Lazaro Nyalandu arudi rasmi Chama cha Mapinduzi akitokea CHADEMA

Lazaro Nyalandu arudi rasmi Chama cha Mapinduzi akitokea CHADEMA

Fisadi limerudi kwa mafisadi wenzake.
Lazaro Nyalandu wa CHADEMA amerejea CCM kupitia mkutano mkuu wa CCM leo jijini Dodoma.

Nyalandu aliyekuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA amesema walikuwa wamechukuliwa na walilazimishwa kumwimbia bwana lakini wao pamoja na mzee Lowassa, Sumaye na Dkt. Slaa wamegoma kuimba kwani bwana yuko CCM peke yake.

Nyalandu ameiomba radhi CCM na amewashukuru kwa kumpokea tena.

Kadhalika mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Lindi Dkt. Suleiman Methew naye amerejea CCM alikokuzwa kisiasa.

Kazi Iendelee.

Sawa kabisa
Mmeshindwa kuwa na taasisi Imara halafu unadhani katiba ndiyo ije iimarishe Chama chenu?

Katiba haina uhusiano na M/kiti Chama chako, haina uhusiano kabisa na maswala yenu ya ndani ya Chama, katiba inahusu mambo ya nchi kisheria, Pambane na Chama chenu
 
Chama cha kikanda hicho, ntawashanga akina salum mwalimu, lissu n.k wakiendelea kukaa pale
 
"Wale waliotuteka walituambia tuwaimbie wimbo wa Bwana, nasi tukawajibu tutaimbaje wimbo wa Bwana katika nchi ya utumwa ?" Lazaro Nyarandu wakati akirejea CCM leo katika mkutano mkuu wa CCM uliompitisha Mh Raisi Samia Suluhu Hassani kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa. Akisisitiza usemi huo Nyalandu amesema wimbo wa Bwana hauimbiki katika nchi ya ugeni.
 
Mwenye akili timamu hawezi kukaa meza moja na Lissu
CDM kinachoiua ni uongozi mbovu na busara ndogo ya kushughulikia mambo lakini pia kujua namna ya kuemdesha siasa komavu siyo za harakati. Hawajifunzi hata cov 19 wote wanakwenda CCM soon.
 
Lazaro Nyalandu wa CHADEMA amerejea CCM kupitia mkutano mkuu wa CCM leo jijini Dodoma.

Nyalandu aliyekuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA amesema walikuwa wamechukuliwa na walilazimishwa kumwimbia bwana lakini wao pamoja na mzee Lowassa, Sumaye na Dkt. Slaa wamegoma kuimba kwani bwana yuko CCM peke yake.

Nyalandu ameiomba radhi CCM na amewashukuru kwa kumpokea tena.

Kadhalika mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Lindi Dkt. Suleiman Methew naye amerejea CCM alikokuzwa kisiasa.

Kazi Iendelee.

FURSA
 
Back
Top Bottom