Lazaro Nyalandu: Tatizo kubwa la CHADEMA ni Uongozi wa juu, CCM imejaliwa mfumo

Lazaro Nyalandu: Tatizo kubwa la CHADEMA ni Uongozi wa juu, CCM imejaliwa mfumo

omtiti

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2019
Posts
1,022
Reaction score
1,591
Akiwa 360 Clouds ameliongea hili leo na yuko live mpaka sasa, anasema tatizo lipo kwenye uongozi. Amesema wanachama wa chini kabisa hawana tatizo kabisa, matumaini yao yanaharibiwa na uongozi wa juu.

Angalizo: Mbowe uongozi wako umeshindwa vibaya sana, achia ngazi

=======

“Nilipoenda nchi ya ugenini (CHADEMA) wimbo ulikuwa haumbiki kwa namna ambavyo nilikuwa naangalia matukio, ilipotokea Mheshimiwa Rais anaumwa kuna baadhi ya viongozi walijitolea wakasema huyu hafai aondoke tufurahi, ilikuwa inanikwaza kupita kiasi”

“Niliposafiri kwenda Chato kuzika mashambulizi ambayo yalikuwa yananipata, hayakutoka kwa wana-CCM, hayakutoka kwa wana-CHADEMA wa kawaida, yalitoka kwa baadhi wenye msimamo mkali, unamshambuliaje mtu alieenda kuzika kiongozi wake wa nchi?"

“Wakati wa matatizo ya Lissu mimi binafsi sikujali kwamba ni CHADEMA, nilimuona ni Mtanzania ni kiongozi mwenzangu kule Singida, nakumbuka hata Mhe Rais alienda pia kumuona. Lakini wanachama wa CCM kuanzia Rais hadi viongozi hakuna aliepiga simu au kututukana”

“Kuna mitihani ilitokea kwenye uchaguzi, kulikuwa na chaguzi za aina mbili, moja ilikuwa kupigiwa kura kwenye kamati, tunaenda kwenye Baraza Kuu. Kwenye Kamati Kuu Nyalandu alipata 100%, nilimgaragaza kweli kweli, kilichotokea viongozi wakasema Nyalandu asije akawa kama Lowassa”

“Uchaguzi wa mgombea ubunge Singida Kaskazini, wajumbe wamefika usiku ule kuanzia saa kumi na mbili watu wananipigia simu wananiambia mbona mgombea Urais wako hakutaki anasema kidogo umkoseshe kugombea Urais kule Dar es Salaam”

“Wana-CHADEMA watu wa kawaida wengi ni watu wazuri, ni watu ambao wanatamani nchi bora, ambacho wanawazidi wana-CCM wewe itisha mkutano watakuja kwa mguu, watatoka walikotoka, watajitolea katika hali ambayo hutoamini”

“Siasa sio matusi, siasa sio kukoseana heshima, sio kutukana kiongozi wa nchi, siasa sio kuwatukana wale unaotofautiana nao, ni kusema hoja zako mbadala”

“Chama Cha Mapinduzi kimejaliwa mfumo, kilivyotengeneza itifaki ya chama, namna ambavyo walitengeneza mfumo wa kutoa dukuduku zako, mfumo wa kuchaguana. Kina strength ya mfumo, naamini imani ya watu tukipeleka kwa public, mwananchi wa kawaida anatoa kura” -
 
Akiwa 360 Clouds ameliongea hili leo na yuko live mpaka sasa,anasema tatizo lipo kwenye uongozi.amesema wanachama wa chini kabisa hawana tatizo kabisa ,matumaini yao yanaharibiwa na uongozi wa juu.
Angalizo,Mbowe uongozi wako umeshindwa vibaya sana,achia ngazi
Tatizo la Chadema ni uongozi, tatizo la CCM ni nini? hadi ukakimbia uko na kuacha ubunge?
 
Nchi hii Dictator number 1 ni Freeman Aikaeli Mbowe huyu siku Mungu akimuita utazuka ugomvi mkubwa sana wa kugombea madaraka Chadema kati ya familia ya na ukoo wa Mbowe na wanaharakati uchwala kina Lissu na wenzake.
Huyu Nyalandu alimkimbia jiwe! lililotaka kumsaga saga kwa kushiriki ujambazi wa mali asili zetu! CDM walikukaribisha kukuepusha na mkono wa jiwe ili akikufuata useme ni SIASA. Unatakiwa uwashukuru.
 
Akiwa 360 Clouds ameliongea hili leo na yuko live mpaka sasa,anasema tatizo lipo kwenye uongozi. Amesema wanachama wa chini kabisa hawana tatizo kabisa ,matumaini yao yanaharibiwa na uongozi wa juu.

Angalizo: Mbowe uongozi wako umeshindwa vibaya sana, achia ngazi
Vp ameelezea sababu ya kwanini aliondoka CCM mkuu.

Ova
 
Akiwa 360 Clouds ameliongea hili leo na yuko live mpaka sasa,anasema tatizo lipo kwenye uongozi. Amesema wanachama wa chini kabisa hawana tatizo kabisa ,matumaini yao yanaharibiwa na uongozi wa juu.

Angalizo: Mbowe uongozi wako umeshindwa vibaya sana, achia ngazi
Baada ya kukosa alichokitaka? Yeye alisaidia nini kwenye uongozi alipokuwa ndani ya chadema? Amerudi alikotoka atulie na aendelee na mipango yake.
 
Chadema mmafanyaga makosa sana kuchukua oil chafu toka ccm. Mkimaliza kuisafisha wanawaachia uchafu wanarudi ccm na kuanza kuwachafua.

Nyalandu
Sumaye
Lowassa
Lembeli
Next tym wakija msiwape uongozi wowote. Wawe wanachama wa kawaida.
 
Akiwa 360 Clouds ameliongea hili leo na yuko live mpaka sasa,anasema tatizo lipo kwenye uongozi. Amesema wanachama wa chini kabisa hawana tatizo kabisa ,matumaini yao yanaharibiwa na uongozi wa juu.

Angalizo: Mbowe uongozi wako umeshindwa vibaya sana, achia ngazi
Nyalandu ndie aliyeshindwa, kwani alifata kuongoza!! Wanasiasa wengine bora wakanyamaza, mtu mpaka kagombea ubunge hakuona hilo. Sumaye, Lowassa, Nyalandu, Mashinji nk. Wote walikimbilia huko..waliona panafaa. Walipokosa uongozi hapafai!
 
Back
Top Bottom