Tundu alisema yeye kazi yake kashamaliza kazi yake sasa ni zamu ya wananchi kuandamana. Akaongeza pia ameshawasliana na bobu ili awasilishe malalamiko yenye ushahidi ICC
Haya maneno ya Tundu yanafikirisha sana.
Kwanini Tundu hakusema sisi wananchi wa Tanzania tunaandama?
Kama kiongozi hakuweka mipango kuhusu hayo maandamano kwamba yanafanyikaje?
Nani anatakiwa kuorganise hayo maandamano?
Yanaanza lini? wapi? na yatafanyika kwa muda gani?
Tundu ameanza kuwajua watanzania kidogo, ila bado anataka kuwatumia kwa maslahi yake binafsi ili aendelee kuichafua nchi.
Wananchi hawawezi kuandamana kwa kushurtishwa, wala kwa kumsaidia Tundu kutimiza malengo yake binafsi.
Wananchi huandamana pale wanapokua wameonewa na Hilo huwa hawaambiwi, hawakatiziki wala hawazuililiki
Watanzania tumeamua kwenda na John Pombe Magufuli Tundu, Maalim na magenge yao waheshimu maamuzi yetu