LATRA: Mabasi yote yaishie Stendi ya Magufuli na Mbagala

Tatizo wanasolve tatizo sio chanzo, jamaa wajinga sana imagine haohao latra wametoa vibali kwa baadhi ya kampuni kujenga stend binafsi kama ABC na allys star hio si double standard.
 
Population inaongezeka
huduma zinatakiwa ziwe karibu na watu na sio mbali na watu.....
Hivi kuna miundo mbinu ya kupela Abiria wenye mizigo na shangazi kaja, asubuhi na jioni huko magufuli?
Shida ni kwamba sijui.waafrika huwa tunawaza nini.

imagine unataka basi lifike mlangoni kwako eti kukusogezea huduma mbona huko mikoani hayo mabasi hayafik ivijijini kwenu ila Dar mnalazimisha kila mtaa uwe na stand?

Mbezi Magufuli siyo mbali ndani ya Dar within one hour mtu unafika kama foleni hamna.

Swala ni kwamba serikali incontrol foleni ili watu wafike Magufuli mapema.

Halafu wa basi analeta watu.mjjni kwa hela ileile daladala zinakosa abiria huoni kwamba ni kuua biashara.za wengine.

Mji lazima upangwe hatuwezi kuwa na vituo vya mabasi holela tu kila mtu anajiamulia anavyotaka tutakuwa taifa la hovyo
 
Kelele tu hizi, tafuteni sababu kwa nini abilia hawapendi kupandia Maghufuri,
Pale pana kelo balaa, ukifika tu unazungukwa na ma dalali kibao, kila mmoja anakupigia kelele njoo huku njoo huku, ma dalali wasio, rasmi kibao, vibaka kibao, kwa nini pasiwe na utaratibu kama Airport, hakuna ma dalali, unafika,ofisi za,mashirika ya, ndege zipo wazi, unakata tiketi, unaenda kupanda,bila ma kelele kibao!
 
M naona hujaelewa kwa hiyo wewe basi likubebe mtaani halafu wengine wakwame kwenye foleni kisa mabasi yamezagaa mjini.

Huo uharaka unausema wewe ni upi wa kwenda na dunia ya sasa kama tutaruhusu msongamano mkubwa wa magari katikati ya mji.

Moja ya sababu mabasi kuishia Magufuli ni kupunguza msongamano mambo mengine yaende faster.

Hatuwezi kuchelewesha mizunguko katikati ya mji kisa mtù mmoja anaenda mpanda anataka basi limfuate chanika
 

BASI 6 KWENDA KIGAMBONI, AU BASI 5 KWENDA GOMS, KWA MFANO ZINAONGEZAJE FOLENI?
JE BASI 120 KUCHUUA BARABARA MOJA KWENDA MAGUFULI, NI ZIPI ZINAONGEZA FOLENI?
Acha basi ubishi wa darasa la pili......
 
BASI 6 KWENDA KIGAMBONI, AU BASI 5 KWENDA GOMS, KWA MFANO ZINAONGEZAJE FOLENI?
JE BASI 120 KUCHUUA BARABARA MOJA KWENDA MAGUFULI, NI ZIPI ZINAONGEZA FOLENI?
Acha basi ubishi wa darasa la pili......
Huko Magufuli barabara ni pana. halafu foleni huko itokee ya kwenda wapi?
 
Eeh mkuu usemee, Dar ni kubwa, mabasi yaishie standi moja ni taabu kweli. Nimeona mtu akisema vituo vya kutosha, lakini utekelezaji ndio shida. Vipi na abiria wanaotoka Mbagala kwenda magharibi? Hii itachanganya sana. LATRA wajenge stendi zaidi kwanza kabla ya kusimamia hili..
 
Badala ya kila kampuni kupeleka mabasi wanakotaka
Ilikuwa ni bora kuweka Bus Terminals mpaka mijini
Mbona miji mikubwa inashusha mpaka katikati ya miji
 
Nashauri mamlaka za Mkoa zifanyr maamuzi kwa kuzingatia ukweli na jografia ya Dar.
Ndio maana hata ruhusa ya kufanya biashara usiku hapo Kariakoo walitangaza ila kiuhalisia limeshindikana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…