LATRA yasitisha leseni ya mabasi ya Katarama

LATRA yasitisha leseni ya mabasi ya Katarama

Mamlaka ya Udhibiti usafiri Ardhini LATRA imesitisha leseni ya usafarishaji kwa mabasi ya kampuni ya KATARAMA Luxury baada ya uchunguzi kubaini wamekuwa wakichezea mifumo ya udhibiti mwendo kwenye mabasi yao (VTS).
Mvunja nchi ni mwananchi, huwezi kumchukulia hatua Katarama bila kumuadhibu fundi anayechokonoa huo mfumo ambaye most likely ni mtumishi wa huko kwenye mfumo
 
Ishu itamalizwa kama ilivomalizwa ya kilimanjaro Express
 
Mamlaka ya Udhibiti usafiri Ardhini LATRA imesitisha leseni ya usafarishaji kwa mabasi ya kampuni ya KATARAMA Luxury baada ya uchunguzi kubaini wamekuwa wakichezea mifumo ya udhibiti mwendo kwenye mabasi yao (VTS).

Aidha LATRA ametoa onyo kali kwa makampuni manne ya mabasi ambayo yamekuwa yakikiuka taratibu za mabasi kusafirI usiku na kusababisha ajali za mara kwa mara akitoa wiki moja kwa uongozi wa mabasi hayo kuongeza usimamizi wa mabasi yao.

KATARAMA ameleta mashine za uhakika za iriza naona vita ya uchumi imeanza tena na ALLYS STAR
Watutamaliza hawa wasipodhibitiwa.
 
Kwa mimi naona ni figisu kwa LATRA kuifungia kampuni ya KATARAMA kwa sababu ukiangalia ni moja ya kampuni ambayo haijawahi kupata Ajali

FB_IMG_1726163014509.jpg

Mwamba anatembea sana dar Mwanza
FB_IMG_1726161514512.jpg
Kutoka Dar es Salaam Mamlaka ya Uthibiti Usafiri Ardhini LATRA imesitisha leseni ya safari ya mabasi ya kampuni ya Katarama kwa kosa la kuchezea mifumo ya mwenendo ya mabasi yaliwekwa na Latra kwenye mabasi hayo ambayo kusitishwa kwake safari yanaanza kesho.

Hayo ameyasema Leo Mkurugenzi wa Latra Habibu Suluo wakati alipokutana na wamiliki wa mabasi ya BM Coach, Super Feo, Abood Bus na Katarama Bus jijini Dar-es-salaam.

Habibu amesema Kampuni ya Bm Coach, Super Feo na Abood Bus imepewa wiki moja wamiliki wa mabasi hayo yanayofanya safari za mchana na usiku kubadilika kutokana na ajali zinazotokea siku za nyuma kwenye mabasi hayo.

ACP Nassoro Sisiwayah Mkuu wa Operesheni kikosi cha usalama Barabarani (T)amesema watafuatilia waliochezea mfumo huo wa LATRA ili kubaini wahalifu na kupelekwa mahakamani.

Kwa upande wake Omary Msigwa Mmiliki wa Mabasi ya Super Feo amesema watafuata sheria na kanuni za barabarani.

Nae Abdala Kiongozi Mwenyekiti wa Chama cha wamiliki wa mabasi TABOA ametoa wito kwa wafanyabiashara wa mabasi kuzingatia sheria na kanuni za Mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini LATRA.
 
Mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini, (LATRA) imesitisha leseni ya usafirishaji kwa kampuni ya mabasi ya Katarama kwa muda usiojulikana kutokana na kuchezea mfumo wa ufutiliaji wa mwendo huku ikitoa wiki moja kwa kampuni zingine tatu kujirekebisha na uvunjifu wa kanuni za leseni walizopewa

Kampuni hizo zilizopewa wiki moja na onyo kali ni pamoja na Bm,Super feo,Abood kwenda kurekebisha na uvunjivu wa Sheria

Akizungumza na wamiliki wa mabasi ya Abood ,Super Feo, Katarama na BM Coach leo jijini Dar es salaam,Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Habibu Suluo,amesema basi Hilo limekuwa na matukio mengi ya kuchezea mfumo huo na matukio mengi ya uvunjifu wa Sheria na kanuni walizowapatia.

Hata hivyo amesema kuwa Katarama watampa muda wa kusikiliza mmliki wake hivyo kwa kupitia uchunguzi utakaofanywa na Jeshi la polisi nchini.

Kwa upande wake, Mkuu wa operationi wa kikosi Cha usalama Barabarani, ACP , Nassor Sisiwayah, amesema kuwa watakwenda kufungua jarada la uchunguzi juu ya tuhuma zinazoikabili basi la Katarama baadaye Kuja na majibu sahihi.

Naye mkurugenzi wa mabasi ya Super Feo Omari Msingwa, amesema amepokea maelekezo kutoka Latra hivyo atakwenda kuyafanyia kazi.
 
Back
Top Bottom