Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imewataka Waendeshaji wa mabasi Jijini Dar es salaam kuzingatia utaratibu wa kupakia na kushusha abiria katika vituo vilivyopangwa na Halmashauri.
Kwa mujibu wa LATRA, mabasi yanayotoka Mikoa ya Kaskazini na maeneo mengine yanatakiwa kutumia Kituo cha Mabasi cha Magufuli, huku yanayotoka Mikoa ya Kusini yakitakiwa kutumia Kituo cha Mabasi cha Mbagala.
Meneja wa LATRA Mkoa wa Dar es Salaam, Ngereza Patel amesema agizo hilo linafuatia maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ya kutaka mabasi yote kurejea katika Vituo vilivyopangwa na kuzingatia masharti waliyopewa wakati wa kupata leseni za usafirishaji.
Patel amesema kwenda kinyume na utaratibu huo ni kuvunja Sheria na masharti ya leseni, hivyo amewataka Wamiliki na Waendeshaji wa mabasi kuzingatia Vituo vilivyotengwa kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria ili kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria.
Soma pia Wamiliki wa mabasi wapewa wiki moja kurejea stendi ya Magufuli