LATRA: Mabasi yote yaishie Stendi ya Magufuli na Mbagala

LATRA: Mabasi yote yaishie Stendi ya Magufuli na Mbagala

Acha mazoea
Mbona uzungumzii stand ilipokuwa mnazi mmoja.

Shida ni umbali
Shida ya usafiri
Ongezeko la gharama

Jiji limekuwa na kutanuka vibaya mno
Wakati wa Ubungo, Chamazi palikuwa shamba, Leo hii?

Zinahitajika stand zaidi ya nne ndani ya jiji la Dar es salaam.

Na sio Kila wilaya Bali ni Kila jimbo

Kama unakaa kigamboni, na umefika stend ya magufuli saa sita usiku, means itabidi ulale hotelini uwez kufika kigamboni kwa mtu mwenye maisha ya kawaida

1. Saa sita hakuna mwendokasi

2. Saa sita hakuna kivuko chochote kigamboni

3. Saa sita hakuna daladala inayokwenda kigamboni

Means upande taxi, ambayo possibly kutoka Magufuli stend mpaka kigamboni inaweza kuwa ni laki moja

Miundombinu yetu mkoa wa dar es salaam bado sanaaaa kuweza kuhande hii mambo
 
Ufafanuzi wa Mgawanyo wa VituoMikoa ya Kaskazini na kwingineko:

Mabasi yote yanatakiwa kutumia Kituo cha Mabasi cha Magufuli (Mbezi).

Mikoa ya Kusini:.
Mabasi yote yanatakiwa kuishia na kuondokea katika Kituo cha Mabasi cha Mbagala.

Sababu na Maelekezo ya Agizo Hilo

Kuzuia mofisi ya mjini:
Amri hii inazuia kampuni za mabasi kuendesha stendi binafsi katikati ya mji.

Usafiri wa ndani:
Abiria watakaoshushwa Stendi ya Magufuli wataendelea na safari zao kwa mwendokasi, daladala, au 'shuttle' za kampuni husika.

Hatua za kisheria:
LATRA imesisitiza kuwa kukiuka utaratibu huu ni kuvunja masharti ya leseni na hatua kali zitachukuliwa kwa wamiliki watakaogoma.
 
Viongozi wanapaswa kujua kwamba Dar ni mkoa na si wilaya.

Kila wilaya Dar inapaswa kuwa na stand kubwa tu.

Temeke iwe na stand
Kigamboni iwe na stand
Kinondoni iwe na Stand
Ila pia
Yes
1. Kigamboni
2. Temeke
3. Mwenge
4. Mnazi mmoja
5. Mbagala
6. Mbezi
 
Back
Top Bottom