoosha miguu? Hiyo luxury inaenda mkoa gani?
Wewe endelea kupanda Saibaba tu.

FB_IMG_1719736230091.jpg
bus.jpg
 
Wanafunzi wa shule ya anwarite ambao walikuwa wanatakiwa kusafiri leo kwa mabasi aina ya luxury wametapeliwa kwa kulazimishwa kusafiri kwa kutumia mabasi ya daraja la kawaida.
Hakuna mabasi ya luxury Tanzania
 
Hivi hili nalo mnawasubili Latra?

Kama umekata luxury umapandishwa gari ya kawaida waambie wakurudishie pesa iliyozidi.

Bus kabla halijatoka traffic lazima walikaguwe mmewaeleza traffic? Isitoshe namba za Latra pia zipo.

Wabongo tunapenda kulalamika kwa vitu ambavyo viko ndani ya uwezo wetu na tunaweza kuvikomesha.

Mimi sichezewi na watu wa mabasi hata siku moja nimeshawachomesha wakapigwa faini vwawa kwa kupakiza abiria na kuwakalisha chini kwenye vindoo vya lita 10 kwa safari ndefu ya Tunduma Dar, abiria wote waliozidi walishushwa na bus likalimwa faini.
Wewe hata hatukushangai unavyopenda utata, si hata humu mara kwa mara unagombana na watu kwa sababu za kijinga.

Huko kwenye jamii yako itakuwa unagombana sana na watu.
 
JF Ni Chombo Nyeti Sana Weka Ushahidi Wa Tickets Ili Tuone
JF Siku Hizi Imejipambanua Vizuri Sana Kwa Tuhuma Zako
Wanaweza Kutaka Kupata Ufafanuzi Kutoka Kwa Hawa Watu
1 .LATRA
2. BM
3. SHULE
 
Tunaomba mamlaka ya usafiri LATRA iifunge kampuni ya mabasi ya BM yandayo Dar -Kilimanjaro/Arusha kutokana na udangajifu kwenye nauli.
Wanafunzi wa shule ya anwarite ambao walikuwa wanatakiwa kusafiri leo kwa mabasi aina ya luxury wametapeliwa kwa kulazimishwa kusafiri kwa kutumia mabasi ya daraja la kawaida.
Tunaombeni mamlaka ichukue hatua mara moja kwani huu ni utapeli wa kupindukia na utakuwa na madhara yafutayo:
1: Serikali itakuwa imekosa mapato kwa maana gharama itakuyokuwa kwenye tiketi sio gharama ililipwa na mtoa nauli.
2: Kampuni ya BM inashindwa kutumiza vigezo vilivyowekwa na LATRA
Mimi na abiria wenzangu ni mhanga wa hilo, wiki tatu zilizopita, ilikuwa safari ya kutoka Dodoma kwenda Dar, ilitakiwa tupande bus la BM luxury ambalo tulikatia tiketi, likaletwa basi la kawaida ambalo halina hata choo ndani.

Abiria walitaka kushuka kwenye basi baada ya kuona basi hilo halina choo na baadhi ya viti vimeharibika na baadhi vimeloa na maji. Kwa hasira kila abiria aliamua kukaa kwenye siti yoyote ambayo aliona inamfaa. Balaa ilikuwa kwa abiria waliopandia njiani, hao ndo waliomgombeza sana konda baada ya kuona siti zao zimekaliwa na abiria wengine na hakuna aliyekubali kunyanyuka kwenye siti.

Baadhi ya abiria walidai kurudishiwa kiasi cha nauli sababu basi walilopandishwa sio luxury kama ilivyotegemewa. Kwa Kulipoza hilo ilibidi konda awasiliane na bosi wake ili kila abiria arudishiwe shilingi elfu tano. Na baada ya muda kidogo konda alianza kupita kwa kila abiria akimrudishia shilingi elfu tano. baada ya hapo kelele na ugomvi kwenye basi vikaisha , na safari ikaenda vizuri na kufika kwa muda muafaka.
 
Back
Top Bottom