LATRA: Mabasi yote yaishie Stendi ya Magufuli na Mbagala

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imewataka Waendeshaji wa mabasi Jijini Dar es salaam kuzingatia utaratibu wa kupakia na kushusha abiria katika vituo vilivyopangwa na Halmashauri.

Kwa mujibu wa LATRA, mabasi yanayotoka Mikoa ya Kaskazini na maeneo mengine yanatakiwa kutumia Kituo cha Mabasi cha Magufuli, huku yanayotoka Mikoa ya Kusini yakitakiwa kutumia Kituo cha Mabasi cha Mbagala.

Meneja wa LATRA Mkoa wa Dar es Salaam, Ngereza Patel amesema agizo hilo linafuatia maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ya kutaka mabasi yote kurejea katika Vituo vilivyopangwa na kuzingatia masharti waliyopewa wakati wa kupata leseni za usafirishaji.

Patel amesema kwenda kinyume na utaratibu huo ni kuvunja Sheria na masharti ya leseni, hivyo amewataka Wamiliki na Waendeshaji wa mabasi kuzingatia Vituo vilivyotengwa kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria ili kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria.

Soma pia Wamiliki wa mabasi wapewa wiki moja kurejea stendi ya Magufuli

Your browser is not able to display this video.
 
Wajengee stand nyingine zaidi ya 3
Haiwezekani mji mkubwa wenye watu milioni 7, wategemee stand Moja tu?

Mwanza ambalo ni jiji la pili, lina stand mbili Nyamong'olo na Nyezegi.

Halafu dar tutegemee Moja tu kama chupa ya chai,

Kigamboni kuwe na stand
Mbagala kuwe na stand
Chanika kuwe na stand
Tegeta iwepo

Inahitaji barabara ya ring road, ili basi ziweze kuizunguka bila kuingia mjini.

Na sio kulazimisha inconvenience kwa wasafiri bila sababu.

Gharama zinaongeza kwa sababu ya umbali na shida ya usafiri
 
Kipindi mabasi yapo ubungo mbona mlikuwa hamlalamiki yaje.huko kigamboni
Acha mazoea
Mbona uzungumzii stand ilipokuwa mnazi mmoja.

Shida ni umbali
Shida ya usafiri
Ongezeko la gharama

Jiji limekuwa na kutanuka vibaya mno
Wakati wa Ubungo, Chamazi palikuwa shamba, Leo hii?

Zinahitajika stand zaidi ya nne ndani ya jiji la Dar es salaam.

Na sio Kila wilaya Bali ni Kila jimbo
 
well done LATRA 💪
 
Bila nguvu ya ziada utemi na kusimamia sheria sawa sawa hili halitakaa liwezekane..
Mtani, Nyumba za Ubungo NHC ni kota za makazi, watu ni wapangaji na mmiliki wa Ardhi ni Rais kwa niaba ya Watanganyika, SAsa kama wapangaji wanabadili matumizi ya eneo bila Rukhsa ya mwenye eneo si afanye REVOCATION?

Pili, Wakati TILISHO nanunua River side, anavunja lazma kibali cha kuvunja , anajenga lazma kibali cha kujenga na leseni ya Biashara , hizo zilitolewa na mamlaka gani? Kamam mamlaka zinaogopa taharuki, basi wasubiri kila lesen inapo expire hakuna ku-renew.
wenye nyumba waizokodishia makampuni ya mabasi wapewe notice of intention to revoke tittle kwa kubadili matumizi bila kumuomba trustee ambaye ni mheshimiwa Rais.
hili jambo kwa upande wangu ni PEREPECHE and rest assured, tarehe 17 ni keshokutwa, nipo hapoa, utaniambia

Hakuna gari itaende huko Mbezi, labda zile ngarangara tu .
SPECIAL HIRE wamechukua maeneo yote ya wazi, wanapaki na watoto hawana pa kucheza, hili nalo i tatizo?

Leo 17-8-2028 wamiliki pale Shekilango upande wa Urafiki ndio kwanza wanaboresha ofisi zao.

Ally Star yeye kanunua kabisa nyumba 5 pale Mwembehai, kajnega hoteli na hapo hapo kituo chake, naye aende mbezi?

Mshana Jr tutarudi kwenye huu uzi baada ya wiki ujue nguvu ya akili za mtaani na wale wenye vyeti vya makaratasi wanaoitwa washauri na mafisa biashara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…