Lawama zote za umeme ziwaendee Kitila Mkumbo na Nehemiah Mchechu

Kitila Mkumbo na Nehemiah mchezhu ndiye wenye jukumu la mashirika ya umma kwa sasa.

Manara si wa kwanza wala hatakuwa wa mwisho kulalamikia umeme Tanzania hii.

Ninachokishauri hapa ni utatuzi wa tatizo wa kudumu, siyo wa zima moto.

Hata ufukuze Tanesco nzima uiete mpya, yatakuwa yake yake. Shirika limekuwa kubwa kuliko uwezo wetu.

Ni lazima likatwe likatwe. Hakuna ujanja mwingine uliobakia amabo haujafanywa bado.
 
Tatizo la umeme ni utendaji mbovu wa Mkuu wa nchi hasa pale alipomteua January kuongoza Wizara asiyoiweza na kupelekea kuzalisha matatizo tunayoyaona leo.

January alipoongoza Wizara ya Nishati badala ya kuendeleza mazuri ya Kalemani akaanza kuchomoka marafiki zake kina Maharage sijui kunde.

Leo tunalala giza tunaamka giza kila siku visingizio kede kede.

Pamoja na matatizo yote anatokea waziri mpuuzi eti anatuambia Waalimu wote wa shule za serekali na Binafsi eti wamemchukulia fomu mama !.

Ukweli mchungu nchi imeshamshinda siku nyingi kabakiza wapambe wajinga kama wewe.

Kila siku anazurura huko kwa waarabu na misafara mikubwa na kuwauzia Bandari na misitu yetu.
 
Like seriously kwenye kichwa chako unaamini una hoja.

Embu tutajie source za umeme kile mkoa?
Kijana source unamaanisha vyanzo vya umeme au siyo?

Haijalishi, shirika la umeme la mkoa ndilo litakalojuwa umeme waake inaugtowa wapi, iwe inaununuwa kutoka mkoa mwengine, nchi nyengine, inafuwa wa jua, wa maji wa nuclear, haijalishi.
 
Ningependa utoe ufafanuzi kuwa kulivunja vunja shirika katika kufanya kila mkoa ujitegemee.je hiyo mikoa itakuwa inazalisha huo umeme kupitia vyanzo vipi vya umeme? Je umiliki utabaki kwa nani? Ni serikali au Secta Binafsi? Kama ni serikali huoni vyanzo vya kuzalisha umeme vitabakia ni hivi hivi ambavyo ndio vimekuwa kiini cha changamoto hii ya umeme wa mgao kutokana na upungufu wa maji ya kutosha kuzalisha umeme katika mabwawa yetu? Kama ni Secta Binafsi huoni itakuwa ni jambo la hatari kwa Taifa na usalama wa Taifa letu kukabidhi watu binafsi Secta nyeti ya nishati bila utafiti na maandalizi ya kutosha? Kama shida na usimamizi kama ulivyosema jana kwenye uzi wangu .je huoni mambo yatakuwa ni yale yale kama ambavyo tumeshuhudia baadhi ya miradi ya serikali ikikwama huku mikoani kuendelea nakuanza haraka pale panapotokea ziara za viongozi wakuu kitaifa kama vile Rais ,makamu na waziri Mkuu?
 
Alie wateua hana macho wala masikio ya kuona kinacho endelea? au wamemuroga? sikiliza Raisi ndie wa kubeba lawama
Ana macho yanaona sana na ana masikio yanasikia sana, ndiyo maana akawateua Kitila na Msechu wayasimamie mashirika yasiyofanya vizuri.

Lawama ziwaendee wao, ndiyo wenye majukumu ya mashirika ya umma kwa sasa, zisiwaendee wengine.
 
Nenda kwenye point, Makamba kaiua TANESCO kwa ufisadi wake
Makamba na Maharage wawajibike kwa mkataba wa mabillioni ya shilingi walioingia na wahindi kununua software bila kufanya uchunguzi wa nini kinasababisha huduma duni za Tanesco!
Matatizo ya Tanesco ili kuyatathmini ni lazima uyagawe katika makundi matatu. Makindi hayo ni; Uzalishaji, usafirishaji na usambazaji. Hitilafu ikitokeo kwenye moja ya shuhuri hizo lazima kutakuwa na mgao wa umeme!
Mara nyingi hatuambiwi ukweli kuwa tatizo liko wapi ndio maana mara watasema hakuna maji ya kutosha hata wakati wa masika! Mara utaambiwa vinu vya kuzalisha umeme vinakarabatiwa; siku nyingine utaambiwa system ya Luku imekorofisha.
The only viable solution to the Tanesco problem is not privatization as some in planning commission would propose ( especially those Brokers within the commission) but to divide it into three separate entities namely;
Generation
Transmission and
Distribution.
Hapo itakuwa rahisi kuyagundua matatizo na kuyatafutia ufumbuzi. Tanesco as it is now is too big!
 
Wawe na mwaka au wawe na mwezi mmoja, jiulize wewe ambae upo "deep" waliwekwa kufanya kazi gani zaidi ya kuweka sawa mashirika ya umma yasiyotenda ipasavyo?

Nahitaji jiu ya hilo swali kutoka kwako uliye "deep".
Kaisome 10 years roadmap ya tanesco..
hiyo roadmap ina kila reform ya kuitoa tanesco kwenye mkwamo

Reforms ni marathon, sio sprinting

Rudi kwenye siasa
 
chuki binafsi zinachakaza nafsi yako harooo..
Naona umekosa hoja. Unaniingia binafsi, ubinafsi wagu unakuhusu nini? Jibu hoja wachana na mimi binafsi, hunijuwi sikujuwi.
 
