Asante kwa taarifa na ushauri.
Mamlaka ya Usafiri wa Ardhini ( LATRA ) imetangaza kwamba hadi kufikia January 6 mwaka 2021 mabasi yote yawe yameanza kutumia tiketi za mtandao , vinginevyo watafungiwa kutoa huduma hiyo .
Bado haijajulikana sababu hasa za wenye mabasi ya abiria kulazimishwa kufuata utaratibu huu mpya huku wakitozwa kodi lukuki ambayo wanailipa bila mizengwe yoyote.
Tahadhari : kama una safari ya muhimu ni bora ukafanya hivyo kabla ya tarehe hiyo , maana lolote la kukukwamisha laweza kutokea .
Nakulilia Tanzania .
Naona serikali ikimalizana na mabasi itazigeukia bajaji, toyo na bodaboda.