Law school of Tanzania yapandisha ada na gharama nyingine, kutoka 1,570,000/= mpaka 2,950,000/=

Kwa nini kusiwe na chambers za watu binafsi na taasisi za sheria za umma na serikali ambako wahitimu wa sheria wawe wanaenda kupata mafunzo ya kuwa mawakili kama internship kwa mwaka mmoja, kama ilivyo kwa madaktari? Yaani hii ni sawa na mtu ahitimu degree ya udaktari miaka mitano, halafu alipe ada nyingine milioni tatu ya kwenda kusomea upya namna ya ku-practice udaktari kwenye "Doctor School" sasa ile miaka mitano alikuwa anasomea nini? makida makida, au? Haya mambo ya ukiritimba kwenye taaluma yalishapitwa na wakati, umebaki ulimbukeni tu...​
 
Awali-njia ya kuwalima wanaoenda law school ili wasi-graduate wengi ilikuwa ni alama/kuwafelisha

Sasa-wamepandisha ada ili mshindwe kwenye gharama na law school iwe na wasomi wachache lakini mwisho wa siku mtaambiwa

"wamefaulu sababu ya uchungu wa gharama kuwa kubwa lakini awali wasomi hawakuwa na uchungu sababu ya gharama kuwa ndogo hivyo walikuwa hawasomi "
 
Tumeshashauri sana humu juu ya hiyo taasisi ya kidhalimu. Hawa hawako peke yao wana baraka na nguvu kubwa ambapo kwa hali ilivyo sasa Tz hawawezi kuchukuliwa hatua zozote kuwajibishwa.

Hapo wametoa onyo sasa kuwa tunafanya tunavyotaka sisi nyie malofa mtatufanya nini?

Tume ya kidhalimu iliundwa kuchunguza taasisi ya kidhalimu, mnategemea nini?

Mateso na mauimivu hayatoisha kwa wataliwa, hadi watawaliwa wakatae kutawaliwa na kuamua wenyewe wanayo haki ya kuongozwa na siyo kutawaliwa.
 
Ifikie hatua hii taasisi isiwepo, mbona watu wa taaluma nyingine Wana Bodi zinazoratibu tu mitihani? Kwamba na madaktar wangekuwa baada ya miaka mitano wanaenda medical school mwaka mmoja, vivyo hivyo Kwa watu wa taaluma nyingine.

Labda Kwa kuwa sijui hiyo miaka minne yote wanasheria Huwa wanasoma Nini, kwamba vitu ambavyo walishindwa kuvisoma Kwa miaka minne wanaenda Tena kufundishwa mwaka mmoja, Tena Kila kozi wakifundishwa wiki 2 tu.

Lakini pia walamba asali wanadai mawakili wa siku hizi Hamna kitu, Sasa Kuna haja gani ya law school? Ni Bora kurudisha mfumo wa zamani ambao wanadai ulitupa mawakili wazuri kama kina kabudi.

Ni Bora mtu afanye internship hata miaka miwili, akapige bar exams na akifanikiwa awe Wakili kuliko kuwa na taasisi ambayo inaendeshwa kidhalimu na Kwa kulinda maslahi ya watu wachache.

Binafsi sio mwanasheria Wala sitegemei kuwa lakini najua umuhimu wa hii taasisi Kwa vijana wetu wanaotamani kufikia ndoto zao za kuwa mawakili
 
Sasa kwani lazima usome sheria someni hata Mechanics au logistics mbn zinapesa nyingi kuliko hata iyo sheria...
Kwahio kama sio lazima kusoma sheria ndio ada ipandishwe kihohela?,Je umewafikiria vijana ambao tayari wamesoma sheria na wengine wako chuoni na wote wanategemea kufanya hio mitihani,unapopandisha ada maradufu unalenga nini?
 
Profession zote zina certification boards ambazo lazima ufanye mitihani kuwa certified

Unajua kwa nini ? kila chuo hutoa degree ok fine lakini kujua mhitimu huyo yuko vizuri kwa level hiyo ili asingie ku practice akiwa hovyo sokoni ndio unakutana na mitihani mingine hiyo ukipenda waweza national examination ile ya degree ulipata ilikuwa local examination ya chuo husika tu

Chuo kikuu mwaweza kuwa mlikuwa mnagawiana tu degree kivumbi kitakuja kuonekana kwenye mitihani ya bodi husika au hiyo law school ambayo hupima hao wasoma sheria kwa mitihani ya kitaifa ya law school
 
Mitihani hamna anaeikataa, ni muhimu sana katika ku set standard, kusingekuwa na tatizo kama baada ya mtu kumaliza degree ya kwanza then anafanya internship hata mwaka then anafanya mtihani Ili awe certified.

Changamoto ya law school ni kwamba wanajidai kama vile wanaanza kufundisha upya tena Kwa gharama kubwa sana na inalipwa Kwa mkupuo mmoja,

Bodi nyingine za kitaaluma zinachofanya ni kuandaa mitihani,Kwa hiyo gharama inakuwepo kwenye kulipia mtihani tu, kujiandaa utajua mwenyewe unaweza jisomea hata Kwa kuunga unga kitu ambacho Kwa law school hakipo.

Tuzungumze yote lakini Kwa familia nyingi za kitanzania kuweka ada kiasi Cha Karib 3M kwenye taasisi ya umma tena Kwa mkupuo mmoja hakikubaliki.
 
Application fees. 20,000/=
Admission fees 20,000/=
Registration fees 20,000/=
Identity card 20,000/=



[emoji81][emoji81][emoji81] hii nchi ngumu sana
 
Application fees. 20,000/=
Admission fees 20,000/=
Registration fees 20,000/=
Identity card 20,000/=



[emoji81][emoji81][emoji81] hii nchi ngumu sana
Kenya law School funga kazi

Fees tu ni sawa na hela za Tanzania shilingi 5,180,000 hapo bado gharama zingine
 
Application fees. 20,000/=
Admission fees 20,000/=
Registration fees 20,000/=
Identity card 20,000/=



[emoji81][emoji81][emoji81] hii nchi ngumu sana
Tanzania iko cheap kuliko Kenya

Kenya cost yake ya admission fee ni sawa na shilingi za Tanzania 160,000 za Tanzania
 
dah, Mungu awasaidie watoto wa maskini nchini kwetu, hiyo ada mimi ndio nalipia mtoto wangu wa chekechea, namshukuru Mungu kwa hili. nadhani kwa vyuo hivyo hasa vinavyolazimisha watu kusoma disploma ya profession kama (CPA na law school), wazingatie mahitaji ya watoto wa vijijini, hawana uwezo kulipa hiyo hela na hadi kufika hapo ni muujiza. na pale law school bado hujasumbuka na ufaulu, wanabana sana, bora sisi miaka yetu tulikuwa tunaenda bar exam haihitaji ada. pale wanabana sana na kuna tuvijana hatujui kitu ila tunanyanyasa sana watu. kwisakwisa, kita na wengine, tukikutana nao wana uelewa mdogo sana wa practice ila wanawanana sana watoto.
 
Pengine ndio maana bunge limefanya mabadiliko!Hakuna haja ya kila mwanasheria kupita LST.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…