Kaisome 10 years roadmap ya tanesco..
hiyo roadmap ina kila reform ya kuitoa tanesco kwenye mkwamo

Reforms ni marathon, sio sprinting

Rudi kwenye siasa
Hakuna cha roadmap wala ushuzi, watu wanataka umeme hawataki porojo. Hiyo roadmap ukute hata huyo mjinga aliyeiandika hayupo tena.

Ethiopia wametoka kwenye janga la vita vya muda mrefu, wametoka kwenye njaa na umasikini wa mwisho duniani na kwa muda mfupi wameweza, sisi tumelala wapi?
 
Kama Tanesco ni shirika niyeti haliwezi kupewa private sector kwa sababu za kiusalama Mbona Bandari mmekubali kuwapa DpWorld kwani Bandari sio nyeti kwa sababu za kiusalama?
 
Sisi tunachatoka ni umeme, awe mfuata Mkumbo, Mchachu au yeyote. Tumechoka umeme kuwa bidhaa ya anasa, tumechoka kelele na gharama za majenereta.
 
Kijana source unamaanisha vyanzo vya umeme au siyo?

Haijalishi, shirika la umeme la mkoa ndilo litakalojuwa umeme waake inaugtowa wapi, iwe inaununuwa kutoka mkoa mwengine, nchi nyengine, inafuwa wa jua, wa maji wa nuclear, haijalishi.
Source za umeme ni zifuatazo

Main stable sources ni carbon (mafuta, coal, or gases). Embu tueleze mikoa ambayo aina uzalishaji huo uwekezaji wa kujikimu ki mkoa tu hela watatoa wapi kwa mapato given the mega watts demands, who to fund the infrastructure ya kusambaza umeme mkoa mzima, how will the retail work.

Kama ni umeme wa vyanzo vya maji mikoa mingapi ina vyanzo, again gharama za plant, vituo vya kupokea umeme, kusambaza umeme na hizo hela wanatoa wapi.

Just give a clue strategically how would your proposal work sio hadithi za alinachs.
 
Wewe wacha ku complicate mambo, unataka tuingie kwenye physics saa hiizi.

Kwani umeme unaotumia wewe nyumbani kwako unazalisha wewe?
 
Hao wameshindwa ( kwa muono wako) wameshaondolewa, wanahusika nini hivi sasa?

Mwenye majukumu ya mashirika ya Umma nani?
Makamba na Maharage wanatakiwa kupelekwa mbele ya kamati maalum ya bunge kueleza nini kimetokea kupelekea hali mbaya hivi ya umeme, wanapaswa kuwajibishwa.
 
Wazo lako ni zuri.Hata hivyo, Sidhani kama linatekelezeka katika mazingira ya nchi yetu kwa kuwa ni mikoa michache tu ambayo ina vyanzo vya umeme vinavyojitegemea vyenye uwezo wa kukidhi mahitaji ya nishati ya Umeme kwenye mikoa husika.


Mikoa mingi ni tegemezi kwa mikoa mingine kwenye vyanzo vya nishati ya Umeme ,Hivyo, kwa maoni yangu ni kwamba "Centralised Management" ya umeme katika nchi yetu bado ni "crucial" na inabidi iendelee ili kuepuka "total blackout" kwa baadhi ya mikoa na gharama kubwa ya nishati ya umeme.

Kinachotakiwa kufanyika kwa sasa ni kuona namna bora ya kuendelea kuboresha miundombinu ya uzalishaji na usambazaji wa umeme , kuhakikisha TANESCO inakuwa na Uongozi na Watumishi wenye uzalendo na weledi usio tiliwa mashaka.

Nawasilisha,

Article.
 
Tanesco ianze kubomolewa kimikoa. Kila mkowa uwe na shirika lake la Umeme la kujitegemea, tuuziane umeme kimkoa. Simple and straight foreward solution.
Mikoa hii hii ambayo hata kutengeneza madawati tu inakuwa ngoma nzito, wataweza kuzalisha kusambaza umeme?

TANESCO kama kwa umoja wake imekuwa kasheshe kuendesha vipi kuliwa na viTANESCO vingi vingi si ndo itakuwa hatari? Sioni tija itapatikana vipi kwa TANESCO kugawanywa kimikoa.
 
Hahah unataka kusema FaizaFoxy kaandika upuz mtupu au

Ova
 
Naona unajichanganya tu, nisome tena, nasema kila mkoa uwe na shirika lake la umeme. Nini huo mkoa inafanya na umeme itaununua mkoa upi au itauuza mkoa upi itakuwa ni jukumu la huo mkoa.

Haihitaji rocket science kuelewa niliyoyaandika.
Nini maana ya shirika.

Kuna shirika ambalo unalolojua alizslishi?

Let’s give the benefit of the doubt.

Let’s say kuna kwenye umeme shirika limejikita kwenye ku supply umeme (retailing) mkoa gani utawajengea infrastructure ya kusambaza huo umeme, ku maintain hizo infrastructure na mkoa gani utawazalishia huo umeme wa uhakika, kwa vyanzo gani, huo mkoa uta charge kiasi gani upate faida ya umeme, uta charge kiasi gani ku-maintain infrastructure za umeme.

Bila ya regulator wa kusdhibu umeme kukatika hovyo, wanaokuuzia wakishindwa kukupa umeme; una majibu gani kwa wateja wa mkoa.

Unajiropokea tu with little understanding to how things work.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…