Andromeda Galaxy
JF-Expert Member
- Feb 7, 2025
- 9,846
- 16,713
Ila Kuna kampuni sita special case ni zipi hizo?
Point!👍👍👍👍Mikoani kila wilaya na miji ina stand yake. Hakunaga stand ya mkoa. Kwa nini wilaya za Dar Es Salaam hazina stand zao?
kamdinyo ukifika morogoro ni DMMimi jumanne nakwenda Morogoro kwa kutumia Abood bus , nakwenda shekilago na nina hakika nitapata basi pale pale kwa siku zote.
We kama siyo mwana "kijani" basi utakuwa mchawi.Kipindi mabasi yapo ubungo mbona mlikuwa hamlalamiki yaje.huko kigamboni
Tuache uvivuKwa sababu Ubungo na karibu zaidi kuliko Mbezi.
Shida ni kwamba sijui.waafrika huwa tunawaza nini.Population inaongezeka
huduma zinatakiwa ziwe karibu na watu na sio mbali na watu.....
Hivi kuna miundo mbinu ya kupela Abiria wenye mizigo na shangazi kaja, asubuhi na jioni huko magufuli?
Kelele tu hizi, tafuteni sababu kwa nini abilia hawapendi kupandia Maghufuri,Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imewataka Waendeshaji wa mabasi Jijini Dar es salaam kuzingatia utaratibu wa kupakia na kushusha abiria katika vituo vilivyopangwa na Halmashauri.
Kwa mujibu wa LATRA, mabasi yanayotoka Mikoa ya Kaskazini na maeneo mengine yanatakiwa kutumia Kituo cha Mabasi cha Magufuli, huku yanayotoka Mikoa ya Kusini yakitakiwa kutumia Kituo cha Mabasi cha Mbagala.
Meneja wa LATRA Mkoa wa Dar es Salaam, Ngereza Patel amesema agizo hilo linafuatia maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ya kutaka mabasi yote kurejea katika Vituo vilivyopangwa na kuzingatia masharti waliyopewa wakati wa kupata leseni za usafirishaji.
Patel amesema kwenda kinyume na utaratibu huo ni kuvunja Sheria na masharti ya leseni, hivyo amewataka Wamiliki na Waendeshaji wa mabasi kuzingatia Vituo vilivyotengwa kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria ili kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria.
Soma pia Wamiliki wa mabasi wapewa wiki moja kurejea stendi ya Magufuli
M naona hujaelewa kwa hiyo wewe basi likubebe mtaani halafu wengine wakwame kwenye foleni kisa mabasi yamezagaa mjini.Hakuna mtu anapinga stand ya magufuli
TATIZO, HATUNA MIUNDO MBINU YA KUPELEKA WATU STAND NA KUWARUDISHA MAJUMBANI
KARNE HII; ULIMWENGU UNA ANGALIA KURAHISISHIA WATU MAISHA NA SIO KUWAONGEZEA UGUMU WA MAISHA
Kipindi kile stand hiyo inafanya kazi kila nikifika dar; nilikuwa naishia kwenda na boda ili nisikose basi sasa tabu zote za nini?
MUDA NDIO KILA KITU KATIKA MAISHA; KWA NINI UFIKE NYUMBANI SAA MBILI USIKU KAMA UNAWEZA KUFIKA SAA KUMI NA MOJA NA NUSU?
Kwa wenzetu huko centra bus station zina ring road za treni za umeme; sisi unategemea bajaji na mwendo kasi ambao hata haupakii mizigo ya abiria???
M naona hujaelewa kwa hiyo wewe basi likubebe mtaani halafu wengine wakwame kwenye foleni kisa mabasi yamezagaa mjini.
Huo uharaka unausema wewe ni upi wa kwenda na dunia ya sasa kama tutaruhusu msongamano mkubwa wa magari katikati ya mji.
Moja ya sababu mabasi kuishia Magufuli ni kupunguza msongamano mambo mengine yaende faster.
Hatuwezi kuchelewesha mizunguko katikati ya mji kisa mtù mmoja anaenda mpanda anataka basi limfuate chanika
Huko Magufuli barabara ni pana. halafu foleni huko itokee ya kwenda wapi?BASI 6 KWENDA KIGAMBONI, AU BASI 5 KWENDA GOMS, KWA MFANO ZINAONGEZAJE FOLENI?
JE BASI 120 KUCHUUA BARABARA MOJA KWENDA MAGUFULI, NI ZIPI ZINAONGEZA FOLENI?
Acha basi ubishi wa darasa la pili......
Nashauri mamlaka za Mkoa zifanyr maamuzi kwa kuzingatia ukweli na jografia ya Dar.Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imewataka Waendeshaji wa mabasi Jijini Dar es salaam kuzingatia utaratibu wa kupakia na kushusha abiria katika vituo vilivyopangwa na Halmashauri.