Ni kweli, hivyo ndio inavyotakiwa iwe, ila watanzania 80%+ ya wapiga kura hawachagui kwa kuangalia sera, bali ushabiki, rushwa, vitisho na mazoea. Ukisema mtu anasema amechaguliwa kwa sera zake, basi ujue ni porojo kama porojo nyingine. Mfano ule uchaguzi wa kihayawani uliopita, unaweza kusema ilikuwa ni kwa ajili ya sera? Na kwa bahati Precidence aliyetengeneza Magufuli ya kushinda uchaguzi kwa kuunajisi, itachukua muda kuondoka maana ccm imeshapoteza ushawishi kwa umma, na haiko tayari kuachia madaraka kidemokrasia.